ZUKU TV mbioni kunipoteza mteja mimi

Aniko

JF-Expert Member
Jan 3, 2016
1,766
960
Wana jamvi salaam!

Naomba niongee kwa uchungu sana juu ya hii decodor tajwa hapo juu,na nimeona niwe muwazi kwao ila nina imani yakuwa haitowapunguzia chochote endapo nitajitoa kutumia Zuku.

Hii decodor imekuwa ya hovyo sana na hapa lenho langu siyo kuwaharibia ama kuwasema vibaya kwenye biashara yao la hasha!huu ni muendelezo wa kuwanusuru wote wanaotumia hii Zuku.

Hawa jamaa kwanza wao local chanels zote lazima ulipie kinyume na hapo hupati habari na chanel utakayoambulia ni ile ya matangazo tu ya Zuku.

Baadhi ya local tv hawa watu kwenye kisimbusi chao hakuna kabisa kama Tv 1,Azam tv kwa haya ambayo tunayoyapata toka kwa hawa jamaa binafsi sitoweza kuendelea kuwa nao kamwe.

Kali kuliko usiombe mvua inyeshe harafu unatumia hii decodor utajuta hiyo scruch!hutoweza kuona chochote kwa kiwango kikubwa sana!

USHAURI

Kwa wote wanataka kuingia kwenye ulimwengu huu wa kidigitali msithubutu kuingia kwa hawa Wakenya ni ujanja ujanja umewajaa na huduma mbovu

Nawasilisha.
 
Ndugu yangu tena afadhali mara elfu moja hao Zuku kuliko wengine wote kidogo Dstv sawa lakini nao wana matatizo yao mengi tuu
-ishu ya ku scratch wakati mvua ikinyesha hii ni kawaida kwa visimbuzi vyote
-ishu ya local channels kwa free labda hilo walitazame upya
 
Mmh mi naona bora Dstv Niko eneo full mvua na maradi but wako vizur tu.
 
Ndugu yangu tena afadhali mara elfu moja hao Zuku kuliko wengine wote kidogo Dstv sawa lakini nao wana matatizo yao mengi tuu
-ishu ya ku scratch wakati mvua ikinyesha hii ni kawaida kwa visimbuzi vyote
-ishu ya local channels kwa free labda hilo walitazame upya
Mkuu unanishauri nitumie kipi maana hawa Zuku hapana wamenichosha sitaki hata kuwasikia nimeshashusha lile dish lao.
 
Kwenye mvua hapo ni majanga.... mimi mvua ikianza kunyesha tu ugomvi na mwanangu unaanza..full kulia na anaanza kunipiga eti nimemzimia katuni
Pole sana mkuu mimi wamenichosha mpaka mwanangu mdogo huwa ananiuliza kama decodor hii nimepewa bure!
 
Ndugu yangu tena afadhali mara elfu moja hao Zuku kuliko wengine wote kidogo Dstv sawa lakini nao wana matatizo yao mengi tuu
-ishu ya ku scratch wakati mvua ikinyesha hii ni kawaida kwa visimbuzi vyote
-ishu ya local channels kwa free labda hilo walitazame upya

KWA zuku , bado safi, channels ziko nyingi za kuelemisha, taarifa za habari ki ingilishi usiseme, radio ndiyo kabisa kwa walokole utaFURAHIA MNO, tatizo ni local free channels na kama kawaida yetu tunapenda mtelemko saana hata pasipo sababu. toa TSH 25000.00 harafu uone kama utahama. NEVER. STAR TIMES DECODER YANGU IKO UVUNGUNI MWAKA NA SIKU KADHAA.
 
Back
Top Bottom