ZNZ ikitafakari juu ya ajenda ya utaifa wake, Ajenda 5 ilizotunga Tanganyika kuimaliza Zanzibar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

ZNZ ikitafakari juu ya ajenda ya utaifa wake, Ajenda 5 ilizotunga Tanganyika kuimaliza Zanzibar

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Kizibao, Aug 29, 2011.

 1. K

  Kizibao JF-Expert Member

  #1
  Aug 29, 2011
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 742
  Likes Received: 349
  Trophy Points: 80
  Na Laila Abdulla,

  Katika kipindi hiki cha mpito kuelekea katiba mpya,wazanzibari wanajikuta katika JAHAZI ya safari ya mwisho kutoka Dar-es-salaam kurudi Unguj.Wakiikosa safari hii, basi ,wataula na chua kwa uvivu wa kuchagua.Tanzania-bara au Tanganyika, katika kipindi hiki cha mpito hadi sherehe za miaka 50 za Muungano mwaka 2014 ,wanajiandaa kukamilisha ajenda yao ya mwisho -ajenda ya 5 itakayo kamilisha KUIMEZA ZANZIBAR na kuifanya MKOA WA PWANI wa Tanzania. Mkakati huu ulitungwa lini na ipi ilikua ajenda ya kwanza ?
  AJENDA I:
  Ni pale Mwalimu Julius Nyerere ,kama Mwenyekiti wa TANU kati ya miaka ya 1956-7,alipofunga safari hadi Zanzibar akibeba ujumbe wa kuunganisha iliokua African Association (Jumuiya ya Waafrika) na Shirazi Association (Jumuiya ya Washirazi) .
  Mwalimu na chama chake cha TANU, walitambua kwamba ,kwa idadi ndogo ya Wazanzibara wakati ule kule Zanzibar ,kamwe wasigeweza kushika mpini na kuongoza Zanzibar ili kutimiza ajenda iliopangwa. Mwalimu anasemekana aliziambia Jumuiya hizo mbili ” kama hamtaungana,Waarabu watatawala hapa daima.”.Kwa njia hii,Mwalimu alisimamia kuundwa kwa chama cha AFRO-SHIRAZI PARTY. Sheikh Karume akiwa Rais na Sheikh Thabit Kombo katibu wake.
  AJENDA 2:
  Kwa kuunda Ushirikiano kati ya TANU na Afro-Shirazi Party,AJENDA ya pili , ni Kuunda “MUNGANO wa Tanganyika na Zanzibar” baada ya Uhuru ambao Tanganyika ikitumai, ungeangukia mikononi mwa Afro-Shirazi Party.
  Mambo yalipokwenda kombo na uhuru Desemba 10,1963, ulipoingia mikononi mwa wapinzani wao ZNP/ZPPP, shabaha hii ilibidi ifikiwe kupitia MAPINDUZI ya Januari 12, 1964.Historia ya mapinduzi na wapi yalipikwa na nani walishiriki, imeandikwa kwa mapana na marefu na Dr.Harith Ghasani katika kitabu chake “KWAHERI UKOLONI,KWAHERI UHURU”.
  Mara tu baada ya mapinduzi yalioun’goa utawala wa Sultani, Mwalimu alianza kupiga hodi mlangoni mwa Sheikh Karume kuulizia juu ya Muungano ? Sheikh Karume alibisha kwanza kuitikia hodi na akisema “Sisi ndio kwanza tumekuwa Jamhuri changa baada ya kujikomboa”. “Ni mapema kuzungumzia Muungano”.
  April, 1964 shinikizo la Mwalimu lilizidi ; na akiungwamkono na dola kuu za Magharibi zilizoiona Zanzibar ni kitisho (Communist Menance) Afrika Mashariki na ( Mecca ya kiislamu ) , Mwalimu alitimiza Ajenda ya pili.
  Ushawishi wa kikoministi Mwalimu aliudhibiti kwa kuwadhibiti wanamapinduzi wa Zanzibar aliowaleta Tanzania-Bara : Abdulrahman Babu aliekua waziri wa nje na biashara alimfanya tu waziri wa mipango ya uchumi chini yake . Katibu wake wa Umma party au (Chicom ) neno waliotumia Marekani kuwaita wafuasi wa Umma party-yaani Chinese communists-Dr.Salim ,akapelekwa nje Balozi na baadae Umoja wa Mataifa. Col.Ali Mahfoudh,alihamihiwa bara baadae Msumbiji.
  Kuiua Zanzibar kama “Mecca ya Uislamu”, Mwalimu alitumia kawa la “KUONDOSHA UWARABU NA USULTANI”. Kwani, angelitumia KUUPIGA VITA UISLAMU, washirika wake Afro-Shirazi wangengamua. Vedeo za Ustaadh Illunga za hivi karibuni zinafunua kawa.
  AJENDA 3:
  KUIDHOFISHA ZANZIBAR KIELIMU NA KIUCHUMI NA KUMUACHIA MZEE KARUME WAKWEZI NA WAKULIMA TU: Aliwachukua wasomi wengi wa Zanzibar na kuwafungulia mlango Tanzania-bara.Wizara zisizokuwa za muungano kama Habari na Utalii wakapewa Wazanzibari na wakazipokea bila kutanabahi mtego waliowekewa.Sheikh Idris Abdul-wakil akawa waziri wa habari .Sheikh Hasnu Makame, waziri wa Utlii.
  Zote hizo mbili si wizara za Muungano. Wazanzibari wengine waliokimbia utawala wa vitisho vya kimapinduzi,walipokewa kwa raha mustarehe Dar-es-salaam.Wapemba wakajitanua kibiashara na kuisahau Pemba. Kila mzanzibari aliambiwa “Tanzania-bara ni njema ,atakae aje.”
  Muda haukupita,Mwalimu akadai “Nipe-ni kupe”.Watanganyika nao wafunguliwe mlango kuingia Zanzibar bila vizuwizi na Zanzibar, mwishoe , ikaitikiabila ya kutanabahi kwamba, ule ulikua mtego wa Mwalimu. Kwani, Wazanzibari milioni 1.2 wanaweza wote leo kuhamia Bara bila kuathiri mila,utamaduni au uchumi wake. Lakini, wakiingia Wamasai 100.000 tu Zanzibar na Pemba, baada ya mwongo 1 tu,mila na utamduni na hata dini itaathirika.
  Hali ya Uchumi wa Zanzibar na Maendeleo yake kwa jumla, ni mbaya.Zanzibar imerudi nyuma miaka 47. Nchi ya kwanza iliokuwa na umeme Afrika Mashariki, leo kiza kimetanda. Hadi miezi 3 ilikosa umeme mwaka jana.Maji yamekuwa haba. Ule mkakati :” Ili kuwa na Tanzania imara, lazima uwe na Zanzibar dhaifu,ungali unfanya kazi. Ni hapa ndipo kipo kielezo :KWANINI ZANZIBAR HAIWACHWI KUNEEMEKA NA MAFUTA AU NA GESI YAKE.Kwani ,kuiachia, kutachafua Ajenda ya 3 ya kuiua kiuchumi na kitaalamu ilioanzia kunyakuliwa akiba yake ya 11% ya mtaji wake kutoka bodi ya sarafu ya iliokua Afrika Mashariki na kutiwa BOT.
  AJENDA 4:
  Wakati kisiwa kilichokua safu ya mbele kielimu na shina la dini ya kiislamu kusini mwa Afrika -Jangwa la sahara,leo kimerudi nyuma,chini ya Ajenda ya 4: Watoto wa Wazanzi-bara wamepelekwa bara na kwengineko kusoma katika vyuo vikuu na vyenginevyo na wanarudi sasa kushika hatamu za uongozi visiwani. Angalia mwenyewe sekta zote- serikalini, Jeshini,Radio na TV ,bandarini nikitaja sekta chache tu. Ni Wazanzibara hawa ndio mwishoe ,wakamilishe AJENDA ya 5:
  AJENDA 5:
  KUIMEZA KABISA ZANZIBAR:MFUMO NI SERA YA CCM:KUTOKA SERIKALI 2 KWENDA 1:
  Mwishoe,Zanzibar itaangukia kuwa MKOA WA PWANI pamoja na Tanga na Dar-es-salaam chini ya mfumo wa Shirikisho.
  Fununu ziliwahi kuchomoza kuhusu kitabu cha aliekuwa waziri-mkuu chini ya Mwalimu:Jaji Warioba kupendekeza mfumo huo.
  Fununu zinadai hizo ndizo AJENDA 5 wenzetu wameziandaa kutumaliza. Lakini kuna ule usemi “It takes two to tango”.Mpira sasa uko katika lango la viongozi wetu na hasa watoto wa Afro-Shirazi Party kuliokoa jahazi lisizame au kuliachia lizame kabisa.Kipindi hiki cha mpito hadi katiba mpya imtungwa na kupitishwa,ni kipindi cha kuamua HATIMA ya Zanzibar na utaifa wake.
  Ikiwa wazanzibari sasa hawakuamka ,hawataamka tena,kwan, kishada kitakua kimeshaenda ARIJOJO 2014 tutakapokuwa na katiba mpya tukiadhimisha miaka 50 ya Muungano au ya kumezwa. Wasia wangu leo ni huu: Hakuna tena Uafro-shirazi wala uHizbu.Hakuna U-ccm wala U-Cuf. Zanzibar ikitoweka; na tumeshaambiwa tangu na Waziri-mkuu Pinda na majuzi hata na FIFA kuwa “si nchi” ,historia ya miaka 2000 ya dola la ZENJ itakuja kutuhukumu . CCM-ZANZIBAR lakini, itabeba jukumu zaidi kwani, ndio ilioshika mpini tanmgu 1964.
   
 2. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #2
  Aug 29, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Tanganyika ingepata faida gani kwa kuizoofisha Zanzibar? Mpaka leo sijui ni kipi cha maana ambacho tunaweza kusema "Tanzania bara" imepata kwa kuungana na Zanzibar zaidi ya migogoro na siasa za "muafaka". I respect and admire Nyerere sana ila katika makosa makubwa ya uongozi wake ni huu muungano.
   
 3. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #3
  Aug 29, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Heshima kwako MwanaFalsafa1.

  Mkuu Nyerere aliona mbali sana hakika kama si muungano Zanzibar wangeshachinjana siku nyingi Dar badala ya kupokea wachuuzi toka Pemba tungekuwa tunapokea wakimbizi.

  Tanzania Bara imesaidia sana Zanzibar mufumo wa serekali tatu wanaolilia hakika hautafanikiwa kwasababu moja kubwa Zanzibar kamwe haitaweza kuchangia gharama za muungano.Tanzania Bara inajiongezea gharama za uendeshaji wa serekali ya shirikisho na serekali ya Tanganyika.Wapika kelele hawawezi kulipa gharama za umeme je wataweza kuchangia gharama za wizara ya ulinzi,wizara ya mambo ya ndani,wizara ya mambo ya nje,wizara ya ushirikiano Afrika mashariki na wizara ya fedha ??????????.
   
 4. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #4
  Aug 29, 2011
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,423
  Likes Received: 395
  Trophy Points: 180
  Kweli urojo ni mbaya!
   
 5. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #5
  Aug 29, 2011
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,423
  Likes Received: 395
  Trophy Points: 180
  Hawa jamaa bado hawaamini kwamba hiyo ni sehemu ya nchi tu wala sio nchi! Hawaelewi kwamba kuwa na bendera, wimbo wako na makorokoro mengine haimaanishi wewe ni nchi...ni kama tu mtu unjiimbia kawimbo kako home, hakuna mtu atasema ati ni wimbo wa taifa wati wa taifa upo. Hawaoni tunavyowa-manipulate kupata rais amabye hataleta kokoro? angalia tumewapa mzee mpooole, Dr. Shein mwenye kushika maadili ya Muungano!
   
 6. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #6
  Aug 29, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Mkuu Mgongo,

  Mimi hili wazo la baadhi ya Zanzibar kufikiria kuwa Tanganyika (Bara) ndiyo ina faidika na huu muungano hata sijui wanautoa wapi. Hawawezi kutoa any facts and statistics kuonyesha kwamba kweli Zanzibar imeleta manufaa haya kwa Tanganyika zaidi ya kutoa mawazo yao binafsi. Saa nyingine wanachosha sana hawa watu.
   
 7. Mtumiabusara

  Mtumiabusara JF-Expert Member

  #7
  Aug 29, 2011
  Joined: Nov 18, 2009
  Messages: 473
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  kuna siku tutaandamana kwenda kudai serikali ya tanganyika bungeni. Hapo ndo wazenji wataelewa vizuri
   
 8. Kiumbemwanadamu

  Kiumbemwanadamu Member

  #8
  Aug 29, 2011
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kweli kama si kuichukua zanzibar leo tungekuwa na mgogoro mkubwa. Kuna taarifa kuwa km 10 kutoka pwani ya tanga, dar, bagamoyo lindi na mtwara lilikuwa eneo la sultani wa zanzibar. Hivyo kama si muungano ingekuwa mgogoro leo hii. Nyerere aliangalia mbele sana. Ni vema kuimeza zanzibar na kubadili mfumo kwenda serikali 1 yenye mfumo wa majimbo. Hivyo basi majimbo yatachagua viongozi kama ilivyo zanzibar, majimbo yataripoti serikali kuu ambayo itakuwa na mawazir wasiozidi wa5. Kazi ya serikali kuu ni kuwakilisha kimataifa na kubalance mapato kutoka majimbo tajiri kunyanyua majimbo maskini. Mwisho wa siku tutatambua kuwa hakuna mtanganyika wala mzanzibari au mzanzibara. Huu ni mchango wangu kuelekea katiba mpya. Kuna wataalamu wenye uwezo kuniweka sawa pale nimekosea.
   
 9. D

  Dopas JF-Expert Member

  #9
  Aug 29, 2011
  Joined: Aug 14, 2010
  Messages: 1,151
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Ati wasomi wa Zanzibar walipelekwa sijui wapi...? Kama walikuwa wasomi kweli kwanini hawakutumia usomi wao kuitetea nchi yao. Usomi wa kubebwabebewa? Mi naomba daima tuachane na huo muungano tuone watafanyeje?
  Ila tatizo wanaweza kuviuza visiwa vya pemba na unguja pamoja na wakazi wake kwa waarabu wa Oman, hapo itakuwa tatizo lingine, kuwa na jirani mwarabu....
   
 10. Jagermaster

  Jagermaster JF-Expert Member

  #10
  Aug 29, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 656
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Sasa kinachofuata Zanzibar chagueni kusuka au konyoa. Mabadiliko ya katiba yanayokuja sisi Tanganyika ni either serikali moja au kufuta muungano, nataoa wito kwa watanganyika tukamae na haya mawili wakati wa kutoa maoni.Hizo serikali tatu ni agenda ya Zanzibar kwani watakuwa wameuwa ndege wawili kwa jiwe moja, tutabaki tunawalisha kama mfugo asiyeuzwa milele na milele. Heri kabisa kuuwa hii ndoa kuliko hizo serikali tatu. Wito kwa Chadema mpaka sasa hatujaona msimamo wenu kwenye issue ya muungano, kila mtu analopoka yake hatujui msimamo wa chama kwa maswala nyeti kama haya. Kama msimamo wenu ni serikali tatu kama wabunge wenu wanavyoongea bungeni, mimi ni mmoja wa watu ninaona wapinga kwa hilo. Sijui kama mmefanya utafiti wa pros and cons wa mfumo huo. CCM wao ni serikali mbili na CUF ni tatu na hili liko wazi kabisa Chadema muko very latent kwenye hii issue, hatujui kama na nyie mnapima upepo kama wengine wanavyoondesha nchi kwa kupima upepo kwa sasa.
   
 11. A

  Albimany JF-Expert Member

  #11
  Aug 29, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 279
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Sisi wazanzibari tutakuja kuwasaidia kwa hilo pamoja na uchache wetu ila tutaungana nanyi ili Tanganyika irudi.
   
 12. A

  Albimany JF-Expert Member

  #12
  Aug 30, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 279
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Tatizo sio Tanganyika kufaidika kutoka Zanzibar bali ni zanzibar kunyonywa na Tanganyika ndio tatizo ambalo tunalipigia kelele wazanzibari.

  Kwa nchi kama zanzibar ilivyo ndogo kuanzia uchumi hadi ardhi haitatokezea kabisa kuinufaisha nchi kubwa kama Tanganyika, lakini uchumi mdogo wa zanzibar ukidhibitiwa na nchi kubwa kama Tanganyika itakuaje?

  Zanzibar ni visiwa ambavyo uchumi wake unategemea zaidi bandari na utalii na biashara ndogo ndogo,kwabahati mbaya mambo haya yamedhibitiwa na Tanganyika nitakupa mfano:

  1)Watalii wote wanaokuja Zanzibar wanalipa viza amma katika ubalozi wa Tanzania(tanganyika) au wanalipa airport Uhamiaji ambayo mambo haya ni ya ni yamuungano,hapa wazanzibari hupokea wageni bila ya kuingiza pesa za kigeni.

  2)Bandari:Bandari ya Zanzibar wanaokusanya ushuru ni TRA ambao huja na boti asubuhi na jioni wakarudi naboti ya Mwisho(jioni) vifurushi vya pesa wakifuatwa na ulinzi mkali pesa hizo ambazo ni za muungano hutumika kulipwa wafanyakazi wote watanganyika ambao hawako katika idara za muungano na zanzibar wakaambulia 4.5% mwisho wa mwezi.

  Hapa sijengi hoja kua Tanganyika ambayo inaidadi kubwa ya watu zaidi 40mill people kua inafaidi kwa vijipesa kidogo vinavyotokea zanzibar bali nakusudia kusema pesa zile kidogo kama zikiacha zanzibar yenye watu wachache si zaidi ya 1.2mill zingalisaidia sana,kuliko kugaiwa 4.5%.

  Wazanzibari wanaamini kua Tanganyika inachukua kodi Zanzibar wastani ya 16% vipi wanapata4.5%

  Nitakupa mfano tena ambao itakua rahisi kuiona athari hii:

  Mfano ukichukua watu wa Zanzibar nzima leo ukawapeleka Tanganyika basi Tanganyika haitajua kua kuna watu wameongezeka kama hawakusikia kupitia habari. Sasa chukua watu wa wilaya ya kinondoni tu si tanganyika yote uwapeleke zanzibar je zanzibar si itaathirika zaidi? na huenda hao wazanzibari wakafikiri wako kinondoni kutokana na athari yake.

  Mifano hiyo michache katika mengi ina weza kuwasaidia kujia kwanini wazanzibari Tunalalamika. nakaribisha suali likijitokeza.
   
 13. Jagermaster

  Jagermaster JF-Expert Member

  #13
  Aug 30, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 656
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  <br />
  <br />. Inashangaza sana unapoona watetezi wa Zanzibar mnapoandika Zanzibar inategemea bandari kwa uchumi wake!. Mimi huu naona sasa ni uvivu wa kufikiri wa Wazanzibar. Hivi toka lini kisiwa chenye population ndogo kama Zanzibar kikategemea bandari?. Kwa nini hamjiulizi je Comoro ama Mauritious wanategemea bandari?. Hiyo stock kubwa ya mizigo mtakayoingiza hapo Zanzibar, itakuwa kwa ajili ya population ipi?. Mnatarajia muingize bidhaa kwa ushuru mdogo hapo Zenj harafu msafirishe kwa maboti madogo kuja Tanganyika na Kenya harafu watu wa bara wawe majuha wakiwaangalia tu!!.Huo ni uvivu wa kufikiri. Kwa ushauri tu concetrate kwenye mambo mengine kama utalii, kilimo na uvuvi hilo la bandari mtagombana sana na bara.Tatizo mmesahau kuwa Bandari ya Zanzibar ilikuwa maarafu kwa sababu ya biashara ya toka bara, wakati huo bara ilikuwa na dola hafifu ya utawala wa machifu. Sultan wa Zanzibar alifanya biashara na machifu wa Tanganyika,hao machifu walikuwa hafifu na sasa kuna dola yenye nguvu zaidi ya Zanzibar. Hii inamaana wala ule utaratibu wa kuitumia Zanzibar kama kitovu cha biashara wala hauwezi kutokea tena.Kwa ushauri tu mnapokaa kwenye vijiwe vyenu mkidiscuss kuhusu muungano jiulizeni je Zanzibar inaweza kuwa kutovu cha biashara, na kuwa na bandari kubwa nje ya muungano?. Mkiona inawezekana ndio mje na hoja za kujitenga. Hilo la Selikari tatu msahau kabisaa
   
 14. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #14
  Aug 30, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Muungano uvunjike tu hawa wazenji wasitumiksi. Sasa najiuliza vitambulisho vya uraia vitakuwaje? Vya Tanganyika, Tanzania au Zanzitanganyika
   
 15. s

  sem2708 JF-Expert Member

  #15
  Aug 30, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 3,094
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  hili suala la wazenji kulalamikia muungano ni la KISAIKOLOJIA zaidi,ni sawa na wanawake walivyo na dhana ya kukandamizwa na wanaume but as a matter of facts wako wanaume wengi tu wanakandamizwa na wanawake ila hawaoni sababu ya kulalamika.
   
 16. enky

  enky Member

  #16
  Aug 30, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 99
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 25
  maoni yangu mie kama ziliungana nchi mbili basi ...serikali moja ndio mpango mzima...kwanza tutapunguza badget ya kuhudumia hizi serikali..pili kutakua hakuna mtu anaelalama kua ananyonywa maana saiz kila mtu anaona anaonewa na mwenzie..swala la msingi hapa ni kupata kiongozi mzuri tu basi...swala la muungano limeanza kua gumzo zaidi baada ya raisi wa muungano kutoka bara two tymz sasa naona jamaa wamepandwa na jazba..lakini enzi zile alivyokua anatoka kwao mambo mbona yalikua shwariiiiiiiiiiii
   
 17. S

  Simcaesor Senior Member

  #17
  Aug 30, 2011
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 112
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kuna wakati lazima ufike tukubali kwamba tanzania ni nchi kubwa kufikia maendeleo ya melenia kwa ukubwa itakuwa ni vigumu sana. tuache ubinafsi na maslahi binafsi, tuwaache wazanzibari hawa wakajenge nchi yao hata kimaono tu inaonekana watu hawa wakiwa na serikali yao wataendelea haraka zaidi kuliko sisi wa bara, tuwaache sisi ni mzigo kwao tena mkubwa sana.....
   
 18. H

  Hamuyu Senior Member

  #18
  Aug 30, 2011
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 119
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mkuu Wazanzibari hatuna jengine la kuchagua zaidi ya kujitenga na Tanganyika katika mchakato wa Katiba unaoendelea, suala la kupapatua nchi yetu ni jambo la kipaumbele cha kwanza kwa wakati huu na ujao na wala halina mjadaloa kwetu.
   
 19. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #19
  Aug 30, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  kama hamufaidiki kwanini mnaulinda muungano kwa gharama zozote zile. je kuna siri gani hapo?
   
 20. Bishop Hiluka

  Bishop Hiluka Verified User

  #20
  Aug 30, 2011
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 4,101
  Likes Received: 1,425
  Trophy Points: 280
  Wanaoulinda ni CCM wa Zanzibar ambao wanaamini kuwa
  nje ya muungano hawana chao, na wafanyabiashara wa Kipemba
  waliojenga majumba na kuwekeza hapa Dar na mikoa ming ya Bara...
   
Loading...