Jua haki yako unapokamatwa na Polisi

kama kawaida yao na ubishi wwt wa kujua haki zako ujue virungu vitautenda mwili wako bila simile kwa kisingizio cha TUMIA NGUVU KIASI KUFANIKISHA UKAMATAJI ENDAPO MTUHUMIWA ANAGOMA KUKAMATWA. Hicho ni kifungu ndani POLICE GEN. ORDER Kinachowapa jeuri ya kututenda. SASA HII C INAENDELEA KUWAPA NYODO HAWA WALINZI?

Je?askari polisi ana haki ya kukudai leseni ya udereva anapokusimamisha unapoendesha gari barabarani.

Je?sheria hizi zinapatikana wapi.
Je?ni kweli kwamba mtu akiwa uchi haruhusiwi kukamatwa.
Naomba utufungue macho
 
Mtuhumiwa ana haki gani anapokamatwa na polisi?
ban.sheria.jpg

Allan Kajembe

amka2.gif
HABARI za wakati huu msomaji wa Tanzania Daima. Nakutakia mwaka wenye amani na mafanikio.
Kwa kuanza ni vizuri tukatupa jicho letu katika haki za msingi za mtuhumiwa wa kosa au makosa ya jinai pindi anapokamtwa na polisi.
Kuna mambo kadhaa unayotakiwa uyajue, ambayo mtuhumiwa wa kosa la jinai anatakiwa afanyiwe wakati wa kupekuliwa au kukamatwa.
Kwanza, kumkamata mtuhumiwa kunaweza kuwa kwa kutumia hati ya kumkamata au inaweza kufanyika bila kutumia hati ya kumkamata.
Kwa mujibu wa kifungu cha 13 cha sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, iwapo mtuhumiwa atakuwa ameshafunguliwa mashitaka, basi mahakama kwa kutumia hakimu wake itamuita kwa kutumia hati ya kumkamata mtuhumiwa huyo na kama mtuhumiwa huyo atakuwa hajafunguliwa mashitaka kabla hajakamatwa, basi samansi itatumika na wakati mwingine mtuhumiwa anaweza kukamatwa bila hata kutumia hati ya kukamata.
Kumkamata mtuhumiwa bila kutumia hati ya kukamata kunaweza kufanywa na mtu yeyote, si lazima ofisa wa polisi kama ambavyo kifungu cha 16 na 14 cha sheria hii kinavyotamka bayana.
Miongoni mwa watu ambao pia wanaweza kumkamata mtuhumiwa wa kosa la jinai ni pamoja na hakimu wa mahakama yoyote iliyowekwa kisheria, walinzi wa amani, yaani wajumbe wa nyumba kumi/mabalozi wa nyumba kumi na ofisa watendaji wa kata na baadhi ya viongozi wa serikali za mitaa.
Hata hivyo, watu hawa watamkamata mtuhumiwa ikiwa tu kama mtu huyo atakuwa anafanya kosa la jinai lililo ainishwa chini ya kifungu cha 18 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai.
Kimsingi ni jukumu la ofisa wa polisi au mtu yeyote anayemkamata mtuhumiwa, kumtaarifu mtuhumiwa huyo sababau ya kumkamata na si kumkamata kiholela kama ambavyo wakati mwingine inafanyika.
Hali hii wakati mwingine inasababisha watuhumiwa kukataa kukamatwa na hivyo kuleta mtafaruku baina yao na mtu/watu wanaoenda kutimiza wajibu wao wa kisheria kuwakamata watuhumiwa hao.
Hiki ni kigezo muhimu cha kisheria kwa watu wanaokwenda kuwakamata watuhumiwa wao kukitimiza kabla ya kuwakamata.
Kwa upande wa watu wasio askari wanaokwenda kuwakamata watuhumiwa, inawalizimu kuwakabidhi watuhumiwa hao katika mamlaka zinazohusika bila kuchelewa.
Na kwa mamlaka husika tuna maanisha ampeleke mtuhumiwa kituo cha polisi au mahakama iliyo karibu naye.
Hii ni muhumu kwa sabababu watu binafsi hawana nyenzo au mahala panakokidhi viwango vya kuwaweka watuhumiwa na zaidi ya yote kuna uwezekano mkubwa kwa wao kutozingatia kanuni na vigezo muhimu vya kisheria katika kuwahifadhi watuhumiwa wao.
Mfano mzuri tunaupata katika kesi ya Jamhuri dhidi ya Dastur, A.L.R 421, ambapo mtuhumiwa aligoma kukamatwa kwa kutoambiwa sababu ya kukamatwa.
Zaidi ya hapo, mtuhumiwa alitoa kisu na kumchoma nacho askari mmoja wapo kati ya watatu waliokwenda kumkamata.
Mahakama baada ya kuridhika na maelezo yake, ilisema kwamba mtuhumiwa alikuwa na haki ya kuelezwa sababu ya kukamatwa.
Kitu kingine cha msingi ambacho unatakiwa kujua ni kwamba mtu anayetakiwa kumkamata mtuhumiwa ni kwamba anatakiwa kutotumia nguvu za ziada wakati wa kumkamata mtuhumiwa.
Hii inamaana kwamba, vitu kama pingu, kumshika mtu kibindo na kadhalika, vinatakiwa kutumika ikiwa tu mtuhumiwa mwenyewe atakuwa anakataa kukamatwa kihalali.
Hii ndiyo maana ya nguvu za ziada kama zilivyoelezewa chini ya kifungu cha 12 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai.
Kwa mujibu wa maamuzi ya mahakama katika kesi ya M’bui dhidi ya Dyer,(1967) E.A 315, ikiwa kama ofisa wa polisi (au mtu yeyote anayemkamata mtuhumiwa) atatumia nguvu za ziada kumkamata mtuhumiwa, basi mtuhumiwa huyo anaweza kumfungulia madai ya kutumia nguvu za ziada kumkamata.
Hata hivyo, suala la kuamua kama nguvu za ziada zimetumika au la, litaamulia kutokana na mazingira
ya kesi yenyewe.

Sheria hii pia imetoa mamlaka kwa polisi kuvunja nyumba ili kumkamata mtuhumiwa aliyejifungia ndani, kama ambavyo kifungu cha 19 na 20 cha sheria hii kinavyoelekeza.
Hii ni kwa sababu inawezekana kwa mtuhumiwa wa kosa la jinai akajifungia ndani ya nyumba au jengo ili akimbie mkono wa sheria.
Hivyo kwa kutambua hilo ndipo chini ya kifungu cha 20 cha sheria kikatoa msimamo huu.
Pamoja na hayo yote, sheria hii imekataza kitendo cha kuwakamata watoto au mke/mume wa mtuhumiwa kwa madhumuni ya kumshurutisha mtuhumiwa ajisalimishe katika mkono wa sheria.
Kitendo hiki ni kinyume cha sheria kama ilivyoamriwa katika kesi ya Lulu Titu dhidi ya Jamhuri (1968), H.C.D 30 ambapo mke wa mtuhumiwa alikamatwa na polisi kwa nia ya kumshurutisha mthumiwa ‘ajisalimishe’ polisi.
Katika maamuzi yake , mahakama ilisema kwamba kitendo hiki ni kinyume cha sheria na kanuni za msingi za haki na kwamba mke wa mtuhumiwa anaweza kuwafungulia polisi shauri la madai kwa kudai fidia.
Kwa upande wa kumpekua mtuhumiwa au nyumba yake, kitendo hiki pia kinaweza kufanywa kwa kutumia hati ya kupekua au bila hata kutumia hati ya kupekua.
Ndugu msomaji unatakiwa kujua kwamba kuna mazingira yanayoweza kumlazimisha askari kukupekua bila kuwa na hati ya kukupekua, na hii mara nyingi hutoke pale ambapo suala lililokuwepo ni dharura.
Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai pia imeiingiza dhana hii katika vifungu vyake. Hata hivyo, mtu mwenye jinsia ya kike ni lazima apekuliwe na mwanamke mwenzake na hivyo hivyo kwa mwanaume ambaye naye ni lazima apekuliwe na askari mwenye jinsia ya kiume.
Hii ni katika kulinda heshima na utu wa mtuhumiwa anayepekuliwa.
Hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 26 cha sheria hii. Kitu cha msingi kuhusu kupekuliwa ni kwamba, kwa mujibu wa sheria, mtu anatakiwa kupekuliwa kati ya mchana hadi jioni, yaani kipindi ambacho jua linachomoza na pale jua linapokuchwa tu, na si vinginevyo.
Kwa maneno mengine ni kwamba mtuhumiwa haruhusiwi kupekuliwa wakati wa usiku isipokuwa kama mahakama imeruhusu hivyo chini ya kifungu cha 40 cha sheria hii.
 
Raia awepo kizuizini ana haki ya kupata huduma za kiafya na matibau

Raia ana haki ya kutoshikwa au kufungwa shati au pingu iwapo hajakaa kukamatwa

Raia ana haki ya kutopigwa na polisi wakati wa kukamatwa

haki nyingi zimeorodheshwa tatitizo ni uwoga uliopo miongoni mwa raia..haki hizi zinavyo vyunjwa raia wengi hawatoi ripoti polisi. Pia polisi wenyewe ni tatizo maana wanajua jinsi wana vyotakiwa kufanya arrest ila ndo wamekuwa wavunjaji wazuri wa sheria, Tunaomba Jeshi la Polisi liwashughulikie polisi wahusika maana wanajulikana imekuwa kama sifa polisi kumpiga eaia wakati wanapomkamata..Tuache woga ukikamatwa na haki zako zikivunjwa report
 
Tatizo yote hayo unayosema yameandikwa tu katika vitabu na hayatekelezwi.

Bongo kuna vyombo vya DOLA NA DOWANS na hatuna polisi.

Nchi za wenzetu polisi ni graduate na anapokukamata anaomba ruhusa kukutia nguvuni.

Nchi km Sweden polisi haruhusiwi kumfukuza mtuhumiwa na iwapo atafanya hivyo mtuhumiwa akaanguka na kuvunja kiungo cha mwili, basi mtuhumiwa ana haki ya kumshtaki polisi na kuhukumiwa.

hapa bongo ni UMANYAKI KWA KWENDA MBELE hakuna ubinadamu.:msela:
 
Tatizo yote hayo unayosema yameandikwa tu katika vitabu na hayatekelezwi.

Bongo kuna vyombo vya DOLA NA DOWANS na hatuna polisi.

Nchi za wenzetu polisi ni graduate na anapokukamata anaomba ruhusa kukutia nguvuni.

Nchi km Sweden polisi haruhusiwi kumfukuza mtuhumiwa na iwapo atafanya hivyo mtuhumiwa akaanguka na kuvunja kiungo cha mwili, basi mtuhumiwa ana haki ya kumshtaki polisi na kuhukumiwa.

hapa bongo ni UMANYAKI KWA KWENDA MBELE hakuna ubinadamu.:msela:


Mkuu hapa Tanzania polisi wengi hawajui kanuni na taratibu za kazi, ni kawaida polisi kupiga watu, ni kawaida polisi kutishia watu kwa kufyatua risasi hewani na ni kawaida kwa polisi kuvunja sheria nyingi tu. Ubinadamu Tanzania ni kitu kilicho mbali sana. Ili polisi ajioneshe kuwa yeye ni polisi lazima apige au atishie watu.
 
Sina shaka na maelezo yako mkuu...lakini najiuliza ni polisi wa nchi gani hasa.... Tanzania????
 
Naomba ufafanuzi polisi anapokuja kukamata aje na taratibu zip ambazo naweza zifahamu kwenu wana JF,pia mtu akikamatwa nduguye anaweza kuhoji kosa lake kwa OCS au OCD au ofisa gani kituoni?ushauri mapolisi wac2mie cheo kwa manufaa binafsi
 
Pia raia anayo haki ya kutojibu chochote pale anapoulizwa na polisi. Sidhani kama kama raia wengi wanalijua hili. You have the right to main silence hata wakikutishia kukuweka ndani
 
Raia awepo kizuizini ana haki ya kupata huduma za kiafya na matibau

Raia ana haki ya kutoshikwa au kufungwa shati au pingu iwapo hajakaa kukamatwa

Raia ana haki ya kutopigwa na polisi wakati wa kukamatwa

haki nyingi zimeorodheshwa tatitizo ni uwoga uliopo miongoni mwa raia..haki hizi zinavyo vyunjwa raia wengi hawatoi ripoti polisi. Pia polisi wenyewe ni tatizo maana wanajua jinsi wana vyotakiwa kufanya arrest ila ndo wamekuwa wavunjaji wazuri wa sheria, Tunaomba Jeshi la Polisi liwashughulikie polisi wahusika maana wanajulikana imekuwa kama sifa polisi kumpiga eaia wakati wanapomkamata..Tuache woga ukikamatwa na haki zako zikivunjwa report

Hapo mkuu issue sio uoga,issue ni elimu ndogo juu haki za msingio za kiraia na elimu kidogo juu ya sheria zetu,hilo ndilo ambalo watanzania wengi hawalifahamu
 
Asante sana mleta hoja baada ya kuonewa na police uko nyuma na baada ya kusoma maelezo hapa kumekuwa na mabadiliko kidogo siogopi tena ila kuna shida ingine unapokuwa unajua haki zako na ukaenda police wanapokuburuza ukakataa na kujibu kwa vifungu vya sheria.

Majuzi kati mdogo wangu alikamatwa kwa hila ya mshikaji wake na police nilipokwenda kituoni kutaka kumwekea dhamana police wakataka ki2 kdogo nilipokataa na kusema ni haki ya raia kupewa dhamana baada ya kusumbuana sana na kuona sina dalili ya kutoa pesa aliniambia dhamana sio lazima asa pale police anapoona kwa kufanya hivyo kutaatarisha amani mfano tukimwachia mdogo wako akaenda kupipigana tayari ni hatari so bora akae ndani wakuu nilichoka alivyonipindishia maneno ila nikitoa pesa akuna shida nilichofanya nikaenda kwa mkubwa wake kama wa 3 nikamsimulia akasema bac mwache alale leo mana fail alijaletwa kwangu asubui litafika ikaniuma lakini nikaona poa kuliko kwenda kumwangukia kweli kesho yake nikamtoa aliponioana akaniambia unaona nilikwambia nikamwambia mzue bac
 
Tatizo yote hayo unayosema yameandikwa tu katika vitabu na hayatekelezwi.

Bongo kuna vyombo vya DOLA NA DOWANS na hatuna polisi.

Nchi za wenzetu polisi ni graduate na anapokukamata anaomba ruhusa kukutia nguvuni.

Nchi km Sweden polisi haruhusiwi kumfukuza mtuhumiwa na iwapo atafanya hivyo mtuhumiwa akaanguka na kuvunja kiungo cha mwili, basi mtuhumiwa ana haki ya kumshtaki polisi na kuhukumiwa.

hapa bongo ni UMANYAKI KWA KWENDA MBELE hakuna ubinadamu.:msela:

Asanteee,naunga mkonao.
 
Ni kweli kwamba raia anatakiwa kutambua haki zake mara anapokamatwa na polisi, lakini tutambue vilevile kwamba polisi tulionao ni mali ya chama cha mapinduzi, hivyo hata kama mtu atakuwa anatambua haki zake hakuna haki atakayotendewa.

polisi wa tanzania wizi mtupu
 
Nimeipenda hii, yote ni kweli. Ila polisi au TAKUKURU ukiwaambia hivyo tu hawatishiki wala hawatakuruhusu upate haki zako hizo za kisheria. Nini cha kufanya sasa?

Mwana JF awaambie wananchi haki hizo ni kwa mujibu wa sheria. Kwanza sheria zote zinatokana na Katiba ya Tanzania ya 1977 (tazama: Ibara ya 64).

Sisi wanasheria tunasema supremacy of the constitution. Kisha haki alizoziainisha mwana JF (ninampongeza) zinatokana na Ibara za 12, 13 nk za Katiba na Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (THE CRIMINAL PROCEDURE ACT) vifungu 10, 53, 57, 58 nk.

Sasa polisi ukimwambia hivyo atashtuka kidogo, atajua huyu anaelewa. KWA PAMOJA TUPAMBANE NA UNYANYASAJI.........
 
Back
Top Bottom