Zuio la Makonda kutowasaidia omba omba litawaumiza sana

maramia

JF-Expert Member
Jul 17, 2015
2,030
1,345
Tangazo la mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kupiga marufuku kuwasaidia omba omba walioko jijini kwake ni zuri lakini lenye walakini mkubwa.

Lina walakini kwa sababu katika jiji hili kuna ombaomba maskini ambao kulingana na ulemavu wa maungo yake hawana namna yoyote ya kujipatia kipato ama mlo wao bila kuomba na kusaidiwa.

Miaka michache iliyopita niliwahi kumwona ombaomba mmoja jijini Dsm ambaye hana miguu wala viganja vya mikono (nadhani kutokana na ukoma) ambaye alinisimlia kwamba ndugu na jamaa zake walimakia kutoka Shinyanga wakamtelekeza jijini na tangu wakati huo hawataki hata kulisikia jina lake achana na habari ya kumwona.

Sijui Makonda amejiandaaje kukabiliana na changamoto za aina hii na atawasaidiaje ombaomba wa jinsi hii ambao kuomba kwao si kwa kujitakia bali kumechangiwa na maumbile yao au maradhi.

Makonda haoni kama ni bora kwanza angewaandalia maskini hawa mahala pa kukaa na jinsi serikali ya mkoa wake inavyoweza kuwasaidia?
 
Km nimemuelewa vzr Mh Makonda kasema hao wote waende vituo vya kulelea yatima ili wasaidiwe kule.
 
Aisee wanazingua na sio wote të wasio na uwezo wa kufanya kazi.. Wagogo ni wavivu hawapendi kujishughulisha... Pale watoto wanazurura kuomba hawaendi shule then wanazidi kuzalisha ombaomba


Warudishwe Dodoma mbona makabila mengine hawapo mitaani wagogo tu watokeeeeeeeee
 
Aisee wanazingua na sio wote të wasio na uwezo wa kufanya kazi.. Wagogo ni wavivu hawapendi kujishughulisha... Pale watoto wanazurura kuomba hawaendi shule then wanazidi kuzalisha ombaomba


Warudishwe Dodoma mbona makabila mengine hawapo mitaani wagogo tu watokeeeeeeeee
Tuombe radhi wagogo, sio wote wanao ombaomba ni wagogo
 
Back
Top Bottom