Zoezi la Vitambulisho vya Kupigia Kura Pemba Lapamba Moto | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zoezi la Vitambulisho vya Kupigia Kura Pemba Lapamba Moto

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Sep 5, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Sep 5, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Akina mama wa Pemba wakionyesha vitambulisho vyao Friday, September 04, 2009 4:57 AM
  Zoezi la uandikishaji wa vitambulisho vya kupigia kura kwa wakazi Chake Chake mkoani Pemba linazidi kupamba moto. Zoezi la uandikishaji wa vitambulisho vya kupigia kura kwa wakazi Chake Chake mkoani Pemba linazidi kupamba moto kutokana na vijana wenye rika ya kupiga kura na vikongwe kujitokeza kwa wingi katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Chake chake mkoani Pemba.

  Afisa usajili wa vitambulisho vya kupigia kura katika wilaya hiyo Ali Mohaned Chande alisema kuwa zoezi hilo, linaendelea vizuri pamoja na kwamba kuna matatizo ya hapa na pale kwa baadhi ya wananchi kulichukulia swala hilo kama la kisiasa zaidi.

  Chande alisema fomu za kujiandikisha zinatolewa kwa mujibu wa kifungu cha sheria namba 7 kifungu cha kwanza kinachosema ni wajibu wa kila raia mzawa mwenye umri wa kuanzia miaka kumi na nane anao wajibu wa kupatiwa kitambulisho hicho.

  Zoezi la uandikishaji wa vitambulisho lilianzishwa mwaka 2005 likivihusisha vyama vyote vya upinzani vilivyopo katika visiwa vyote vinavyounda Zanzibar ambavyo ni Unguja na Pemba.

  Afisa usajili wa vitambulisho Ali Mohamed alisema changamoto wanayokabiliana nayo ni baadhi ya vyama kulifanya jambao hilo kuwa la kisiasa zaidi na hivyo kuwakwamisha watu wengi.

  Watu wengi wamekuwa wakijiandikisha lakini hawafiki kuchukua vitambulisho vyao.

  Mpaka sasa zaidi ya vitambulisho 1,720 tayari vimeshakamilika katika Wilaya ya Chake chake lakini wenye navyo hawajakwenda kuvichukua.

  Hali hii inasemeka kuwa inatokana na kwamba waliojiandikisha si wakazi wa eneo husia kwani baada ya kujiandikisha wameondoka kurudi makwao jambao ambalo linaleta usumbufu zaidi.

  Zoezi hilo la uandikishaji wa vitambulisho vya kupigia kura lilianzia vijijini kabisa na sasa tayari zoezi hilo limehamia mijini.

  Kwa upande wake Sheha wa shihiya ya Madugu (mwenyekiti wa serikali za mitaa) Sulemani Abrahimu, alisema zoezi hilo linakwenda vizuri kwa kuwa tayari serikali imeshatoa agizo kuwa wenye sifa tu ndio waandikishwe kama mtu hana sifa zinazohitajika hawezi kuandikishwa .
  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=2994186&&Cat=1
   
Loading...