Zungu wa ILALA kufuata nyayo za Rostam? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zungu wa ILALA kufuata nyayo za Rostam?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by FUSO, Aug 16, 2011.

 1. F

  FUSO JF-Expert Member

  #1
  Aug 16, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,813
  Likes Received: 2,297
  Trophy Points: 280
  Jana Mbunge wa Ilala Mh. Zungu aliijia juu wizara ya ardhi kwa kutaka kupoka eneo lote la jangwani magomeni kuwa la shughuli za michezo na mapumziko kwani wananchi walivamia eneo hilo la wazi. Zungu ametishia kuuachia hata ubunge wa Ilala ikibidi na kuungana na wananchi wake wote waliojenga Jangwani kuiburuza serikali mahakamani.

  Kwa sauti ya ujasiri zungu alisema " Mheshimiwa spika nipo na swaumu yangu nasema niko radhi kuuachia ubunge wangu wa Ilala na kujiunga na wananchi wangu kuipeleka serikali mahakamani kama mpango huu utaendelea, najua mnataka kutoka Masaki mje Magomeni kula ice cream, mimi hilo napinga. Hakuna aliyevamia eneo lile, lile eneo limevamiwa na vyura si raia. Narudia kusema siungi mkono HOJA hii asimili mia"

  Navyojua mimi kama bajeti hii itapita basi hilo eneo hilo lote lazima lichukuliwa na serikali kwa ajiri ya shughuli za viburudisho na michezo, na Je Zungu atatimiza ahadi yake hii? Ana roho ya ujasiri (roho ya paka) kama ya Rostam au anatishia nyau serikali yake ya CCM?
   
 2. J

  JACADUOGO2. JF-Expert Member

  #2
  Aug 16, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 930
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kwani Rostam alikuwa na roho ya ujasiri?
   
 3. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #3
  Aug 16, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,010
  Likes Received: 1,815
  Trophy Points: 280
  Mkuu nilimuona Zungu jana akinena kwa hisia kali. Unajua Zungu naye anaishi jangwani (amevamia). Hakika serikali inatakiwa ichukue eneo lote la jangwani na kuliboresha ili iwe pahala ambapo ni pa wananchi kupumzika. Jiji kubwa kama Dar linakosa sehemu ya kupumzika kwa wananchi wake kweli?
   
 4. Amiliki

  Amiliki JF-Expert Member

  #4
  Aug 16, 2011
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Kwani huyu Zungu ni Mbunge wa Chama gani? Si ni mmoja wa wale wanaofikiri kwa kutumia "Malalio"! Hao huwa wana mkwara wa Nanasi tu, Nje Miba lakini ukiingia Ndani wamejaa Utamu tuu. Pinda akiwapiga Mkwara tu wanarudi na kusema NDIOOOOOOOOOOOOOOOOOO!!!!!!!!!!!!!!!!!!.

  Kwanza aanze kufikiri kwa kutumia Ubongo ndio tutakubaliana na anachokisema.

  Bajeti itapita, na yeye hutamwona akiacha Ubunge. Anadiriki hata kuapa uongo kwa jina la Swaumu!
   
 5. N

  Nyadunga Member

  #5
  Aug 16, 2011
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 98
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 25
  Hawa magamba nao!! Wanapinga 100% halafu wanakuja kuunga 100%. Ukishasikia hivyo basi wawekezaji wameshapatikana. Maeneo ya wazi wameshagawa yote wamegeukia bonde la msimbazi. Wameshindwa kuondoa wavamizi katikati ya jiji na maeneo mengine wamerudia msimbazi. Tumekwisha. Prof. Tibaijuka aliingia kwa mbwembwe sasa yuko wapi?
   
 6. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #6
  Aug 16, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,446
  Likes Received: 5,833
  Trophy Points: 280
  Hivi mnajua kwanini anaitwa ZUNGU?.......Sio kwa rangi yake
   
 7. F

  FUSO JF-Expert Member

  #7
  Aug 16, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,813
  Likes Received: 2,297
  Trophy Points: 280
  ni kweli lazima jiji la kubwa kama dar kuwa na sehemu za wazi za mapumziko, lakini ni eneo la jagwani tu lilikokuwa limetegwa kuwa la wazi? ningependa sana kama serikali ingechukua maeneo yote ya wazi waliogawiana then waje na hii option. lakini hoja hii inaonekana kama uonevu kwa watu waliojenga pale jagwani. Waziri kashindwa kuyarudisha maeneo mengi tu ya wazi yaliyoporwa na vigogo na wafanyabiashara wakubwa lakini laliona hili la magomeni peke yake sababu waliojenga pale ni wananchi maskini?
  Hiki ndicho kilio cha Zungu pamoja na wapiga kura wake.
   
 8. The Emils

  The Emils JF-Expert Member

  #8
  Aug 16, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 570
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mungu wangu magamba wanatumaliza hata hilo eneo la msimbazi limepata mwekezaji?????
   
 9. Erick G. Mkinga

  Erick G. Mkinga Member

  #9
  Aug 16, 2011
  Joined: May 19, 2011
  Messages: 62
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kama wamevamia wanabidi watoke..sio habari za kutaka tukapate ice cream..nini maana ya jiji sasa kama kila sehemu wanatakiwa wakae watu...kuna maeneo maalumu ya kupumzika,michezo,na mengineyo..Zungu asitusumbue kama eneo lilikowa kwa ajili ya kupumzikia basi serikali iwatoe tena bila fidia.
   
 10. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #10
  Aug 16, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,446
  Likes Received: 5,833
  Trophy Points: 280
  Jiji nalo hukitaji kupumua pia......
   
 11. suleym

  suleym JF-Expert Member

  #11
  Aug 16, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,714
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  jangwani mkuu, kwa jinsi alivyokuwa anachangia zungu na kauli alizokuwa anazitoa dhidi ya waziri wa wizara kwa ujumla angekuwa wa upinzani 4 sure ungeombwa muongozo, alitumia kauli kali sana tusubiri majibu ya waziri jioni ili 2one kama zungu atajiuzuru kama majibu yatakuwa kinyume na matakwa yake.
   
 12. F

  FUSO JF-Expert Member

  #12
  Aug 16, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,813
  Likes Received: 2,297
  Trophy Points: 280
  kweli mkuu, ile hisia ya huyu mbunge ilionyesha kuwa yupo tayari kwa lolote, na kama wengi wa wachangiaji wa hii mada wangepata sound clip yake wangekubaliana na mimi kwamba endapo waziri ataendelea na zoezi lake la kutaifisha ile ardhi basi tunaweza kuwa na uchaguzi mdogo ilala.

  Mimi si mwanamagamba ila kwa hili la jana - zungu ameonyesha usimamo wa dhati kutetea wananchi wake. Wabunge wengi huwa wana dukuduku zao nyingi tu ila wanashindwa kuzitoa bungeni kuogopa fagio la chuma la wanamagamba.

  Hakuna anayeunga mkono ujenzi holela lakini kwa nini wananchi wanafikia hatua ya kujenga kiholela?
   
 13. s

  sativa saligogo Senior Member

  #13
  Aug 16, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 126
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu,hiyo rangi hapo kama kweli atakuwa mtanzainia wa pili mwenye asili ya asia wa kujivua gamba???? lkn yawezekanaje m-asia amwonee uchungu m-tz (black) ??????? isijekuwa ipo special interest hapo, perhaps anataka kujiuzulu kukwepa ile scandle ya DDC ie. hon masaburi-saga!!!!!
  ammo-te!!!
  UKISTAAJABU YA MUSA UTAONA YA .......................???????
   
 14. Amiliki

  Amiliki JF-Expert Member

  #14
  Aug 16, 2011
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Kwani ameacha biashara ya "Bwimbwi"! Katuumizia sana vijana wetu pale Kariakoo.
   
 15. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #15
  Aug 16, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  hayo ni mabaki ya wagiriki ndo maana wanamwita Zungu,kama kuna jingine zaidi ya hilo tujuze!!!!!!!!!!!!!!!
   
 16. m

  mfngalo Member

  #16
  Aug 16, 2011
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 87
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Zungu jn kaongea sn kwa hisia 2subili 2majibu ya leo jion
  ope watamsikiliza ha2taki uchaguz mdogo wa ilala
   
 17. m

  mfngalo Member

  #17
  Aug 16, 2011
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 87
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  <br />
  <br />
  Jaman Zungu c ni jina km majina mengine mbona mna2mia kufikiri kwa masahuri n abt kuwaaribia watoto coz of...mnaprove o mnasema 2
  mi c gamba bt kunamengine ni 2much sa2
   
 18. N

  NDOFU JF-Expert Member

  #18
  Aug 16, 2011
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 656
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kwanza natangaza interest' mim ni afisa mipango miji mtarajiwa(nipo mwaka wa nne) Tatizo la miji Tanzania 1. ni kuingiliwa na siasa 2.Uchache wa wataalamu wa ardhi(waliopo ni 24% tu) 3.Rushwa.Hotel ya Golden tulip ilipelekea umbali kutoka kwenye vyanzo vya maji(BUFFER ZONE) Kupunguzwa kutoka mita 200 mpaka mita 60-kuna waziri alihusika kubadili hizo standards ili jamaa wakaribie bahari.(rushwa) ndio maana leo hata beach zinamilikiwa na watu binafsi.Maeneo ya wazi kama hilo la jangwani na mengine kwanza ni siasa(vimemo) kwenda kwa watu wa ardhi (mimi kama meyor nakuagiza mpe hilo eneo!) na rushwa pia ndio maana maeneo hayo yanajengwa pia wanasisa wanaogopa kuwaondoa watu waliovamia wakihofia kupoteza wapiga kura wao! NTARUDI BAADAYE.
   
 19. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #19
  Aug 16, 2011
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,850
  Likes Received: 2,425
  Trophy Points: 280
  COPLO ZUNGU ...[alikuwa coplo JWTZ]...lazzima kuenzi vyeo vyetu...mbona kulikuwa na Sergent Samuel doe..sio kuwwachia maafisa tu ndio watambie vyeo....

  HUYU ZUNGU NI MJINGA SANA....HIVI PALE JANGWANI KUNA NYUMBA AU VIBANDA VYA TOPE....AACHE SIASA..ANATETEAJE WATU KUKAA KWENYE MAZINGIRA HATARISHI...YOTE HII NI KURA TU ANATAKA..KWA WAJINGA WENZAKE..WANAOISHI MABONDENI...WANAPOKUFA KWA MAFURIKO ANAFURAHIA??

  NI MUHIMU ENEO LOTE LA JANGWANI KUANZIA SALENDA BRIDGE NA MABONDE YOTE JIJINI YAKAGEUZWA KUWA GREEN ZONE...NA ZIJENGWE AMUSEMENT PARKS AND SPORTS FACILITIES..TENA TUANZISHE KABISA CHOMBO KUDHIBITO BONDE LA JANGWANI ...SEHEMU NYINGINE TUWEKE MASHAMBA YA MBOGA MBOGA...VUNJA VUNJA MABONDE YOTE DAR NA SIO JANGWANI TU ..HATA KEKO,....NA KULE MTONI..KOTE!!
   
 20. M

  Mkwe21 JF-Expert Member

  #20
  Aug 16, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,834
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  Hili ndio Tatizo la Miji Mikubwa Kama Dar es Salaam Kuwa na Viongozi BOGUS!! Just anaongea Kujifurahisha ili aonekane anatetea!! Dar es Salaam yote imekuwa Slums (Squatter) kutokana na kuwasikiliza watu kama hawa ambao wanafikiri kutumia MASABURI!! For any sustainable cities planning must be a key thing for proper environment!! Nadhani alitakiwa aulize je Hawa wavamizi tutawafidia Vipi? Ila nisingependa kuwaita wavamizi kwani Dar es salaam limekuwa moja ya majiji duniani ambayo hayana any Master plan, Hivyo kila mtu hujifanyia mambo yake kutokana na urefu wa kamba yake!! (Financial Capabilities)
   
Loading...