Jua haki yako unapokamatwa na Polisi

Mkuu asante sana kwa hii kitu, wengine tukiona tu magwanda ya hawa 'watu' huwa hata hatujui tufanyeje
 
Very usefull, wish leo nirudi home (Tanzania) halafu polisi anikamate ndio atajua nitakavyomuoji kabla yeye ajanikamata. U know sometimes polisi wanaonea sana hawa jamaa. Juzi nasikia vurumai ya Mbeya Jeshi la Wananchi (JWTZ) limempora mfanyabiashara blackberry. Jamani kama mishahara haitoshi acheni kazi.................
 
Hapa Tanzania!

Nikitaka kwenda kuabudu najua kuwa nitakwenda Msikiniti au Kanisani!

Nikuugua nikitaka kwenda kupta huduma ya Afya nitakwenda Hospitalini!

Nkitaka elimu nitakwenda Shuleni kwa njia ambayo inaelewaka na kufahamika waziwazi!
SWALI?

Nikitaka kujua haki zangu zote niende wapi?
 
  • Raia ana haki ya kumwomba askari ajitambulishe kwako.
    • Mwulize jina lake
    • Mwulize namba yake ya uaskari
  • Raia ana haki ya kujulishwa kwanini anatiliwa mashaka ama kukamatwa.
  • Raia ana haki ya kuwajulisha ndugu, jamaa ama sehemu anakofanyia kazi kwamba ama amekamatwa na polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa.
  • Raia ana haki ya kuomba na kupewa dhamana wakati akiwa kituo cha polisi ama Taasisi ya kuzuia rushwa.
    • Hutakiwi kutoa fedha kama dhamana uwapo kituo cha polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa, isipokuwa maelezo utakayoandika.
  • Raia ana haki ya kuwaeleza polisi ama Maafisa wa Kuzuia Rushwa kwamba lolote atakalosema linaweza kutumiwa kama ushahidi mahakamani, na asiburuzwe kuandika tu.
  • Raia ana haki ya kuomba Wakili wake awepo kituo cha polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa wakati anatoa maelezo yake.
  • Raia ana haki ya kuyasoma kabla ya kutia sahihi yake.
  • Raia ana haki ya kudai risiti ya orodha ya vitu vyake/fedha zake alizozitoa ama kukabidhi kituo cha polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa.
  • Raia kama ni mwanamke ana haki ya kupekuliwa na polisi wa kike, na iwapo hakuna polisi mwanamke, basi mwanamke yeyote na vile vile kwa mwanamume.
  • Raia ana haki ya kufikishwa mahakamani katika muda usiozidi saa 24 tangu alipokamatwa na kufikishwa kituo cha polisi.

Hizi haki zina maana na thamani kwa PILISI na VYOMBO VYA SHERIA Vyenye HAKI! AKILI TIMAMU, UTU NA UBINADAMU!
Kama Polisi wenyewe hawana Akili nzuri, hawana Utu, hawna ubinadamu, hawana Utashi, wanaonekana kuwa vichaa, wababishaji, wendwazimu waendawazimu hivi, hawana utambuzi, hawana ustaarabu na virtue nyigine za kibinaadamu HIZI SHERIA HAZINA MAANA YEYOTE!

SULUHU!

Kinachotakiwa kufanya kazi kwenye hali kama hiyo sio UKWELI Ila ni BUSARA!

Kwamba ni kweli kuwa wewe una hakifulani hiyo haina maana tena! Wewe jua hiyo ni haki yako lakini anayeishughulika Hana wadhafa ya kuishughulikia hivyo sio sahihi wewe kuchukulia kuwa hiyo ni haki.

Inakuwa ni haki tu kama upande wa pili uko TIMAMU!

Kwa utambuzi huo cha kufanya SIO kusimamia UKWELI! Hapo unatakiwa kucheza na BUSARA! habari kuwa ni kweli na Mungu anajua haisaii kitu! Hapo tumia Busara!

Unamkimbiza Mama anataka kujifugua kwa upasuaji! Ghafala jamaa kakupiga Mkono! Haelewe pamoja na kuwa anaona wazi wazi hali ya Mzazi!

Ni Kweli unahaki ya kumkimbiza Mama Hosptali lakini jamaa maechachamaa ..washa taahii, shika breki ..kama chizi vile .. Unaaza kutoleana povu naye ..ni kweli ni haki yako lakini wewe ndio huna busara!

BUSARA!

Unamlipa na kumuhonga kwa sabubu toka moyoni kwako unajua kuwa yule ni Mshenzi, Punguani, Mtumwa wako .. Mlpie muhonge .. Bila kujali kabisa.. wala hakuna kusononeka hapo, wala hakuna kusita .. Huyo ni mnya kama wengine tu! Lazma kuonyesha ukomavu wako ... Mlipe ukimaliz akama unaona hali inaruhusu mtukane vizuri ... Then ..usipoteze muda naye .. Muwahishe Mgonjwa!!

Utatueelza nini ..kuwa ulikuwa unabisha na Trafiki chizi ..hadi Mama amefaikiri mble yake ...?

Hapa nataka kuonyesha

Umuhimu wa kujua namna ya kuzitumia hizi sheria Mbele Ya UKWELI au Mbelea ya BUSARA!
Yaani Mtu unaijua Bongo! Vizuri ...Ni Busara kujua kuwa kuna wakati Kusimamia Ukweli ni jamabo la Kijinga ..N autambuzi huo Unakufanya wewe kuwa na BUSARA!

Kuzijua sheri ni muhimu lakini ..inabidi kusoma hali na mwenendo wa tukio zima!

Wapi utumie Ukweli na wapi kutumia Busara!!

Inawezekana uko klwenye mood, trafiki anakupa notification... unaweza kumalizana nyae pale pale ..ukinagalia huna haraka, huna dharura, hakuna mkutano , huwahi mtihani au interviwe nk ... Ukimtizama alate upuuzi nk ... Uanamuambie munede kituoni ... Notification kama ni ya laki ... unaitoa ..na kumkatalia hogo ya elfu thelathini ... kwakuwa ni mpuuzi tu!

Lakini Mpuuzi huyo huyo ..akuzuie usiwahi Interviwe, fainal impotant exam kisa unatetea haki yako ..huko ni kukosa Busara!

Haki hizi zina maana sana kwenye sysytem ambazo zimesimamia UKWELI Kwa asilimia mia mia moja!

Hapa BONGO ..hawajamaa Tuachiewe sisi wenyew e..We Know them and How to fix them!!
 
He mbona hata mimi sikuwa najua hayo yote mara nyingi nimekuwa nakamatwa naulizwa leseni na kadi ya gari sikumbuki hata kumuuliza hata jina asanta kwa ujumbe mzuri
 
Wanajamii mimi ni kuku hanuni lakini pia ni kuku mgeni, msinishangae ninapojibu au kucomment kwenye mambo yaliyosemwa back 47, maana ndio nimejiunga na jamii na ndio napitiapitia baadhi ya threads, Senior Expert, hili la kuhusu police ni kweli kabisa, mwananchi hana haki hata kidogo, mimi nilishangaa sana mwaka jana nilibahatika kwenda uingereza, basi mwenyeji wangu akawa ananizungusha mitaani, mara mjomba kapunga gari ikawekwa pembeni, basi police juu ya kuwa alikuwa katika sare zake, alitoa kitambulisho kisha akasema excuse me sir, could you pull your car and come out?

Mengine yakaendelea kwa heshima na adabu, kilochonishangaza police kumwita dereva Sir? na kuongea nae kwa adabu, mwisho wa mahojiano akasema thank you sir, sorry for taking your time this is part of the routine check, drive safe and good bye upooooooooooooo.

Je, hapa yawezekana? kama ulivyosema here Police is above the law no matter what, Mhesh. Said Mwema Wasemaje?
 
Bikra na Mwanahaki, nawapa big up. Yaani mmetupa vitu vitu vya maana sana. Binafsi mmeninielimisha sana katika hili, thanks again.

Ni kweli kabisa kuwa kuna haki nyingi za raia zinavunjwa. Polisi wengi vituoni-'frontliners' ni darasa la saba au form four failures. Tatizo na wao hawazijui hata sheria zao wenyewe. Wanachojua wao ni kuwa wananchi wanaogopa vituo vya polisi na ili dhana hiyo iendelee basi kuendeleza ubabe ule ule wa kupiga watu makofi, virungu na kila aina ya kuwa-provoke. Na ukileta kujua zaidi unaweza hata tolewa mahabusu na kupelekwa MSITU WA PANDE unapigwa risasi na kusema jambazi sugu lilikuwa linatupiana nao risasi.

Kwa ujumla Tanzania hatuna utawala wa sheria, tunautawala wa MSITUNI - LAW OF THE JUNGGLE. Ukionesha unajua sana polisi wanakuona ni threat unaweza kuwatia matatani na kuamua hata kukuua kabisa. Mi usemi ni KUVUNJA JESHI LA POLISI na kuunda kitu ambacho ni Friendly kwa wananchi kitakachosimamia haki zao na kupata trust yao. Jeshi la MANUMBA is DISGRACE to POLICING PROFESSION
 
Kwa bongo hizo haki zote hazipo, unapata ajali gari yako inaenda kituoni kesho unatoka hospitali unakuta scrapper wakati polisi walifika mapema na wameichukua wao unawaona.
 
1. Yaliyowekwa ni kweli na yanawezekana ila kwa kuwa yeye ni law enforcer huwa anakuja na confidence sana na hudhani mkamatwaji hajui haki zake (most oftenly)

2. Cha maana hapo usikubali hata siku moja akusogelee to the maximum proximity (kugusana) as huwa wanaleta mambo kama ulitaka kumshambulia, kupora silaha etc.....so from the distance ongea kwa kujiamini na kama inawezekana draw attention ya watu wanaokuzunguka then tembea na haki zako kama ilivyoainishwa hapo juuu......

3. Approach za hallo ndugu naomba kukuuuliza....halafu anakutoa mbali na watu ni moja ya mitego ya kuku isolate na watu........so never accept request za aina hii kutoka kwa hawa wapiga kura wenzetu
 
Vile vile unaweza ukanyoosha maelezo police ukifika mahamani ukayakataa, maana unaweza singiziwa jambo usiposema ndio unapigwa hata waweza kufa! mahakamani ndio mpango mzima
 
``Hakuna haki pasipo wajibu``Binafsi na shukuru kwa mchango wako mkubwa katika kuelimisha raia juu ya haki zetu tunapokamatwa na polisi.

Hata hivyo ninaomba kutoa rai kuwa; wanasheria na wanaharakati wengi wamekuwa wakitumia muda mwingi kutoa elimu juu ya haki za raia kwa polisi huku wakisau kuwa raia wanawajibu kwa polisi.kitendo hiki kinapelekea raia wengi kujikuta wanaingia matatani kwa Polisi kwa kudai haki bila kutimiza wajibu wao.Mfano kudai uhuru wa kujieleza kwa njia ya maandamano bila kutimizi masharti,kuongea na ndugu,jamaa au marafiki kwa lugha za kienyeji kama kigogo au kisukuma bila kujua kuwa ni sharti atumie lugha za kiofisi ili polisi naye askie kinachoongelewa n.k

Wewe kama miongoni mwawanasheria/wanaharakati nakuomba kupitia safu hii utoe elimu juu ya wajibu wa raia kwa polisi


  • Raia ana haki ya kumwomba askari ajitambulishe kwako.
    • Mwulize jina lake
    • Mwulize namba yake ya uaskari
  • Raia ana haki ya kujulishwa kwanini anatiliwa mashaka ama kukamatwa.
  • Raia ana haki ya kuwajulisha ndugu, jamaa ama sehemu anakofanyia kazi kwamba ama amekamatwa na polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa.
  • Raia ana haki ya kuomba na kupewa dhamana wakati akiwa kituo cha polisi ama Taasisi ya kuzuia rushwa.
    • Hutakiwi kutoa fedha kama dhamana uwapo kituo cha polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa, isipokuwa maelezo utakayoandika.
  • Raia ana haki ya kuwaeleza polisi ama Maafisa wa Kuzuia Rushwa kwamba lolote atakalosema linaweza kutumiwa kama ushahidi mahakamani, na asiburuzwe kuandika tu.
  • Raia ana haki ya kuomba Wakili wake awepo kituo cha polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa wakati anatoa maelezo yake.
  • Raia ana haki ya kuyasoma kabla ya kutia sahihi yake.
  • Raia ana haki ya kudai risiti ya orodha ya vitu vyake/fedha zake alizozitoa ama kukabidhi kituo cha polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa.
  • Raia kama ni mwanamke ana haki ya kupekuliwa na polisi wa kike, na iwapo hakuna polisi mwanamke, basi mwanamke yeyote na vile vile kwa mwanamume.
  • Raia ana haki ya kufikishwa mahakamani katika muda usiozidi saa 24 tangu alipokamatwa na kufikishwa kituo cha polisi.
 
katika ilo swala la kufikishwa mahakamani nya tegemeana na siku au mda mtuhumiwa anapokamatwa pia ikatokea mtuhumiwa akakamatwa ijumaa baada ya mda wa kazi ulowekwa na serekali iyo itakuwa exceptional as italazimu asubiri mpaka jumatatu ndio afikishwe mahakamani ili hali kama kosa lake lina ruhusiwa udhamini atadhaminiwa ilo kidogo ulikuwa umelisahau
 
107 Reactions
Reply
Back
Top Bottom