Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 4,783
- 14,975
Upande wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) umeeleza kuwa mafao yanayotolewa na mfuko huo kwa sasa ni yake ambayo yalifanyiwa maboresho ya Kisheria mwezi Oktoba 2022.
Ambapo fao la kutokuwa na ajira wanufaika wanapatiwa hata kama wamefanya kazi chini ya miezi 18 na kwamba Sheria hiyo inatumika kwa Watanzania wote bila kujali ni Mkazi wa Zanzibar au Tanzania Bara.
Pia soma ~ Wageni tunaomaliza mikataba Zanzibar chini ya Miezi 18 hatupewi Mafao ya Mfuko wa Kijamii, hii Sheria ibadilishwe
Taarifa ya ZSSF imeeleza kuwa fao hilo ni sehemu ya mafao kama yalivyo maengine yakiwemo Fao la Kupoteza Ajira, ambalo Mwanachama aliyepoteza kazi atalipwa baada ya kukaa nje ya ajira kwa miezi sita.
Kiwango cha Malipo, aliyechangia miezi 18 hadi 36 hulipwa michango yake yote pamoja na asilimia 1 ya ziada, aliyechangia miezi 36 hadi 56 hulipwa michango yake yote pamoja na asilimia 20 ya mshahara wake wa mwisho.
Fao la Ulemavu:
Mwanachama anayepata ulemavu akiwa kazini ana haki ya kulipwa fidia kulingana na asilimia ya kiungo kilichoathirika.
Ikiwa amechangia kwa angalau miezi 156, atalipwa mkono wa kwaheri (lumsum) na pensheni ya kila mwezi maisha yake yote.
Fao la Uzazi:
Mwanachama mwanamke anapojifungua anastahili kulipwa fao hili kulingana na taratibu za mfuko.
Fao la Uzee (Kustaafu):
Hutolewa kwa mwanachama aliyetimiza umri wa kustaafu (kuanzia miaka 55 hadi 60), Mwanachama hupata mkono wa kwaheri na pensheni ya kila mwezi maisha yake yote.
ZSSF inashauri wanachama waliofikisha miaka 50 kusubiri hadi miaka 55 ili wafaidike na pensheni ya kila mwezi.
Fao la Mafunzo:
Mwanachama anapokuwa kwenye mafunzo ya kikazi anaweza kulipwa nauli na gharama nyingine za mafunzo.
Taarifa imeeleza kuwa ZSSF inatambua wanachama kutoka pande zote za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Bara na Visiwani).
Wageni (Foreigners): Wageni wanaofanya kazi Zanzibar wanaweza kuchukua michango yao yote mara wanapomaliza muda wao wa kazi na kuondoka nchini.
Ili kuendelea kupata pensheni ya kila mwezi, mstaafu lazima afanye uhakiki kila baada ya miezi sita.