Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,007
- 9,873
Mbunge wa Ilala, Azzan Zungu, alipendekeza kuwepo kwa kodi ya Uzalendo itakayokatwa kila siku kupitia Mitandao ya Simu kwa kila Mtanzania ili kuwa chanzo kipya cha mapato kwa Serikali.
Zungu amejibu kwa ku-comment kwenye ukurasa wa Instagram wa JamiiForums akieleza kuwa Tsh. Bilioni 540 alizotaja sio kwa siku bali zitakusanywa kwa mwaka.
Pia amewataka wananchi kufikiria mahitaji ya elimu, huduma za afya na barabara ambazo zinapaswa kugharamiwa.
Zungu amesema mitandao ya simu imefanya watu waishie kupigiana simu na kuokoa kiasi cha nauli ambacho wangetumia kuwatembelea ndugu zao. Hivyo sio mbaya kulipa kodi.
ZAIDI SOMA
- Azzan Zungu ataka uwepo wa kodi ya uzalendo itakayokatwa kwenye Mitandao ya simu kwa kila Mtanzania