Jua haki yako unapokamatwa na Polisi

Mtu ukishaandikiwa notification na Police Trafic kwa kosa flan na ukailipa sasa ni kwa muda gani notification hiyo inakua valid hata ukishikwa tena within kipindi hicho huwezi andikiwa tena kwa kosa la namna hyo?
 
Bendera ya papa inapepea wakati wote kwa kuashiria kwamba utawala wake upo wakati wote.Lakini bendera ya nchi yetu huwa inashushwa baada ya saa 12.30 jioni inamaanisha utawala umeenda kulala.Nafikiri hapa ndipo chanzo cha mtu kushindwa kukamatwa baada ya muda huu.Infact, pana mkanganyiko.
 
Ahsante sana bikra,
pia nawashukuru mod kwa kuona umuhimu wa hii kitu na wakaiacha hapa mpaka muda huu,
 
Kwa hiyo jizi likivamia usiku wa manane inabidi kisheria tusubiri kuche ndio tiulikimbize kulikamata na kulisachi?

Matukio ya papo kwa hapo yamebeba dhana tofauti ya utuhumiwa na yale matukio yaliyotokea kitambo. Utuhumiwa wa matukio ya papo kwa hapo yana sheria zake madhubuti ya namna ya kukabiliana nayo.
 
Ikiwa umekamatwa katika misingi ya kuzingatia sheria na taratibu zote kama ulivyozibainisha na kupelekwa kituo cha polisi na kisha mahakamani ndani ya masaa 24 na mahakama kuonelea kuwa huna hatia, Je, ni hatua gani (za kisheria kama zipo)unaweza kuchukua ili kufidia hasara kubwa uliyoipata kutokana na kukamatwa kwako kimakosa?
 
Ikiwa umekamatwa katika misingi ya kuzingatia sheria na taratibu zote kama ulivyozibainisha na kupelekwa kituo cha polisi na kisha mahakamani ndani ya masaa 24 na mahakama kuonelea kuwa huna hatia, Je, ni hatua gani (za kisheria kama zipo)unaweza kuchukua ili kufidia hasara kubwa uliyoipata kutokana na kukamatwa kwako kimakosa?

Unaweza kufungua kesi ya madai 'malicious prosecution,' lakini ili ufanikiwe inapaswa kusiwe na 'reasonable and probable cause' ya wewe kushitakiwa. Kukutwa huna hatia haimaanishi kuwa 'hakukuwa na probable cause' kinachoangaliwa ni mazingira mazima ya kesi yako ya jinai na ushahidi wake yanaleta sababu ya mtu kudhani ulitenda kosa? Kama jibu ni ndio hutafanikiwa kwenye kesi yako ya madai.
 
Ndugu zangu Wana JF, si kwamba Polisi wanasoma au wanajua sheria, wanachotumia ni "Excess Force" pale wanapotaka kumkamata Mshukiwa....Excess Force ya nini kwa Mshukiwa kama si kuogopa kivuli chake mwenyewe?

Upandaji wa vyeo vya "KIJESHI" katika Component zetu nne unafafnua aina mbili ambazo ni "upandaji cheo au utunukiwa kwa njia ya Elimu aliyo nayo mhusika, Pili Upandaji cheo kwa njia ya RPL (Recognition Prior Learning) kupitia uzoefu kazini pamoja na kozi mbalimbali anazopitia muhusika kwa awamu tofautitofauti.

Miezi tisa ya Polisi Pale CCP si ya kusoma SHERIA,(Hakuna sheria inayosomwa kwa miezi tisa)bali ni ukakamavu na mbinu mbalimbali za jinsi ya kukabiliana na wahalifu, pamoja na uhalifu wenyewe.
 
Topic hii nitaichangia kulingana na ufahamu wangu kidogo kuhusu masuala hayo.....
 
yeyote
naitaji sana nipate copy ya P.G.O (police general orders ya Tanzania) hapa
 
Asante sana lakini huku T.SEGEREA kituo UGOMBOLWA polisi na jamiipolisi wanatuvizia wanywaji nakutuweka selo asabuhi utackia ulipokamatwa jana waliibiwa,ukitoa kitamburisho kazi yako inakataa kutembea saa hizi nilazima kumi ikutote,kwahiyo watz heri umwambie jwt tarifaa kuliko polisi,nina aleji polisi mno
 
ni kweli haya msemayo yanatukuta mimi nilikamatwa nilitoka mahakamani ktk case kuna jamaa nimemstaki ,kwa kuwa nilipata elimu kiasi juu yahili nipata ujasiri wa kuhoji kwa nini nakamatwa ,bila maelezo na nataka nipewe charge sheet kabla ya kwenda huko watakako twende ,askari ikabidi aniache akalete charge sheet nikaisoma ndo tukaondoka kwenda kituo cha police ,twawshkuru watanzania wenzetu msichike kutoa elimu kwetu tutakombolewa nanyi
 
  • Raia ana haki ya kumwomba askari ajitambulishe kwako.
    • Mwulize jina lake
    • Mwulize namba yake ya uaskari
  • Raia ana haki ya kujulishwa kwanini anatiliwa mashaka ama kukamatwa.
  • Raia ana haki ya kuwajulisha ndugu, jamaa ama sehemu anakofanyia kazi kwamba ama amekamatwa na polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa.
  • Raia ana haki ya kuomba na kupewa dhamana wakati akiwa kituo cha polisi ama Taasisi ya kuzuia rushwa.
    • Hutakiwi kutoa fedha kama dhamana uwapo kituo cha polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa, isipokuwa maelezo utakayoandika.
  • Raia ana haki ya kuwaeleza polisi ama Maafisa wa Kuzuia Rushwa kwamba lolote atakalosema linaweza kutumiwa kama ushahidi mahakamani, na asiburuzwe kuandika tu.
  • Raia ana haki ya kuomba Wakili wake awepo kituo cha polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa wakati anatoa maelezo yake.
  • Raia ana haki ya kuyasoma kabla ya kutia sahihi yake.
  • Raia ana haki ya kudai risiti ya orodha ya vitu vyake/fedha zake alizozitoa ama kukabidhi kituo cha polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa.
  • Raia kama ni mwanamke ana haki ya kupekuliwa na polisi wa kike, na iwapo hakuna polisi mwanamke, basi mwanamke yeyote na vile vile kwa mwanamume.
  • Raia ana haki ya kufikishwa mahakamani katika muda usiozidi saa 24 tangu alipokamatwa na kufikishwa kituo cha polisi.

Hili ni somo zuri sana liko hapa yapata miaka minne sasa, halafu bado dr. Ulimboka alikubali kukamatwa na polisi bila kuzingatia haki zake hizo? hasa zile nne za kwanza. Marekani kuna kitu kinaitwa miranda rights, ambazo kwa Tanzania usipojibu swali la polisi nadhani utapata kipigo kilai sana.
 
dah asante sana kwa msaaada wako wapo raia wengi ambao wananyanyaswa na polisi bila hata kujua haki zao za msingi!!!
mmoja wao ni mimi ambapo polisi walinishka nikiendesha gari nikiwa cna leseni wakachukua gari yangu na kuiendesha wao!!

pia wawakunipa risiti walivo nisweka lumande theni walinipiga bila ya kujieleza!!!!

nduguzanguni wanasheria wapeni watanzania elimm ya uraia wasionewe ovyo!!!

tha alot let us calll each other
 
107 Reactions
Reply
Back
Top Bottom