OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 49,238
- 103,907
Moja kati ya makosa makubwa yaliyowahi kufanyika nchi hii ni kumpa Jakaya Kikwete madaraka ya uraisi. Pamoja na mapungufu makubwa aliyoonyesha kiungozi bado aliingiza familia nzima katika urais huku wakipigana vikumbo kutafuta fursa na kujipenyeza.
Mengi yanajulikana, lakini kinachoniuma zaidi ni familia yake kupeleka hoja ya kuwalipa pensheni wake wa viongozi. Kwa wasiofahamu hoja hii ilipelekwa bungeni na Mama Salma Kikwete ambaye ni mke wa Rais Kikwete. Hiki ni kiwango kikubwa zaidi cha tamaa zaidi hata tamaa ya fisi. Bila shaka hiki ndio legacy anayoacha Kikwete kwa familia yake, kutotosheka.
Pamoja na kufuja rasilimali za nchi katika kipindi chake, pamoja na mauwekezaji rasmi na yasiyo rasmi katika familia yake bado watu hawa hawatosheki?
Familia inakosa utu kabisa. Nchi ina ukata kutwa kuchwa kupokea misaada. Lakini kuna watu baba raisi, mama mbunge, kaka waziri bado hawatosheki wakaja na pensheni kwa wake wa viongozi.
Familia hii haikuona kabisa pesheni ndogo wanazolipwa watumishi wa umma, pengine ipeleke hoja bungeni na kutia ushawishi kwa Rais. Haikuona mishahara midogo yenyewe ikaona walichonacho waongezewe maradufu.
Kuna wakati Rais Magufuli alionyesha chuki ya wazi kwa Kikwete, pengine alichukia sana tamaa za Kikwete na familia yake.