- Raia ana haki ya kumwomba askari ajitambulishe kwako.
- Mwulize jina lake
- Mwulize namba yake ya uaskari
- Raia ana haki ya kujulishwa kwanini anatiliwa mashaka ama kukamatwa.
- Raia ana haki ya kuwajulisha ndugu, jamaa ama sehemu anakofanyia kazi kwamba ama amekamatwa na polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa.
- Raia ana haki ya kuomba na kupewa dhamana wakati akiwa kituo cha polisi ama Taasisi ya kuzuia rushwa.
- Hutakiwi kutoa fedha kama dhamana uwapo kituo cha polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa, isipokuwa maelezo utakayoandika.
- Raia ana haki ya kufikishwa mahakamani katika muda usiozidi saa 24 tangu alipokamatwa na kufikishwa kituo cha polisi.
Nyongeza kutoka kwa MwanaHaki
- Iwapo askari polisi ataamua kumpekua mtuhumiwa, mtuhumiwa ana haki ya kumpekua askari polisi KABLA ya kupekuliwa yeye mwenyewe
- Pia, askari polisi hawana haki ya kuingia kwenye gari, nyumba au ofisi ya mtu wanayemtuhumu, kwa madhumuni ya kufanya upekuzi, pasi na kuwapo kwa (a) hati ya upekuzi ambayo hutolewa mahakamani, (b) mashahidi wanaotambulika rasmi kisheria, kama vile, mwenyekiti/mjumbe wa serikali ya mtaa au mwenyekiti wa nyumba kumi kumi (iwapo mfumo huo unatumika), au (c) jirani wa myu anayetuhumiwa
- Aidha, mtuhumiwa hatakamatwa au kupekuliwa na askari polisi baada ya saa 12.30 jioni au kabla ya saa 12.30 alfajiri, kwa mujibu wa Mwendendo wa Makosa ya Jinai (Penal Code Act), isipokuwa tu, kama kutakuwa na ushahidi wa kutosha kwamba, kumpekua mtuhumiwa kabla ya saa 12.30 alfajiri au baada ya saa 12.30 jioni kunaweza kuleta madhara kwa askari polisi, mashahidi au watu wengine wowote wale
=============================
Haki zako za Kisheria unapokamatwa na Polisi
Raia unayo haki ya:-
*Kumwomba Askari ajitambulishe kwako....
-Muulize Jina lake.
-Muulize namba yake ya Uaskari.
*Kujulishwa ni kwa nini unatiliwa mashaka au kukamatwa.
*Kuwajulisha ndugu, jamaa na marafiki ama sehemu unakofanyia kazi kwamba ama umekamatwa na Polisi au TAKUKURU.
*Kuomba na Kupewa dhamana wakati ukiwa Kituo cha Polisi ama TAKUKURU.
*Hutakiwi kutoa Fedha kama Dhamana uwapo Kituo cha Polisi ama TAKUKURU, isipokuwa maelezo utakayoyatoa na kuandikwa Kituoni hapo.
*Kuwaeleza Polisi ama Maafisa wa TAKUKURU kwamba lolote utakalolisema linaweza kutumika kama ushahidi mahakamani na usiburuzwe wakati wa kuyatoa maelezo hayo.
*Kuomba wakili wako au mtu wa karibu yako utakayemchagua ili awepo Kituo cha Polisi ama Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa wakati unatoa maelezo yako.
*Haki ya kuyasoma maelezo yako kabla ya kutia sahihi katika maelezo hayo.
*Kudai risiti ya Orodha ya vitu vyako/fedha zako ulizotoa ama kukabidhi Kituo cha Polisi ama TAKUKURU.
*Haki ya kufikishwa mahakamani katika muda usiozidi Saa 24 tangu alipokamatwa na kufikishwa Kituoni.
Haki za Raia Kupekuliwa
*Mtuhumiwa anayo haki ya kumpekua Polisi kabla ya yeye kupekuliwa na Polisi huyo.
*Raia kama ni Mwanamke, anayo haki ya kupekuliwa na Askari wa Kike, na iwapo Askari wa Kike hayupo, basi Mwanamke yeyote anaweza kumfanyia upekuzi, vile vile kwa Mwanaume.
*Askari hawana haki ya kuingia kwenye Gari, Nyumba au Ofisi ya Mtu wanayemtuhumu, kwa madhumuni y kufanya upekuzi bila kuwa na:
(a) Hati ya Upekuzi ambayo hutolewa Mahakamani.
(b) Mashahidi wanaotambulika rasmi Kisheria, kama vile Mwenyekiti/Mjumbe wa Serikali ya Mtaa au Kijiji husika.
(c) Jirani wa Mtu anayetuhumiwa.
Aidha, Mtuhumiwa hatakamatwa au kupekuliwa na Askari Polisi baada ya Saa 12:30 Jioni au kabla ya Saa 12:30 Alfajiri, kwa mujibu wa makosa ya Jinai (Penal Code Act).
Isipokuwa tu, kama kutakuwa na ushahidi wa kutosha kwamba kumpekua Mtuhumiwa kabla ya Saa 12:30 Alfajiri au baada ya Saa 12:30 Jioni kunaweza kuleta madhara kwa Askari Polisi, Mashahidi au Watu wengine wowote wale.
./Mwana wa Haki
Zaidi soma=>Sheria :Zitambue haki zako unapokamatwa na Polisi
Zifahamu sheria pale unapokamatwa na polisi
Last edited by a moderator: