Zitto Zuberi Kabwe soma huu waraka ukusaidie kutekeleza azimio lako la hoja binafsi

Zitto ana wazo zuri ila kamwe hatapata sahihi za wabunge wa magamba. Hatafanikiwa

Hilo tunajua laweza tokea, lakini pia inaweza isiwe hivyo... Kikubwa Zitto tunaomba list ya watakao kuwa wamekweka hizo signature... ziwe zimetimia au hazikutumia ... tutajua wanafiki ni kina nani na tota dela nao huku majimboni.

Hapo ndio utaelewa wabunge maslahi na wanafiki ni kina nani... mapovu mengi mpaka wanalia... ikifika kwenye action wanagwaya.. utasikia sababu kibao.... tunaomba hayo majina pls.
 
Nimependekeza plan B kama hii itashindwa ni kukusanya sahihi za wananchi na kupeleka PETITION hiyo bungeni kutoka kwa wananchi this will work.

Brilliant idea..wananchi tukiamua NOTHING is impossible!!
 
Mh Zitto ni kweli kwa wazo lako wengi wa raia wema wa nchi yetu wanakuunga mkono. Hata hao wabunge wa CCM pia wanapenda iwe hivyo lakini ni woga tu ndio unawasumbua.

Sisi tumeamua kujitolea kuwashawisi wabunge wetu ili waweze kutia hizo sahihi ili upate kuwasilisha hoja binafsi. Ni kweli kama hutopata sahihi za wabunge wetu basi watakuwa wametusaliti kwa kiwango cha juu sana.

Hapo tunakuomba utusaidie ili na sisi kazi yetu iwe rahisi kuwatia adabu kwa usaliti wao. Baada ya kupata hizo sahihi tutakuomba utupe orodha ya wale walioweza kukupatia sahihi zao ili tuwajue wasaliti ni akina nani.

Unajua kwa jinsi wabunge walivyokuwa wakiongea kwa uchungu kiasi kile nitashangaa sana kama watashindwa kutumia nafasi hii kuiwajibisha serikali yao.

Haiwezekani kabisa eti uchangie kwa kupinga uozo wa serikali yako halafu unashindwa kuiwajibisha. Hapa Mh Zitto tunakuomba utuwekee orodha ya wote watakao saini.

Kushindwa kutupa hiyo orodha ni kutusaliti sisi wananchi wa Tanzania. Kwa kitendo hicho na wewe pia tutakuchukulia pia ni msaliti na mfitini wa taifa letu. Mimi naamini huwezi kutusaliti sisis watanzania wenzako.

Mungu akubariki na akulinde na wale wote wanaotaka kukufanyia ubaya!

Ubaya ni kwamba hata akiondoka anaenda kula pensheni kama mtangulizi wake za uPM mstaafu.
 
"All men are intellectuals but not all men have the function of intellectuals in the society"wabunge wanaonyeshwa kuguswa sana na kile kinachoendelea ndani ya jamhuri ya mungano wa tanzania lakin kujua kame kweli they mean what the are saying ni hapa kwenye brilliant idea proposed by zitto,hapo kwenye VOTE OF NO CONFIDENCE WITH THE PRIME MINISTER OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
 
Mkuu, huyo ana lake jambo, mbona sisi wengine tunaiona hii thread/waraka umetulia?
Nashukuru mkuu kwa kunielimisha. Kama nimeeleweka bsi ni vyema nikatoa shukurani kwa wale woote waliochangia huu uzi.
 
me na mshahuri mh filikunjombe ahamie airtel a.k.a CDM sababu naona juhudi ya kwahadabisha magamba kama ina unafki mwingi me naona ajitoe kule aje kwetu! me naona tutumie plan b kama inawezekana maana naona mpango wetu umeingiliwa na magamba!
 
Ni kweli mkuu Mnyisanzu, hawa wabunge huwa wanatuona sisi hatuna akili kabisa. Kwa hili ndio tutaona hivi ni kweli wabunge walikuwa wakiongea kwa kumaanisha au ni hadaa tu za kisiasa? Hivi Olesendeka kwa hili amesimama upande gani?
Ole Sendeka jana alikuwa anawashawishi wabunge wa CCM kuachana na hatua ya kuwatakata mawaziri na WM kujiuzulu eti nao ni watu wana mapungufu ya kibinadamu. (Gazeti Mwananchi - jana 20/04/2012). Ushahidi wa unafiki wa wabunge wa CCM. Hivi akina Sitta na Kilango mbona wako kimya. Au kwa mitazamo yao ufisadi umisha CCM?
 
Kuna ndg zangu wengine wanaamin kuwa akina sita,mwakyembe,kilango na sendeka wana dhamira ya dhati dhidi ya ufisad,niwambie ambao bado mnaiman na hao jamaa ondoa kabisa.kama kwel wangekuwa wanauchukia ufisad wangekuwa wameondoka ndan ya ccm kama mpendazoe.hao ni wanafik wakutupwa.walipanga kuondoka na uncle fred wakamtosa baada ya kuhaidiwa vyeo na msera.
 
Mimi nina mawazo tofauti. Wakati watu wengi, ikiwa ni pamoja na mimi tuanahamu ya kujua ni Mbunge yupi yu pamoja nasi, lakini labda si busara sana kumlazimisha Kamanda Zitto kuyatoa majina hayo katika mazingira yoyote. Mawazo yangu ni kuwa Zitto apime mazingira na aamue kama inafaa kutoa orodha hiyo. Bado tuna safari ndefu na huenda huko mbele tutahitaji hoja ya kutokuwa na imani na rais. Kama kwa mfano ikitokea hoja hii imeshindwa, wale watakao kuwa wabaya wa ccm kwa mfano, wanaweza kushughulikiwa kiana. Sasa ikitokea kura ya kutokuwa na imani na rais, hata kama watakuwa tayari kufanya hivyo, woga utakuja pale watakofikiri uwezekano wa kushindwa ilihali majina ya waliopiga yako hazarani. Si unajua viongozi wetu ni wa visasi. Kwahiyo ushauri wangu ni kuangalia mazingira. Nawasilisha
 
Back
Top Bottom