Upupu mtupu!!!. Mkuu naona unania ya kueneza chuki zisizo na maana. Kwanza taarifa yako imejaa maneno kama 'Nyerere anasemekana' na mengineyo kama hili, kwamba huna uhakika na unachokiandika. Pili TANU ilianzishwa mwaka 1957, hivyo kabla ya hapo Mwl. hajawahi kuwa mwenyekiti wa TANU. Hata huo uhuru wa Zanzibar unaouzungumzia historia inatuambia kwamba hadi tarehe 12/1/1964 Zanzibar ilikuwa inapeperusha bendera nyekundu ya Sultan Jamshid mhamiaji kutoka Oman aliyemrithi marehemu baba yake Sultan Seyyid Abdulla bin Khalifa. Hivyo hata vyama vya Hizbu na ZPPP viliposhinda uchaguzi wa Julai 1963 Zanzibar ilikuwa bado chini ya Sultan. Kama huijui historia ya Zanzibar bora ukae kimya usituletee upupu humu kwa great thinkers.