Zoa zoa ya bure mwaka mpya

Ferruccio Lamborghini

JF-Expert Member
Apr 15, 2020
1,664
2,517
BAADHI ya majina ya mastaa wakubwa kabisa kwenye soka yatakubali kujiunga na klabu yoyote wanayotaka kuanzia keshokutwa Jumamosi na hakuna kitu kitafanywa na klabu zao za sasa kuzuia jambo hilo.

Kylian Mbappe, Paul Pogba na Gareth Bale ni baadhi ya masupastaa wa soka la dunia kwenye orodha hii, ambao wanaingia kwenye miezi sita ya mwisho ya mikataba yao, hivyo kuanzia Januari Mosi, watakuwa na ruhusu ya kusaini mikataba ya awali na klabu nyingine kwa ajili ya kujiunga nazo bure kabisa.

Hata hivyo, hawataweza kujiunga na klabu hizo mpya watakazosaini bure hadi hapo msimu utakapofika tamati.

Kitu kinachovutia kuna wachezaji 539 kutoka kwenye Ligi Kuu tano bora za Ulaya wanaingia kwenye miezi sita ya mwisho ya mikataba yao, hiyo ina maana wanaweza kukubaliana na klabu yoyote kwa ajili ya kusaini mikataba ya awali siku ya kwanza tu ya Mwaka Mpya na kusubiri msimu umalizike wakajiunge nao.

Wachezaji kuhama bure si kitu kipya kwenye soka, lakini kwa miaka michache iliyopita imeshuhudiwa mastaa wengi wenye vipaji vya maana kabisa kwenye soka wakiachwa na timu zao hadi nyakati za mwisho kabisa bila ya kusaini mikataba mipya na hivyo kuachana na timu hizo kama wachezaji huru msimu unapofika tamati.

Mambo hayo yamekuwa yakisababisha presha kubwa kwa klabu katika kulazimisha wachezaji hao walau wasaini mikataba mipya ili kuwafanya kuwa na uhakika wa kupata chochote kitu wakati wachezaji hao watakapoondoka.

Hawa hapa mastaa ambao Mwaka Mpya ukiingia tu, unaweza kusainisha mikataba ya awali, ukawanasa bure.

Makipa

Sam Johnstone (West Brom)

Kipa huyo namba tatu wa England kuna timu kibao za Ligi Kuu England zimekuwa zikihitaji saini yake na mkataba wake unafika tamati huko Hawthorns. Tottenham na West Ham ni kati ya timu zinazomtaka.

Hugo Lloris (Tottenham)

Kipa huyo veterani wa Ufaransa atafikisha mwaka wake wa 10 kwenye kikosi cha Tottenham Hotspur itakapofika 2022, lakini si mchezaji mwenyewe wala klabu iliyoamua kuhusu kubaki. Lloris anawindwa na klabu kibao za Ulaya.

Mabeki

Andreas Christensen (Chelsea)

Mshindi huo wa medali ya ubingwa ya Ligi ya Mabingwa Ulaya amecheza kwa kiwango bora kabisa miezi 18 iliyopita, lakini hakuna dili lolote jipya lililowekwa mezani. Pande zote mbili zipo kimya huku Christense akifikiria kubadili wakala.

Antonio Rudiger (Chelsea)

Amekuwa staa matata kabisa huko Stamford Bridge, lakini hajasaini dili jipya Chelsea na inaelezwa kuna ofa nene mezani kutoka Real Madrid huku nyingine ikitokea Bayern Munich. Rudiger atakuwa huru kusaini mkataba wa awali Januari 1.

Thiago Silva (Chelsea)

Veterani huyo ana miaka 37 kwa sasa, lakini amekuwa akionyesha kiwango bora kabisa uwanjani kila anapocheza. Anaonekana kutuliza daruga zake vyema huko Stamford Bridge, lakini hajasaini dili jipya na hapo anawavuruga mashabiki.

James Tarkowski (Burnley)

Newcastle United wanapambana wasishuke daraja, hivyo wanahitaji huduma ya James Tarkowski kutoka Burnley. Wanaweza kufanya haraka kupata saini yake kwa Pauni 10 milioni kuliko kusubiri bure mwisho wa msimu wakashuka.

Cesar Azpilicueta (Chelsea)

Panga pangua amekuwa mchezaji muhimu chini ya Thomas Tuchel, lakini kuibuka kwa Reece James kunawafanya mabosi wa Chelsea kuchelewa kumsainisha dili jipya beki huyo. Azpilicueta ni miongoni mwa mastaa wanaomaliza mikataba yao.

Viungo, Paul Pogba (Man United)

Manchester United wanajiandaa kupata hasara kwa sababu walitoa Pauni 89 milioni kupata saini ya Paul Pogba mwaka 2016, lakini sasa kiungo huyo anajiandaa kuondoka bure kabisa huku PSG, Real Madrid na Juventus zikihitaji saini yake.

Boubacar Kamara (Marseille)

Kiungo mkabaji kijana kabisa ambaye kiwango chake bora kimefanya klabu kadhaa za Ulaya ikiwamo Man United na Chelsea kumtolea macho. Kitu kizuri ni kwamba Januari Mosi anaweza kusaini mkataba awali akabebwa bure baadaye.

Axel Witsel (Dortmund)

Akielekea kwenye uveterani, Witsel, 32, bado ana uwezo wa kumfanya mambo makubwa ndani ya uwanja. Bado anaweza kucheza kwa miaka mitatu zaidi huku huduma yake ikipatikana bure hakuna hasara kwenye hilo akinaswa na timu yoyote.

Franck Kessie (AC Milan)

Staa huyo wa Ivory Coast amekuwa kwenye kiwango bora na hivi karibu aliwaambia AC Milan anataka kuondoka. Jambo hilo linakuja wakati ambao mkataba wake umebakiza miezi sita huku Tottenham wanapambana kunasa huduma yake bure.

Luka Modric (Real Madrid)

Kiwango bado kipo kwenye ubora uleule licha ya kwamba hatakuwa kila sehemu ya uwanja ukinasa huduma yake kwa sasa. Mwanasoka bora dunia wa zamani bado kuna kitu anaweza kukifanya huku saini yake ikipatikana bure kabisa.

Gareth Bale (Real Madrid)

Mmoja wa wachezaji bora kabisa duniani, lakini miaka michache ya karibuni mambo yake yametibuliwa na majeraha. Timu zilishindwa kumchukua kisa mshahara wake wa Pauni 650,000 kwa wiki, lakini sasa mwisho wa msimu anapatikana bure.

Washambuliaji Kylian Mbappe (PSG)

Moja ya mastaa wakubwa kabisa kwenye soka la dunia. Aligomea ofa ya mkataba wa miaka sita huko PSG huku moyo wake ukitaka kwenda kukipiga Real Madrid. Bila ya shaka Januari Mosi atasaini mkataba wa awali na Los Blancos.

Paulo Dybala (Juventus)

Aliwahi kuwamo kwenye rada za Man United na Tottenham huko nyuma na sasa siku zake huko Juventus zinahesabika. Paulo Dybala atakuwa huru kusaini mkataba wa awali na klabu yoyote ya Ulaya Januari Mosi ili kujiunga bure baadaye.

Ousmane Dembele (Barcelona)

Alihusishwa na kila klabu ya maana huko Ulaya. Staa huyo Mfaransa ni moja ya wachezaji wenye vipaji vikubwa, lakini amekuwa na tatizo la kuwa majeruhi wa mara kwa mara. Barca ilimsajili kwa Pauni 135 milioni, lakini sasa ataondoka bure.

Lorenzo Insigne (Napoli)

Moja ya mashujaa wa Italia kwenye Euro 2020. Amekuwa na ofa kutoka sehemu mbalimbali za Ulaya pamoja na Marekani. Napoli imeshindwa kumshawishi asaini mkataba mpya, hivyo atakuwa mchezaji huru kuondoka bure Naples.

Andrea Belotti (Torino)

Akiwa straika aliyetuliza akili yake ndani ya uwanja, Belotti, 28 yupo kwenye kilele cha soka lake. Torino wanaweza kuhitaji kumuuza walau kupata pesa, lakini klabu zinaweza kufanya ujanja wa kumsainisha dili la awali ili mchukue bure msimu ukiisha.

Alexandre Lacazette (Arsenal)

Mambo yanaweza kubadilika huko Emirates. Wakati msimu unaanza, ilionekana huu ni msimu wa mwisho kwake kuichezea Arsenal, lakini sasa kila kitu kimebadilika na huenda Lacazette akabaki. Hata hivyo ni miongoni mwa mastaa watakaopatikana bure.

Jesse Lingard (Man United)

Alikuwa moto msimu uliopita alipocheza kwa mkopo huko West Ham akarudi Man United na kusahaulika tena. Sasa Lingard anaingia miezi yake sita ya mwisho huko Old Trafford na ni miongoni mwa wachezaji watakaopatikana bure kabisa.

Divock Origi (Liverpool)

Hata Jurgen Klopp mwenyewe haamini kama straika huyo Mbelgiji amebaki Anfield kwa muda mrefu. Kipaji cha juu kabisa, lakini Origi anahitaji timu itakayompa nafasi ya kucheza. Liverpool wanataka kumuuza kabla ya kuondoka bure.

©MwanaSpoti
 
Thiago Silva mtoe hapo Coz tayari ame extend mkataba wake pale darajani
 
Isigne kashatua Ligi Kuu ya Marekani
 
Back
Top Bottom