Makoye Matale
JF-Expert Member
- May 2, 2011
- 6,491
- 2,104
Polisi zingatieni haki za binadamu maana yaliyoandikwa hapa hayatekelezwi nanyi vijana wa CCP Moshi.
Raia ana haki ya kujua elimu ya anayemkamata
- Raia ana haki ya kumwomba askari ajitambulishe kwako.
- Mwulize jina lake
- Mwulize namba yake ya uaskari
- Raia ana haki ya kujulishwa kwanini anatiliwa mashaka ama kukamatwa.
- Raia ana haki ya kuwajulisha ndugu, jamaa ama sehemu anakofanyia kazi kwamba ama amekamatwa na polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa.
- Raia ana haki ya kuomba na kupewa dhamana wakati akiwa kituo cha polisi ama Taasisi ya kuzuia rushwa.
- Hutakiwi kutoa fedha kama dhamana uwapo kituo cha polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa, isipokuwa maelezo utakayoandika.
- Raia ana haki ya kuwaeleza polisi ama Maafisa wa Kuzuia Rushwa kwamba lolote atakalosema linaweza kutumiwa kama ushahidi mahakamani, na asiburuzwe kuandika tu.
- Raia ana haki ya kuomba Wakili wake awepo kituo cha polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa wakati anatoa maelezo yake.
- Raia ana haki ya kuyasoma kabla ya kutia sahihi yake.
- Raia ana haki ya kudai risiti ya orodha ya vitu vyake/fedha zake alizozitoa ama kukabidhi kituo cha polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa.
- Raia kama ni mwanamke ana haki ya kupekuliwa na polisi wa kike, na iwapo hakuna polisi mwanamke, basi mwanamke yeyote na vile vile kwa mwanamume.
- Raia ana haki ya kufikishwa mahakamani katika muda usiozidi saa 24 tangu alipokamatwa na kufikishwa kituo cha polisi.
Kama siridhiki na namna nilivyotendwa na polisi naweza kulalamika kupitia channels zipi? Kufungua shauri kawaida unaanzia polisi, je shauri la kumshtaki polisi linaanzia wapi?
Raia ana haki ya kujua elimu ya anayemkamata
Asante,wabheja, sancho mukwai,tuhongise,sante kalesa,dankie,aika, mwalemi,enaa, wasalipa!
Polisi wakisha kukamata unakuwa wewe tena huna haki. Wao ndio wenye haki kwako wewe haswa hizi Nchi za Afrika zote. Afrika hakuna Haki za kibinadamu Polisi hana haki ya kukupiga akisha kukamata lakini wapi Afrika yetu Polisi ndio wamegeuka wao ndio Mahakimu badala ya Mahakimu wenyewe.Hizo haki na nyingine nyingi tu Zinavunjwa kila leo na polisi. Ama kwa makusudi ama kwa wao polisi kudhani wako juu ya sheria. Kwa nchi kama Tanzania Polisi hujifanya mahakimu. nitajie aliywahi kulalmikia kuhusu unyanyasaji wa polisi na akashinda! sana sana polisi wakibaini mwenzao kacheza Faul basi ni quick transfer! Hayo labda ughaibuni. Maana Polisi waweza kuwakoromea mpaka wakaingia mitini!! as afar as wakigundua kuwa kuwa wajua haki zako. Jifanye kujua hakia zako katika vituo vya Polisi Tanzania uone vijana wa Said Mwema watakavyokurarua na virungu!!