Wickama
Platinum Member
- Mar 8, 2009
- 1,577
- 1,365
Wanajamvi, Ziwa Victoria ndilo ziwa kubwa kuliko yote hapa barani Africa. Theluthi moja ya wakazi wa nchi za Kenya Uganda na Tanzania wanaishi kulizunguka na kuendesha maisha kutokana na ziwa hili. Lakini hivi kwa sasa ziwa hili linapigania uhai wake. Tatizo ni magugu maji. Japokuwa hivi karibuni kumeelezwa kuwa serikali zetu zinajitahidi kuyaangamiza (Hatua zatakiwa kuchukuliwa kulinusuru ziwa Victoria - china radio international) hali niliyoishuhudia kwenye pwani ya jiji la Kisumu inatia wasiwasi. Sijui katika nchi zingine hali iko vipi. Hapa nabandika picha nilizopiga nikiwa juu ya eneo husika ili tuchangie mawazo:
1. Haya magugu yapo ndani ya ziwa kama kilometer 3 toka jiji la Kisumu
2. Hapa ni jirani na kiwanja cha ndege cha Kisumu, mahali hapo kuna uoshaji wa magari kwa wingi na vibanda vingi vya kina mama lishe. Kwa sasa hakupitiki ila sehemu ndogo inayoonekana
3. Eneo unaloliona kijani lote limeathirika na magugu
My take: Hili ziwa linahitaji serious efforts kulinusuru vinginevyo maisha ya wakazi wanaolizunguka na hata ekolojia yake itaharibika sana. Wakati wa kuwa tegemezi na misaada ya nje ili kulinusru nadhani umepita, umefika wakati juhudi zetu wenyewe East Africa zilinusuru ziwa letu.
Where did we go wrong?

![25112012127[1].jpg 25112012127[1].jpg](https://www.jamiiforums.com/data/attachments/3228/3228771-52e2094612fc7c1374f9c1d535800530.jpg?hash=UuIJRhL8fB)
![25112012131[1].jpg 25112012131[1].jpg](https://www.jamiiforums.com/data/attachments/3228/3228773-0c27443b25f998e61f812352b060a7e2.jpg?hash=DCdEOyX5mO)
![25112012132[1].jpg 25112012132[1].jpg](https://www.jamiiforums.com/data/attachments/3228/3228774-f98f5b54cb65848d3849fdb6ad47149b.jpg?hash=-Y9bVMtlhI)