Jua haki yako unapokamatwa na Polisi

  • Raia ana haki ya kumwomba askari ajitambulishe kwako.
    • Mwulize jina lake
    • Mwulize namba yake ya uaskari
  • Raia ana haki ya kujulishwa kwanini anatiliwa mashaka ama kukamatwa.
  • Raia ana haki ya kuwajulisha ndugu, jamaa ama sehemu anakofanyia kazi kwamba ama amekamatwa na polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa.
  • Raia ana haki ya kuomba na kupewa dhamana wakati akiwa kituo cha polisi ama Taasisi ya kuzuia rushwa.
    • Hutakiwi kutoa fedha kama dhamana uwapo kituo cha polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa, isipokuwa maelezo utakayoandika.
  • Raia ana haki ya kuwaeleza polisi ama Maafisa wa Kuzuia Rushwa kwamba lolote atakalosema linaweza kutumiwa kama ushahidi mahakamani, na asiburuzwe kuandika tu.
  • Raia ana haki ya kuomba Wakili wake awepo kituo cha polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa wakati anatoa maelezo yake.
  • Raia ana haki ya kuyasoma kabla ya kutia sahihi yake.
  • Raia ana haki ya kudai risiti ya orodha ya vitu vyake/fedha zake alizozitoa ama kukabidhi kituo cha polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa.
  • Raia kama ni mwanamke ana haki ya kupekuliwa na polisi wa kike, na iwapo hakuna polisi mwanamke, basi mwanamke yeyote na vile vile kwa mwanamume.
  • Raia ana haki ya kufikishwa mahakamani katika muda usiozidi saa 24 tangu alipokamatwa na kufikishwa kituo cha polisi.

Shukrani kwa kutujuza haki zetu za msingi. Keep it up!
 
Kama siridhiki na namna nilivyotendwa na polisi naweza kulalamika kupitia channels zipi? Kufungua shauri kawaida unaanzia polisi, je shauri la kumshtaki polisi linaanzia wapi?

Nimejaribu kucheki site yao, lakini haionyeshi ni jinsi gani ya kulalamika dhidi ya polisi. Kwenye nchi nyingine huwa wanakuwa na tume huru ambayo kazi yake ni kuhakikisha kuwa malalamiko dhidi ya polisi yanashughulikiwa ipasavyo. Unless kama kuna utaratibu mwingine, unaanza kulalamika kwa kupitia inspecta wa kituo chako cha polisi au kwa police staff manager kama yupo then unapanda ngazi taratibu. Lakini kama malalamiko ni mazito, sidhani kama hii ni njia muafaka.

Pia sidhani kama polisi wanaweza kuwa fair na unbiased ku handle complaints from a member of the public. Labda wadau wenye ufahamu na hili watasadia kujua taratibu za kuilalamikia polisi.
 
Naweza nikajua haki yangu nikikamatwa na polisi lakini nikijaribu kujitetea mbele ya polisi watasema wanafahamu wajibu waho,na wanajua sheria za kazi yao hapa cha maana tanzania akuna usawa na haki kwa nchi yetu pia tumezoe sana ruhwa ukisema ukweli ukimzidi atakwambia nipe kdogo kitu ndio tuelewane.
 
Rushwa ipo tz.lakini pia wabongo wengi aidha tunapungufu au hatujiamini kila tuingiapo mahali kuhitaji huduma hutanguliza kitu kidogo.Naamini tukiwa wasafi rushwa itakoma.
 
hongereni wachangiaji wote kuzidi kuelimishana ndio madhumuni ya jamii forum wala sio mipasho na matusi na lugha chafu
 
Dilunga

KWANI HAPO JIZI LINAKUWA LIMEKUJA KUSEARCH? KUKWIBA? HAPA LINALO ONGELEWA NI KUKAGUA SIO KUIBA
 
Hizo haki na nyingine nyingi tu Zinavunjwa kila leo na polisi. Ama kwa makusudi ama kwa wao polisi kudhani wako juu ya sheria. Kwa nchi kama Tanzania Polisi hujifanya mahakimu. nitajie aliywahi kulalmikia kuhusu unyanyasaji wa polisi na akashinda! sana sana polisi wakibaini mwenzao kacheza Faul basi ni quick transfer! Hayo labda ughaibuni. Maana Polisi waweza kuwakoromea mpaka wakaingia mitini!! as afar as wakigundua kuwa kuwa wajua haki zako. Jifanye kujua hakia zako katika vituo vya Polisi Tanzania uone vijana wa Said Mwema watakavyokurarua na virungu!!
Polisi wakisha kukamata unakuwa wewe tena huna haki. Wao ndio wenye haki kwako wewe haswa hizi Nchi za Afrika zote. Afrika hakuna Haki za kibinadamu Polisi hana haki ya kukupiga akisha kukamata lakini wapi Afrika yetu Polisi ndio wamegeuka wao ndio Mahakimu badala ya Mahakimu wenyewe.
 
Mdau naomba ujue kwamba kuna upekuzi wa dharula ambao huhitaji search order soma S.42 34 ya CPA (R.E 2002) at page, kuna wakati polisi wanalazimika kufanya upekuzi huo kufuatana na mazingira ya kosa hivyo ni muhim ukajua hilo.

PILI, umezungumzia kwamba hati ya upekuzi hutolewa na mahakama but for my understanding search order ipo polisi na kuna mazingira court may issue search that is in practice kwa tz. just imagine kuna tukio limetokea j.mosi and search is needed to be conducted na mahakam hazifanyi kaz utafanyaje.
 
107 Reactions
Reply
Back
Top Bottom