CHADEMA kujifungia kwa saa 48 kujadili Azimio la Mtwara

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) inatarajiwa kujifungia kwa siku mbili kuanzia leo kuandaa Azimio la Mtwara la kushiriki au kutokushiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka huu.

Pia, kikao hicho kitakachohitimishwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe kitafanya tathimini ya maandamano ya amani waliyoyafanya katika majiji ya Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya na Arusha.

Februari 27 mwaka huu, Mbowe akihutubia mamia ya wananchi viwanja vya Reli, Arusha katika maandamano ya amani alisema wanakwenda kujifungia mkoani Mtwara kufanya tathimini ya maandamano hayo na mikakati mingine ya chama.

Lengo la maandamano hayo yaliyopewa jina la ‘Vuguvugu la haki ya Watanzania’ ni kuishinikiza Serikali kushughulikia gharama za maisha kwa madai kuwa, yamekuwa magumu kutokana na mfumo wa bei za bidhaa mbalimbali.
 
Yah, nimeona magari mengi ya m4c hapa Mtwara. Jamaaa wana mikakati ya kutosha sana hawa. Watafika mbali kama hawasambaratishwa .
Kwa vyovyote vile, kuwepo kwa upinzani nchini ni muhimu sana kwa mustakabali wa taifa. Kuna namna ambayo sisi kama taifa tukiondoa itikadi zetu tunaona tofauti kati ya wakati upinzani ulipokuwa na nguvu (2015 -2020) na hali ilivyo sasa. Ule uwezo wa kuisimamia serikali imedorora sana. Hivyo wale wa mashabiki wa chama tawala kama ni mzalendo wa kweli na hauongozwi na ushabiki na itikadi utaelewa kuwa ni muhimu sana kiwa na mtu wa kukukosoa, yeye atakupa nafasi ya kujitathmini, na nafasi ya kuona njia bora ya kuwatawala hao viumbe wenu.
 
Hii itakuwa kama 2019 na 2020.
Local government wakakataa
Uchaguzi mkuu wakaingia mazima kwakuwa uchaguzi mkuu uligusa maslahi yao ya Moja kwa moja.
 
TATHMINI YA MAANDAMANO NI ZERO HAKUNA KILICHOBADIRIKA , YAAANI YALE YALIKUWA MAANDAMANO AU MATEMBEZI TU? NANI ATAKUSIKILIZ AKWA MAANDAMANO YA AINA HIYO BIL AHATA MABOMU VURUGU NA KILA AINA YA FUJO NANI ANAKUSKILIZA NDIYO MANA MAMA KAWAJIBU KAWAAMBIA TUNAWAACHA WAANDAMANE NA ULIZNI TUNA WAPA WAKMALIZA KUTEMBEA WAKAE WAHUTUBIANE KISHA WASAMBAE MAKWAO KWISHA KAZI
 
Back
Top Bottom