Polisi Lindi wadaiwa kumlinda askari anayeshukiwa kumbaka binti wa miaka 13

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
3,660
12,304
Polisi wametakiwa kumsaka na kumkamata askari anayedaiwa kumbaka msichana wa miaka 13 ili kuondoa hisia kwamba wanajaribu kuificha kashfa hiyo na kumkingia kifua afisa wao huyo.

Askari huyo aliyefahamika kwa jina la Madushi Mhogota Ng’wala, aliyekuwa akifanya kazi katika dawati la jinsia la kituo cha polisi cha wilaya ya Liwale, anadaiwa kumbaka msichana huyo wa darasa la sita katika moja ya shule za msingi shule Liwale, na kusababisha taharuki na hasira kwa wazazi na wanajamii ambao kwa sasa wanataka haki itendeke.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopo, Ng’wala anadaiwa kumbaka msichana huyo majira ya saa mbili za usiku wa Februari 18, 2024, wakati binti huyo akitoka nyumbani kwao kuelekea nyumba ya jirani alikokuwa akienda kulala. Inasemekana Ng’wala alimkamata msichana huyo, na kumpeleka kichakani kisha kumfanyia kitendo hicho cha kikatili.

Familia ya binti huyo ilifahamu kuhusu tukio hili siku ya pili asubuhi mara baada ya mama wa mtoto huyo kuona damu ikichuruzika kutoka katikati ya miguu ya bintiye, jambo lililopelekea msichana huyo kusimulia masaibu yake kutoka kwa afisa wa huyo wa polisi.

Mama huyo alisema kuwa, ni binti yake ndiye aliyefichua jina la askari polisi huyo anayedaiwa kumbaka.

Source: TheChanzo
 
@doroth gwajima
 
Back
Top Bottom