DR. MWAKABANJE
JF-Expert Member
- Nov 7, 2012
- 1,976
- 3,122
Ndugu wana Jf, ni kweli tumekuwa tukilalamika sana kuhusu tatizo la ajira hapa nchini, kwa hivyo basi tumekuwatukijitahidi sana kutafuta kazi, au taarifa juu ya wapi tunaweza kupata kazi kupitia njia mbalimbali za mawasiliano zikiwemo social networks kama vile Zoom Tanzania.Kutokana na shida/tatizo hili wajaja miongoni mwetu katika jamii wamekuwa wakitumia mbinu mbalimbali ili kunufaika kwa namna moja au nyingine kupitia wasaka ajira.
Kilichonisukuma leo kuandika jambo hili ni hawa matapeli wanaotuma ujumbe mfupi wa simu pindi unapoomba kazi wakikutaka uwatumie chochote ili wakusaidie. binafsi hadi sasa nimetumiwa jumbe tatu ndani ya miezi miwili mfululizo, moja kutoka kwa mtu aliyejitambulisha kama Rachael Mwakapalila, pamoja na mambo mengine yote alinitaka nitume sh. 10,000 ili anisaidie nipate maswali ya interview kwa makubaliano kwamba nitamlipa sh. 300,000/= kutoka kwenye mshahara wangu wa kwanza kama malipo ya kunisaidia kupata kazi, ila sikufanya hivyo.Ndani ya mwezi huu nimepata massage kutoka kwa mtu anayejitambulisha kwa jina la Shafii, mara ya kwanza alinitaka nimtumia sh.30,000/= leo anataka nimtumie sh. 35,000/= kumbuka hizi ni kazi mbili tofauti kwa lengo lilelile kama la Rachael, kama ningewalipa hawa wote ningetumia sh. 75,000/=.
Massages zote nilizozipata, nafasi hizo za kazi nimeomba kupitia ZOOM TANZANIA, sasa swali langu kwa ZOOM ni nani anafanya upuuzi huu, ni kwenye kampuni/shirika niliyoomba kazi au zoom imeingiliwa na wajanja wanaochukua taarifa zetu?Ujumbe wangu kwa hawa matapeli, wamekuwa wakiandika kuwa wamependa CV yangu, jibu langu ni kuwa kama umeipenda ibusu basi inatosha au kwenye huo mchakato niweke kwa kuwa umependa cv yangu, huwezi ukapenda cv yangu halafu ukataka nikulipe eti kwa sababu cv umeipenda!
Namba anayotumia shafii ni 0652795853 na 0768978077