Zumari ikipulizwa zanzibar wanadimka hadi maziwa makuu.

umenikumbusha ni swali pekee nililokosa kwenye mtihani wa historia wa kidato cha pili enzi za Makwetta. They whisper in ....... they dance at..........
 
Hawa ni warabu wenye kujiita wazanzibar.
Maelezo yameegemea zaidi katika historia ya kuivamia Zanzibar,
Hii yote ni kupiga kelele ili Sultan wa Zanzibar arudi eti waukate
Dawa ni kuwa na serikali moja tu ya Tanzania.

eeh! Dawa ni wao kutoka zao.
 
take your Zenj and go! Cha ajabu kuna wazenj kwenye maoni ya katiba wanang'ang'ania muungano. Wapuuzi
 
Muungano hausadii pande zote mbili kisiasa na kiuchumi. Tanganyika na znz zitafanya vizuri kama kila moja ikiwa huru kabisa.

Sasa Tatizo ninaloona mimi ni katika sheria za kimataifa nchi inayopakana na bahari ina access au kumiliki maili 600 za mipaka ya bahari yake (zanzibar ipo maili 21 tu! toka mwambao wa Tanganyika). Hapa sasa ni shida, zanzibar itakuaje nchi katika bahari ya Tanganyika? nani atavua samaki katika maili 600 hizi?, madini na maliasili nyingine za majini zitakua za nani sasa?. Hili ni mojawapo ya matatizo makubwa ya kuvunjwa kwa muungano huu..Nakumbuka Nyerere aliwahi kusema privately, kama angeweza kuisogeza znz mbali huko baharini ingekua kitu kizuri sana kwa tanganyika.
 
Written by Said-Said // 14/07/2012 // Habari // 5 Comments


(Amri zikitoka Zanzibar kwenda Oman, Tanganyika na maeneo mengine ya afrika)
Nianze makala yangu kusimulia kwamba wengi hawajui nini ZANZIBAR na hapa ndipo wanapopata tabu kukubali ukweli unaozungumzwa na wazanzibari kudai mamlaka ya taifa lao.
Zanzibar ikijuulikana tokea zamani (miaka mia tano kabla kuzaliwa nabii Issa), ilikua ni dola yenye nguvu sana kipindi hiko hata mataifa makubwa yakija kukopa Zanzibar na yakiitambua Zanzibar kwa heshma iliyonayo na wasifu wake wa kiutawala, eneo lake lilianzia kaskazini Kismayuu hadi Msumbiji sofala (kuanzia hapa zanzibar ya sasa hadi kongo) hii ilikua kabla ya kukatwana kugawiwa na na wakoloni, na ndio mana katiba yetu (Baada ya marekebisho ya 10) inatambua mipaka yetu kwa kuviongelea mpaka visiwa vidogo vidogo kama ni sehemu halali za Zanzibar.
Zanzibar ni Dola kongwe miongoni mwa dola za Afrika na ndio mana katika ramani iliyogunduliwa na chuo kikuu cha Oxford uengereza iliyochorwa katika karne ya kumi na moja viswa vya unguja na pemba vilikuwemo na makao makuu yake yalikuwa unguja ukuu, katika ramani hiyo hakuna Tanganyika.
Zanzibar ilitambulikana kuwa dola huru mnamo mwaka 1832, hadi mataifa makubwa ya magharibi yakafungua balozi zao Zanzibar, Kwa mfano Marekani alifungua balozi yake hapa mnamo mwaka 1837 na mwingireza nae akafungua balozi yake 1841, ufaransa akafungua balozi yake hapa 1844 na ujerumani akafungua nae mwaka 1847, hakuna nchi yeyote kusini mwa jangwa la sahara iliyokua ikijuulikana kama dola na kuwa na mahusiano ya kibalozi na mataifa makubwa zaidi ya Zanzibar.
Zanzibar ilikuwa na Benki kuu yake na pesa zake, na uchumi wake ulikua ni mzuri kuzidi mataifa mengi tu, ukenda WORLD BANK wakikupa takwimu za kifedha za miaka ya Raisi Karume Utakuta ni Nchi ya pili ama ya tatu kiuchumi kwa afrika (wachumi huita GDP), huku ikiwa na akiba ya Paundi milioni 800 katika banki ya kiengereza.
Zanzibar kibiashara ilijuulikana kama "THE INTERNATIONAL TRADE GATE WAY" LANGO KUU LA KIBIASHARA, serikali za wakati huo zikijifunza biashara kutoka hapa kwakua na uzoefu mzuri wa kuendesha biashara za ndani na nje ya nchi. Zanzibar ilikua ni kituo kikuu kibiashara, kisiasa na kiuchumi katika miaka hiyo.
Historia ya Zanzibar bado imbaki ya kipekee na imeshazungumzwa sana nyakati tofauti, nimekusudia kugusia haya ili kuwaomba wenzangu turejeshe mamlaka yetu ya utawala wa zanzibar.
Wazee wetu walitabiri na kusema "UTAWALA WA ZANZIBAR UTARUDI NA UTAKUWA NA NGUVU ZAIDI KULIKO ULE WA ZAMANI" M/mungu athibitishe maneno haya ya wazee wetu.

Amini ninakwambia kama Zanzibari ingekuwa na aina hiyo ya nguvu kimamlaka na kiutawala, leo hii tungeona japo mabaki ya katika damu na mioyo yenu, lakini hali ilivyo sasa ni kinyume kabisa, mmebaki kuwa walalamishi wenye malamiko ya kufikirika.
Mnaendelea kujipoteza kwa ku-fake historia ili kujenga vichwani mwa watu aina ya asili ambayo hamjawahi kuwa nayo. Hivi mwarabu kupita Tanganyika kutafuta watumwa hadi kongo ndiyo kutawala? Unafahamu maana ya halisi ya kutawala? au unaweza kutuonyesha kumbukumbu za wazanzibar ziliopo huku bara? kama zile za mjerumani yaani maboma, mashamba, mashule, miundo mbinu jeshi, n.k? unaweza ukatuonyesha hivyo ili kuthibitisha dhana yako ya Zanzibar kuwahi kuwa mtawala?
Zanzibar yenyewe ilikuwa ikitawaliwa na hapo kilikuwa ni kituo cha kusafirisha wakoloni kwenda uarabuni ina maana unaisifia zanzibar ya mwarabu? Inakuwaje pamoja na kuwa mlikuwa dola yenye 'nguvu' mkaja kutawaliwa na taifa ambala halikuwepo au mlikuwa mkilitawala (Tanganyika).
Acheni upumbavu fikirini kama watu walipo katika Dunia halisi....mnazidi kujipoteza na hizo historia ambazo hazijawahi kuwepo....mnaona nini kuwaambia mawaziri waliopo katika serikali ya muungano warudi kwenu, makamu wa rais arudi kwenu wafanyakazi na wafanyabiashara na wengineo warudi kwenu ili mjitenge...Mzee Mwanakijiji aliandika kwa lengo la kuwapa ushauri mbona sijamuona jasiri miongoni mwenu aliyethubutu kuufanyia kazi? Mnaogopa kufa njaa? au mnaogopa kuchinjana?
Tuondoleeni alfa lela olela zenu.....watu wenyewe mnabebwa bebwa, kama mnajiamini fuateni ushauri wa Mzee Mwanakijiji......nyamafu.
 
Kazi ipo kama kweli waZNZ wenye akili timamu wanajiona hivyo. I wish wangejitokeza waseme huyu aliyetoa huo msimamo ni wake binafsi na wanawasiwasi na afya yake ya akili. Badala yakufikiria mambo ya msingi yakujenga nchi unazungumzia historia isiyo na mashiko..

Vyanzo vipi vya mapato ambavyo Znz inavyo vyakuifanya iwe dola imara lenye nguvu? nisaidien wana JF.. msitaje mafuta ambayo bado yapo kwenye mchakato.
 
Zanzibar ni Dola kongwe miongoni mwa dola za Afrika na ndio mana katika ramani iliyogunduliwa na chuo kikuu cha Oxford uengereza iliyochorwa katika karne ya kumi na moja viswa vya unguja na pemba vilikuwemo na makao makuu yake yalikuwa unguja ukuu, katika ramani hiyo hakuna Tanganyika.

underline: imenifanya nisiendelee kusoma, hapo ni sawa na kusema visiwa vya zenji viligunduliwa kabla ya bara la africa. Unaweza kujiuliza maswali mepesi
-nchi ya Tanganyika imeaanza lini? kabla ya hapo kipindi cha wajerumani mipaka ilikuwa vipi? na kabla ya wajerumani kulikuwa na mipaka gani huku africa?
-tukiendelea mbele zaidi tutaanza kuuliza asili ya watu wa zenji
 
Wazanzibar hawana shida na muungano,
Waarabu wote na wale wadhaniao ni waarabu ndo shida.
Wanataka utawala wa Sultani,
Weusi Zanzibar hawatakuwa na nafasi wala haki.
Ubwana na Utwana utarudi Zanzibar[/QUOT

dah hii kazi ipo
 
Muungano hausadii pande zote mbili kisiasa na kiuchumi. Tanganyika na znz zitafanya vizuri kama kila moja ikiwa huru kabisa.

Sasa Tatizo ninaloona mimi ni katika sheria za kimataifa nchi inayopakana na bahari ina access au kumiliki maili 600 za mipaka ya bahari yake (zanzibar ipo maili 21 tu! toka mwambao wa Tanganyika). Hapa sasa ni shida, zanzibar itakuaje nchi katika bahari ya Tanganyika? nani atavua samaki katika maili 600 hizi?, madini na maliasili nyingine za majini zitakua za nani sasa?. Hili ni mojawapo ya matatizo makubwa ya kuvunjwa kwa muungano huu..Nakumbuka Nyerere aliwahi kusema privately, kama angeweza kuisogeza znz mbali huko baharini ingekua kitu kizuri sana kwa tanganyika.

umekosea dogo ! Tanganyika haina bahari wewe,angalia geograghy vizuri,usione tanganyika iko karibu na bahari ukajua ni yake,zanzibar ipo kabla haijazaliwa kongo,tanganyika na kenya ! Tanganyika mwisho chumbe ukivuka hapo ugomvi.
 
Wanzazibari ni bora mfanye kila liwezekanalo mvunje muungano tena mkishauvunja mbebe na visiwa vyenu mwende navyo Arabuni hilo nadhani ndio litakuwa suluhisho.
 
umekosea dogo ! Tanganyika haina bahari wewe,angalia geograghy vizuri,usione tanganyika iko karibu na bahari ukajua ni yake,zanzibar ipo kabla haijazaliwa kongo,tanganyika na kenya ! Tanganyika mwisho chumbe ukivuka hapo ugomvi.


Toa vigezo kamilifu kunielimisha (kama unafikiri sijui) ramani ya jiografia haijibu wala kusaidia hoja yako. Unajua sheria za kimataifa kuhusu matumizi ya Bahari au unakimbilia ushabiki wa kijinga. Hamna nchi inayopakana na bahari ikaamrishwa isitumie maji yale kwa sababu zako za kipuuzi.

Tanganyika ikiwa huru chini ya sheria ya kimatiafa inarithi umiliki wa 22 km za bahari toka mwambao wa Tanganyika hii ni kutokana na 1982 international convetion of the law of the sea. Kila nchi inayopakana na bahari kuna kitu kinaitwa territorial waters (nafikiri unajua kwa nini wasomali wanateka zile meli za kigeni) Kama ilivyo Cuba na Marekani (wameachana umbali wa maili 90) wamarekani wanamiliki maili 14 na cuba maili 14, katikati yao ni maji ya kimataifa.

sasa nyie wazanzibari mko maili 21 au km 36 toka Tanganyika na hili nilikua nasema ni tatizo kwa sababu kila mmoja hawezi kufikisha maili 14 zake kwa mujibu wa taratibu na sheria za kimataifa.... Kuhusu maili 600 hii inaruhusiwa kuombwa kwenye jumuia husika za kimataifa umiliki wa maji ya bahari ya umbali huu, kama juzi Tibaijuka alivyoomba hizo maili.

jifunze kujibu kwa kutumia vigezo muda mwingine
 
Ni kweli hatuna,
Lakini msidhani mkichukua Zanzibar eti ukanda wa pwani huku bara ni sehemu ya Zanzibar.
Hilo litakuwa ni Tangazo la vita.

Ili uwe mtu huko Zanzibar ni lazima uwe na kadamu ka kiarabu,
Ukikosa damu ya kiarabu basi hata vijindevu vya suna uwenavyo.
Waarabu Zanzibar ni sawa na Makaburu kule South Afrika
Ni wakuja, walowezi na wakoloni.

Eti TipRip ni moja kati ya mashujaa wenu??

Yule mkamata watu na kuwauza huko Omani kama ndezi??

Mtu anauzwa sawa sawa iuzwavyo kanzu??

Ustaarabu uko wapi?


Nyie watanganyika ndo mnakioloniwa nyuma ya pazia ebu angalia madini yanachimbwa na wazungu kwa mgawo wa 3% wala hawalipi kodi!kweli mna akili nyie?
 
Back
Top Bottom