Naomba nilete utapeli unaofanywa ama uliokwishafanywa na hawa wanajiita GOLDEN BISTRO HOTEL ya arusha ...kazi za nafas kibao zilitangazwa zoomtanzania na watu waka apply, lakini katika majibu ya kuitwa usaili wakasema kwamba ili uconfirm ushiriki wako utume shilingi elfu 10 ...
Mimi mmoja wao nliyeomba kazi lakin sikutuma hio elfu 10, lakin cha ajabu email iliyotumika kwamba ndo tutume maombi kule ndio ikatuandikia katika email zetu na zaidi ya watu 500 kwamba eti ni utapeli ...badae mmoja wa walituma hela akaja kusema kwamba eti mhusika kaapiga simu kasema asamehewe kwamba kweli hakuna hio hoteli arusha na hizo kazi hamna kwamba alikua anatafuta ada ya chuo.
Watu wengi wametoa hio elfu 10 ...