Si kila omba omba anao umaskini wa fedha

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2023
4,695
6,398
Kipindi Luteni Mstaafu, Yusufu Makamba akiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, kulikuwa na omba omba maarufu, nafikiri aliitwa Matonya, ambaye kila aliporudishwa kwao Dodoma, baada ya muda, alirudi tena jijini.

Inasemekana, hakuwa maskini kama ambavyo ingeweza kudhaniwa. Alikuwa anamiliki mali kiasi fulani, yakiwemo magari. Sijui kama hayo ni kweli.

Nilisikia pia kuhusu bibi mmoja mlemavu katika mkoa fulani ambaye pamoja na kuwa alitegemea kupata hela kwa njia ya kuomba omba, kuna wakati alikuwa wakiwasidia hela watoto wake waliokuwa watu wazima wenye afya njema.

Mwaka huu nikiwa kwenye duka moja mjini majira ya Jioni, kipofu
mmoja aliyekuwa akiongozwa na mvulana mdogo, alipita dukani hapo kubadilisha hela ya shilingi (silver) aliyokuwa nayo ili aweze kupewa hela ya noti. Inaelekea alishazoea kwenda kubadilishia fedha zake hapo. Alibadilishiwa kwa kupewa za noti, nafikiri ,ilikuwa shilingi elfu ishirini na moja.

Nilipomwona siku hiyo huyo kipofu akibadilisha hela ambayo nilihisi ilitokana na jitihada zake za kuomba omba, nilikumbuka nilichokuwa nikisikia kuhusu omba omba, kwamba baadhi wanamiliki mali lakini hawataki kuacha kazi ya kuombaomba. Kama hiyo elfu ishirini na moja ilikuwa mapato ya siku moja, akipata makusanyo ya kiwango hicho kwa siku thelathini mfululizo, anaweza akawa "tajiri" kumzidi dereva wa dala dala.

Sisemi kuwa omba omba wasiendelee kupewa misaada hasa ya kifedha, ila nafikiri kunahitajika msaada zaidi wa kuwabdilisha fikra ili waweze kufikia hatua ya kutumia kidogo walicho nacho kujiingizia vipato hivyo kuondokana na adha ya kuendelea kuombaomba.

Kama unapenda kuwasaidia omba omba, ni jambo jema. Endelea kufanya hivyo, lakini angalia kama unaweza kumsaidia fikra zitakazomtoa katika gereza la kuombaomba.

Omba omba wanaweza wakawa na uhitaji wa fedha, lakini uhitaji wa kubadilishwa fikra ni mkubwa zaidi kuliko uhitaji wa fedha walio nao. Wanahitaji kusaidiwa kifikra.
 
Back
Top Bottom