Jua haki yako unapokamatwa na Polisi

  • Raia ana haki ya kumwomba askari ajitambulishe kwako.
    • Mwulize jina lake
    • Mwulize namba yake ya uaskari
  • Raia ana haki ya kujulishwa kwanini anatiliwa mashaka ama kukamatwa.
  • Raia ana haki ya kuwajulisha ndugu, jamaa ama sehemu anakofanyia kazi kwamba ama amekamatwa na polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa.
  • Raia ana haki ya kuomba na kupewa dhamana wakati akiwa kituo cha polisi ama Taasisi ya kuzuia rushwa.
    • Hutakiwi kutoa fedha kama dhamana uwapo kituo cha polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa, isipokuwa maelezo utakayoandika.
  • Raia ana haki ya kuwaeleza polisi ama Maafisa wa Kuzuia Rushwa kwamba lolote atakalosema linaweza kutumiwa kama ushahidi mahakamani, na asiburuzwe kuandika tu.
  • Raia ana haki ya kuomba Wakili wake awepo kituo cha polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa wakati anatoa maelezo yake.
  • Raia ana haki ya kuyasoma kabla ya kutia sahihi yake.
  • Raia ana haki ya kudai risiti ya orodha ya vitu vyake/fedha zake alizozitoa ama kukabidhi kituo cha polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa.
  • Raia kama ni mwanamke ana haki ya kupekuliwa na polisi wa kike, na iwapo hakuna polisi mwanamke, basi mwanamke yeyote na vile vile kwa mwanamume.
  • Raia ana haki ya kufikishwa mahakamani katika muda usiozidi saa 24 tangu alipokamatwa na kufikishwa kituo cha polisi.


ya ukweli ka Bikra ilivo.... thanks..umenielimisha!!1
 
Jamani hizi sheria zipo tu kila siku lakini msiziamini sana wakati mwingine hata kama unazijua tulia. Sheria kubwa kuliko zote "be obedient" maana kuna vifungu ambavyo pia vinawaruhusu hawa jamaa kufanya kazi zao bila kuangalia haki hizo. hivyo msizitegemee sana mimi yaliwahi kunipata. Lakini namshukuru aliye post at least mtu unaweza kujua mahali ambapo umechezewa rough.
 
Kwa hiyo jizi likivamia usiku wa manane inabidi kisheria tusubiri kuche ndio tiulikimbize kulikamata na kulisachi?
jizi likivamia usiku wa ma8 huwa haisubiriwi kuche linakamatwa na kupekuliwa chini ya K/F 42 cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jina (criminal procedure act ) yaaani search on emergence
 
Mgambo wa jiji walinipeleka kituoni kwa issue nyingine nikafika wakanigeuzia kibao eti nimewazuia kufanya kazi zao kihalali, niliwaomba wajitambulishe wakagoma wakasema watajitambulisha kituoni kufika wakageuza kibao, bado natafuta msaada lazima nije kulipa kisasi at any cost, walinisweka rumande pale urafiki hadi nikatoa 50 elfu, bado inaniuma sana, nitalipa kisasi bado natafuta msaada
 
Mgambo wa jiji walinipeleka kituoni kwa issue nyingine nikafika wakanigeuzia kibao eti nimewazuia kufanya kazi zao kihalali, niliwaomba wajitambulishe wakagoma wakasema watajitambulisha kituoni kufika wakageuza kibao, bado natafuta msaada lazima nije kulipa kisasi at any cost, walinisweka rumande pale urafiki hadi nikatoa 50 elfu, bado inaniuma sana, nitalipa kisasi bado natafuta msaada

Mapolisi wanapata kiburi wakiwa kituoni,kama ishu inaweza ikaisha pasipokwenda kituoni ni vizuri zaidi.
 
Unajua Polisi wanajua raia hawafahamu haki zao za msingi wanapokamatwa na hata ukiwa unazifahamu wanakupa vitisho mwenyewe utatulia,ila ukijiamini nao wenyewe wanaona hapa pagumu..

Vipi pale polisi wanapokuja kukukamata nyumbani au ofisini ukiwauliza nije kituoni kwa kosa gani wao wanasema hutakiwi kujua hapa utaenda kufahamu hukohuko kituoni,na ukienda huko unaingizwa moja kwa moja ndani....

Na vipi unaweza kujidhamini mwenyewe?
 
Thanks this has been so useful. Please kama inawezekana mwingine atoe haki ya madereva pindi wakamatwapo na polisi usalama barabarani
 
Hii post imenifurahisaha sana, kwanini nilikuwa najiandaa kuandaa thread yenye madhumuni kama hayo.

kwa kifupi ni kwamba nyumbani kuna gari inayofanya biashara za usafiri, sasa jana askari akawa ameikamata na kuomba mmliki aende eti kosa ni kuwa hakuwa na insurance ya kufanyia biashara( sasa kwa kutokujua akajua kuwa labda kuna insurance nyingine tofauti na zile tunazonunua za kawaida) wakapewa faini ya tz elfu 20 , katika kujitetea yule traffic akamwambia alipe elfu kumi ili wamalizane( wakati huo mama akiwa kesha nitumia sms kunieleze kuhusu hilo swala), alipomaliza kumlipa Mama ikabidi afatilie kwenye vyombo husika ili kujua kama anatakiwa kulipa insurance nyingine, bahati nzuri kafika kule na kuelezwa kuwa hakuna bima nyingine zaidi ya hiyo uliyonayo, baada ya kama dk 45 mama akanitumia tena sms akisema "swala lile lilikuwa ni uonevu tu, wamechukua elfu kumi".

Siyo siri nilighadhabika sana na kumpigia simu na kumuuliza "kulikoni mtu umeshatambua kuwa ni uonevu bado unampa elfu kumi? kwa nini usirudi na kumwomba hiyo pesa yako? hivi ni kwa nini mnaruhusu kunyonywa wazi wazi kiasi hicho? akanijibu kuwa yaani huku Tanzania kila kitu ni rushwa tu iwe unataka au hutaki haki yako bila rushwa hakuna chochote..huku akiongezea kuwa sasa mimi nitafanyaje wakati sijui hata sheria zinasemaje? mmh hapo nikachoka kabisa.

Je, ni wangapi wanaofanyiwa madudu kama haya? unajua matatizo mengine tunayasabisha sisi wenyewe wananchi kwa kupenda kufanya haraka haraka bila kufuata procedure..
Nimetafakari sana na kutambua kuwa wananchi wengi hawajui sheria na wanaendelea kunyonywa tena wakinyenyekea kutoa chochote ili wapate haki yao, hivi hawa matraffic wataacha huu ubabaishaji hadi lini? sio siri kama ningekuwa Tanzania ningehakikisha namfatilia huyu traffic hadi mwisho ili iwe funzo kwa wengine kama hao.
 
Bikra na wengineo mliochangia shukrani sana kwa elimu hii. Naomba utuwekee na nukuu za vifungu vya sheria (citation) ambavyo vinatoa hizi haki.
 
  • Raia ana haki ya kumwomba askari ajitambulishe kwako.
    • Mwulize jina lake
    • Mwulize namba yake ya uaskari
  • Raia ana haki ya kujulishwa kwanini anatiliwa mashaka ama kukamatwa.
  • Raia ana haki ya kuwajulisha ndugu, jamaa ama sehemu anakofanyia kazi kwamba ama amekamatwa na polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa.
  • Raia ana haki ya kuomba na kupewa dhamana wakati akiwa kituo cha polisi ama Taasisi ya kuzuia rushwa.



    • hii kitu hapa vituo vya polisi ni ngumu sheria yetu inapindishwa sana na hawa wanaoitwa polisi!!
 
107 Reactions
Reply
Back
Top Bottom