Zumari ikipulizwa zanzibar wanadimka hadi maziwa makuu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zumari ikipulizwa zanzibar wanadimka hadi maziwa makuu.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by abdulahsaf, Jul 14, 2012.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  Jul 14, 2012
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  [h=1][​IMG][/h]Written by Said-Said // 14/07/2012 // Habari // 5 Comments


  (Amri zikitoka Zanzibar kwenda Oman, Tanganyika na maeneo mengine ya afrika)
  Nianze makala yangu kusimulia kwamba wengi hawajui nini ZANZIBAR na hapa ndipo wanapopata tabu kukubali ukweli unaozungumzwa na wazanzibari kudai mamlaka ya taifa lao.
  Zanzibar ikijuulikana tokea zamani (miaka mia tano kabla kuzaliwa nabii Issa), ilikua ni dola yenye nguvu sana kipindi hiko hata mataifa makubwa yakija kukopa Zanzibar na yakiitambua Zanzibar kwa heshma iliyonayo na wasifu wake wa kiutawala, eneo lake lilianzia kaskazini Kismayuu hadi Msumbiji sofala (kuanzia hapa zanzibar ya sasa hadi kongo) hii ilikua kabla ya kukatwana kugawiwa na na wakoloni, na ndio mana katiba yetu (Baada ya marekebisho ya 10) inatambua mipaka yetu kwa kuviongelea mpaka visiwa vidogo vidogo kama ni sehemu halali za Zanzibar.
  Zanzibar ni Dola kongwe miongoni mwa dola za Afrika na ndio mana katika ramani iliyogunduliwa na chuo kikuu cha Oxford uengereza iliyochorwa katika karne ya kumi na moja viswa vya unguja na pemba vilikuwemo na makao makuu yake yalikuwa unguja ukuu, katika ramani hiyo hakuna Tanganyika.
  Zanzibar ilitambulikana kuwa dola huru mnamo mwaka 1832, hadi mataifa makubwa ya magharibi yakafungua balozi zao Zanzibar, Kwa mfano Marekani alifungua balozi yake hapa mnamo mwaka 1837 na mwingireza nae akafungua balozi yake 1841, ufaransa akafungua balozi yake hapa 1844 na ujerumani akafungua nae mwaka 1847, hakuna nchi yeyote kusini mwa jangwa la sahara iliyokua ikijuulikana kama dola na kuwa na mahusiano ya kibalozi na mataifa makubwa zaidi ya Zanzibar.
  Zanzibar ilikuwa na Benki kuu yake na pesa zake, na uchumi wake ulikua ni mzuri kuzidi mataifa mengi tu, ukenda WORLD BANK wakikupa takwimu za kifedha za miaka ya Raisi Karume Utakuta ni Nchi ya pili ama ya tatu kiuchumi kwa afrika (wachumi huita GDP), huku ikiwa na akiba ya Paundi milioni 800 katika banki ya kiengereza.
  Zanzibar kibiashara ilijuulikana kama “THE INTERNATIONAL TRADE GATE WAY” LANGO KUU LA KIBIASHARA, serikali za wakati huo zikijifunza biashara kutoka hapa kwakua na uzoefu mzuri wa kuendesha biashara za ndani na nje ya nchi. Zanzibar ilikua ni kituo kikuu kibiashara, kisiasa na kiuchumi katika miaka hiyo.
  Historia ya Zanzibar bado imbaki ya kipekee na imeshazungumzwa sana nyakati tofauti, nimekusudia kugusia haya ili kuwaomba wenzangu turejeshe mamlaka yetu ya utawala wa zanzibar.
  Wazee wetu walitabiri na kusema “UTAWALA WA ZANZIBAR UTARUDI NA UTAKUWA NA NGUVU ZAIDI KULIKO ULE WA ZAMANI” M/mungu athibitishe maneno haya ya wazee wetu.
  Utawala ni kitu kikubwa sana, na kujitawala ni bora kuliko kutawaliwa, kujitawala ni ile hali ya kuwa na mamlaka kamili ya kuendesha serikali bila ya kuingiliwa na upande wowote.
  Hivyo basi ili kuwa na utawala kamili wenye nguvu zake kimadaraka turudishe yafuatayo:-
  1. Mambo ya Nje na uhusiano wa kimataifa
  2. Ulinzi na usalama (Jeshi kamili la Zanzibar kama ilivyokua Nyuki)
  3. Polisi.
  4. Mamlaka yanayohusiana na mambo ya hatari.
  5. Uraia wa Zanzibar.
  6. Uhamiaji liwe chini ya Zanzibar.
  7. Mikopo na biashara ya Nchi za Nje.
  8. Bandari, mambo yanahusiana na usafiri wa anga, posta na simu.
  9. Benki Kuu, Mambo yote yanahusiana na sarafu na fedha kwa ajili ya malipo yeyote halali (pamoja na noti), Mabenki (pamoja na mabenki ya kuweka hakiba) na shughuli zote za kibenki, fedha za kigeni na usimamizi wake.
  10. Leseni ya viwanda na takwimu.
  11. Elimu ya juu.
  12. Maliasili ya Mafuta.
  13. Usafiri na usafirishaji wa anga.
  14. Utafiti.
  15. Vyama vya siasa view chini ya mamlaka ya Zanzibar.
  Haya tukiyadai yakarudi na kuyaweka katika katiba yetu ya Zanzibar yatakidhi yale marekebisho ya 10 ya katiba ya Zanzibar.
  Katika maswala haya na maslahi ya Zanzibar tuache kuchezewa na wanasiasa, sisi tunakuwa na tunazaa tuwaandalie urithi mwema vizazi vijavyo, kutumiwa kisiasa ni kosa kubwa lililotufikisha tulipo mpaka viongozi wetu wakayagawa mamlaka yetu DODOMA.
  Vyama hivi vya siasa vinazaliwa na kufa (kwakua ni fikra na mawazo tu ya kundi Fulani la watu wanaosaka mamlaka ya kuendesha Nchi), ila Zanzibar ilikuwepo na itaendelea kubakia, ikibaki na mamlaka kamili ndio utakua natija kwetu na urithi mwema wa vizazi vyetu.
  AHSANTENI SANA
   
 2. W

  Wimana JF-Expert Member

  #2
  Jul 14, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 2,453
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 145
  Weye Abdulahsafu wacha urongo yakhe. Hiyo historia ya Zanzibar kuanza miaka 500 KK umeivumbua wapi? Historia ya Zanzibar inaanza pale Seyid Said alipohamia Zanzibar kwenye karne ya 9, ya huko nyumba umeyapata wapi?
  Kuhusu Tanganyika kutokuwapo ktk ramani enzi hizo ni sawa maana Tanganyika ilikuja kuwepo baada ya wakoloni kugawana Afrika, ambapo Wajerumani waliita Deutche East Africa Rwanda na Burundi zilikuwa sehemu ya Germany East Africa, kabla kulikuwa na himaya za kikabila tu kama Unyanyembe nk
   
 3. F

  Falconer JF-Expert Member

  #3
  Jul 14, 2012
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 658
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 60
  Wimana, samahani ndugu yangu. Historia imekupita. Siwezi kukulaumu ila ni mfumo wa elimu ndio unaozaa tatizi hizi. Sisi wazenji tulikuwepo zamani sana na tutakuwepo hadi liamba. Historia yetu na mchango wetu katika medani za dunia zipo na zitabaki. Wenzetu nyinyi ni porojo mitaani tu. Munaikataa historia kwa kujifanya wajuaji mno wakati hamuna munachokijua.
  Basi nawaambia kuwa Sultan Seyyid Said alikuja zanzibar kwa sababu ya kumuondosha mkoloni wakireno na akafanya zanzibar makao yake makuu na akatawala Omani kutoka Zanzibar. Hawa ndio waliotuletea utajiri Zanzibar kwa nguvu za Allah Subhan wataala. Leo sisi wazanzibari tumeamua hatutaki tena kutawaliwa na process ya kuvunja muungano imeanza kupitia mchakato wa katiba. Hata tutakapo maliza mchakato huu na muungano utakuwa maiti. Sasa hivi muungano upo ICU na tunazidi kuhakaikisha hadhi ya zanzibart inarudi. Leo, baraza la wawakilishi limepitisha "ZANZIBAR PETROLEUM AND ENERGY EXPLORATION" kuangalia usimamizi wa nishati na mafuta ya Zanzibar. Nyinyi kaeni mukitutusi tu. Ngoma imenoga.
   
 4. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #4
  Jul 14, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,876
  Likes Received: 6,230
  Trophy Points: 280
  hata ingekuwepo kwenye ramani toka enzi za adamu na hawa.....

  Bado zigo la misumari haibebeki.....
  Nashangaa watanganyika mnaing'ang'ania nini?
   
 5. Jagermaster

  Jagermaster JF-Expert Member

  #5
  Jul 14, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 656
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ya Zanzibar kigeographia iko sehemu nzuri sana, mkipanua bandari yenu itatumika kuingiza bidhaa katika nchi za Kenya, Tanganyika, Somalia na Mozambique kwa kuwa nchi hizi hazitakuwa na bandari zao. Na population ya Zanzibar ni kubwa sana inatosha kabisa kuwa soko kubwa sana kwa cargo kubwa sana itakayokuwa inaingizwa hapo Zanzibar. Harafu Tanganyika ni watu wakarimu sana, baada ya muungano kufa watawaruhusu tu mpitishe biashara zenu hapo kuzipeleka mpaka Zambia, DRC, Malawi na Rwanda kama sasa mnavyofanya sasa kwa kupitisha bidhaa za maredio used kutoka arabuni.
   
 6. J

  JokaKuu Platinum Member

  #6
  Jul 15, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,815
  Likes Received: 5,134
  Trophy Points: 280
  Abdulahsaf,

  ..They used to say, "the sun never sets in the British empire." Sasa hivi Uingereza siyo dola ile yenye maguvu na mabavu tena.

  ..Uhusiano wa Tanganyika na Zanzibar unaweza kufananishwa na ule wa Mmarekani na Muingereza. Kihistoria Marekani ilikuwa koloni la Muingereza, lakini leo hii mambo yamemchachia Muingereza kiasi kwamba amebakia kuwa kibaraka tu wa Marekani.

  ..Zanzibar nayo kuna kipindi ilikuwa na mabavu. Sultani wa Zanzibar na vibaraka wake walikuwa wana-terrorize Tanganyika nzima mpaka Congo kwa kukamata watumwa na kuwauza kwa Wazungu. Leo hii mambo yamebadilika. Tatizo ni kwamba mabavu hayo yalianza kupungua kidogo kidogo mpaka ikafikia Sultani wa Zanzibar akatawaliwa na Waingereza.

  ..hata eneo alilokuwa "akitawala" Sultani wa Zanzibar nalo lilendelea kupungua. Kwa mfano baada ya Berlin Conference, Wajerumani walichukua eneo la Tanganyika mpaka Rwanda na Burundi, wakati Sultani akiachiwa 10 miles coastal strip, pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba. Baada ya muda[around 1890], Sultani akapiga bei the 10 miles coastal strip, na kubakiwa na visiwa vya Zanzibar pamoja na eneo la Mombasa. Kabla ya uhuru wa Kenya, Sultani akawauzia Wakenya eneo la Mombasa.

  ..Sultani aliendelea kudhoofika kimadaraka mpaka kufika 1963 akawa na hadhi ya Constitutional monarch, yaani ni mtu "ceremonial" tu. Hali haikuishia hapo, 1964, siku ya MAPINDUZI MATUKUFU, Sultani akafurumushwa toka Zanzibar na mzao[Waafrika/weusi wa Znz] wa wale aliokuwa akiwauza utumwani. Sultani akakimbilia Mombasa ambako Kenyatta alikataa kumpa hifadhi. Baada ya hapo nasikia akaja Tanganyika ambapo alihifadhiwa na Nyerere mpaka pale Waingereza walipokubali kumpa hifadhi.

  ..I could go on, lakini naomba niishie kwa kueleza kwamba Zanzibar ya sasa imebakia kuwa omba-omba kwa Tanganyika. Baada ya zao la karafuu kuporomoka Zanzibar imetetereka kiuchumi kiasi kwamba sasa hivi inapumua kwa msaada[umeme bure, mishahara ya watumishi, ulinzi na usalama] wa Tanganyika.
   
 7. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #7
  Jul 15, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,876
  Likes Received: 6,230
  Trophy Points: 280
  znz ni sawa na zigo la misumari, halibebeki!
   
 8. UKI

  UKI JF-Expert Member

  #8
  Jul 15, 2012
  Joined: Jun 12, 2012
  Messages: 699
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  sijui kwanini bado watanganyika mnatumia muda wenu kwenye huu muungano ambao sioni umenisaidia nini na kwanini tuwalazimishe tuendelee kuwa nao hawa jamaa tuwaache waende zao hatuwataki bana, itatusaidia sana hili tukiachana nao warudi kwaoooooooooooo tuachiwe kariakoo yetu na ilala yetu maana huko ndio wamejaa kama nini
   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #9
  Jul 15, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,394
  Trophy Points: 280
  hizi porojo nyingine muwe mnapigiana huko huko kwenye Zumari!!! utaona vitu viwili havitajwi kabisa katika hiyo historia feki ya "Zanzibar"!!!!
   
 10. Msalagambwe

  Msalagambwe JF-Expert Member

  #10
  Jul 15, 2012
  Joined: Jul 11, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Hawa ni warabu wenye kujiita wazanzibar.
  Maelezo yameegemea zaidi katika historia ya kuivamia Zanzibar,
  Hii yote ni kupiga kelele ili Sultan wa Zanzibar arudi eti waukate
  Dawa ni kuwa na serikali moja tu ya Tanzania.
   
 11. Msalagambwe

  Msalagambwe JF-Expert Member

  #11
  Jul 15, 2012
  Joined: Jul 11, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Wazanzibar hawana shida na muungano,
  Waarabu wote na wale wadhaniao ni waarabu ndo shida.
  Wanataka utawala wa Sultani,
  Weusi Zanzibar hawatakuwa na nafasi wala haki.
  Ubwana na Utwana utarudi Zanzibar

   
 12. A

  Alhabaad Member

  #12
  Jul 15, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 72
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wacha propaganda za kizamani ww!hii karne nyengine babu ww vp!?
   
 13. A

  Alhabaad Member

  #13
  Jul 15, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 72
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tafuteni probaganda nyengine hii ishachusha haina soko tena!!!
   
 14. A

  Alhabaad Member

  #14
  Jul 15, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 72
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ww mzee mwaka huu utakufa nacho kijiba cha roho!kamfufue Baba yako wa taifa aje azuie.Jamhuri ya Watu wa Zanzibar Kwanza Shengesha baadae upooooo!!
   
 15. fyddell

  fyddell JF-Expert Member

  #15
  Jul 15, 2012
  Joined: Dec 19, 2011
  Messages: 2,082
  Likes Received: 774
  Trophy Points: 280
  2kiwapa mamlaka kamili hawa waz'bari watadai 10miles ohoo.
   
 16. Msalagambwe

  Msalagambwe JF-Expert Member

  #16
  Jul 15, 2012
  Joined: Jul 11, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Mnamatusi mkisha fuga ndevu!

   
 17. mgen

  mgen JF-Expert Member

  #17
  Jul 15, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 15,195
  Likes Received: 1,914
  Trophy Points: 280
  ooh mie ni mwinyi! mie ni mwinyi! huku shati limepasuka, na umeshona ndala na waya! daah! ahahahahaaa! unachekesha bro!
   
 18. mgen

  mgen JF-Expert Member

  #18
  Jul 15, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 15,195
  Likes Received: 1,914
  Trophy Points: 280
  z'bar kwishney! Yaliyo pita si ndwele mgange yajayo;
   
 19. simplemind

  simplemind JF-Expert Member

  #19
  Jul 15, 2012
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 11,813
  Likes Received: 2,586
  Trophy Points: 280
  Ni self evident truth zumari la uamsho llikipigwa kisawasawa litatikisa hadi Kigoma.
   
 20. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #20
  Jul 15, 2012
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,187
  Likes Received: 1,189
  Trophy Points: 280
  Hiv wazenji wote wanaamini hivyo? "ujio wa waarabu zanziba siyo ukolon, ujio wa wazungu wa ulaya huko zanzibar ni ukoloni!
   
Loading...