Huyu ndiye kijana aliyepoteza maisha kwenye mvutano baina ya police na CHADEMA

Siku zoooote ukombozi wa damu una thamani kwa waliobakia. Ndugu yetu Ally damu yako iliyomwagwa na Ccym na dola lake ni kirutubisho na chemchem ya ukombozi wa ndugu zako waliobakia. Pumzika kwa amani amina.
 
Hii ni ishara mbaya sana kwa CCM, tawala zote zilizotumia mtutu wa bunduki zilianguka na hata zinazoendelea kufanya hivyo ikiwamo Syria na Tanzania zitaanguka very soon, ni sula na kusubiri na kuona huku tukiendelea na M4C ambayo inawafanya wasilale.
 
Heading siyo hiyo:

HUYU NI KIJANA ALIYEUAWA NA POLISI AKITIMIZA HAKI YAKE YA KIKATIBA
Hakuna uhuru usio na mipaka , haya yote wakulaumiwa ni CDM na sheria wanazijua, kibali chakufanya haya maandamano walipewa ? huwezi shindana na dola hata siku moja
 
Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi lkn pia damu yake iwamwagikie na kuwamaliza magamba hatimaye ukombozi wa kweli kwa nchi yetu upatikane. Amen
 
Hii ni ishara mbaya sana kwa CCM, tawala zote zilizotumia mtutu wa bunduki zilianguka na hata zinazoendelea kufanya hivyo ikiwamo Syria na Tanzania zitaanguka very soon, ni sula na kusubiri na kuona huku tukiendelea na M4C ambayo inawafanya wasilale.
Napata wasi wasi na uwezo wakufikiri wa kwako, soma historia ya syria ndio utajua sababu za kule na za tanzania pia, ni vitu viwili tofauti kabisa unavyo vilinganisha.
 
Hakuna uhuru usio na mipaka , haya yote wakulaumiwa ni CDM na sheria wanazijua, kibali chakufanya haya maandamano walipewa ? huwezi shindana na dola hata siku moja

Hata Gadafi aliamini hivyo. Hata Hosni Mubarak aliamini hivyo pia.

Jambo la msingi ni iwapo dola inatenda haki au la na Kama dola inatenda haki raia watatii. Kama dola haitendi haki, haiwezi kunyamazisha raia kwa kuwatisha kwa bunduki.
 
Mnaambiwa msifanye maandamano mnang'ang'ania, ona sasa, mnapoteza roho za watu kwa ubishi wenu.

Mkiulizwa maandamano ya nini? hamjui!

Hiki chama kifungiwe tu, hakina mwisho wa amani.
Chadema ndio waliofyatua Risasi. Kila mkoa lazima muue mtu
 
Mnaambiwa msifanye maandamano mnang'ang'ania, ona sasa, mnapoteza roho za watu kwa ubishi wenu.

Mkiulizwa maandamano ya nini? hamjui!

Hiki chama kifungiwe tu, hakina mwisho wa amani.

Wakiandamana 'wagomea sensa' unajua umuhimu wa maandamano...
 
We refuse to be what they wanted us to be,we are what we are and that the way its going to be. M4C 4EVER.
 
Mwenzenu amekufa nyie mpo bize kupiga mapicha mwili wa marehemu ili msambaze mitandaoni!!

Lawama ziwaendee Chadema kwa kutotii amri ya polisi.
 
Nasikitika na kuumia kuona damu za wadanganyika zinapotea kwa kudai haki yao ila wale wanao wafanya maskini wanaendelea kudunda mtaani, risasi za moto ni stahiki ya wezi wa makaratasi na sio wadai haki, risasi za moto ni haki za wezi wa RADAR, RICHMOND, EPA, MEREMETA, WATOROSHAJI TWIGA, WAFICHA MABILLIONI USWISS na WAINGIA MIKATABA MIBOVU.

Wandhani kutupiga risasi za moto ndio wanatutisha kumbe wanasahau ndio wanatupa ujasiri zaidi, wanatupa hamasa zaidi.
Yuko wapi Muamar Gaddafi, yuko Hosni Mubarak, yuko Ben Ali, yuko wapi Gbagbo? hawa wote walitumia risasi za moto na nzito zaidi ya polisi wa Tanzania ila wamedondoka katika tawala zao.

CCM na serikali yake isome alama za nyakati
 
Mwenzenu amekufa nyie mpo bize kupiga mapicha mwili wa marehemu ili msambaze mitandaoni!!

Lawama ziwaendee Chadema kwa kutotii amri ya polisi.

Picha ni ushahidi, kwani tayari Kamanda wa Polisi ameanza kukana. Polisi hawana uhalali wa kutumia silaha za moto hata kama wanalazimika kutawanya maandamano.

Marehemu Ally alipigwa risasi kigogoni, ina maana Askari hawezi kujitetea kuwa alimpiga risasi kwa self defence. Hii ni blunder kwa jeshi la polisi. Hata Polisi wanaonea aibu kitendo hicho, tusiwe washabiki.
 
Hakuna uhuru usio na mipaka , haya yote wakulaumiwa ni CDM na sheria wanazijua, kibali chakufanya haya maandamano walipewa ? huwezi shindana na dola hata siku moja
Mkuu acha kushabikia mauwaji, kibali kilitolewa kuandamana that why gari la matangazo lilitangaza juzi Jpili siku nzima, kuna maandamano, hakuwa chombo chochote kilichokataza maandamano, kulikuwa na kibali cha polisi tena ni halali baada ya CDM kukubaliana na polisi.

Mkuu Blue! Marehemu alishindana na dola? kijana wa magazeti hakuwa hata na mpango wa kwenda kwenye mkutano, ama kwakuwa siyo nduguyako unachukulia poa tu? kwetu siye ni mtanzania ni ndugu yetu!
 
nadhani Tz tuna baraka ya kuwa na the least professional police force duniani kote, kama polisi anaweza kutumia live bullet bila ya kuwa provoked, tena kwa mtu anayesoma magazeti mtaani, seriously, huyu tutamwita muuaji au mlinda usalama wa watu na mali.
 
Mwenzenu amekufa nyie mpo bize kupiga mapicha mwili wa marehemu ili msambaze mitandaoni!!

Lawama ziwaendee Chadema kwa kutotii amri ya polisi.

Tumia hata ubinadamu jombaa hata kama kushindana kwa hoja unashindwa? huyo kijana hakuwa na Bango, gwanda wala bendera ya CDM, ni kwanini polisi IMUUWE?

Back
Top Bottom