Maboso
JF-Expert Member
- Feb 18, 2013
- 5,164
- 5,761
Nadhani Zitto lengo lake ni kuuteka umma usiojua kwamba data za ndege zinapatikanaje. Ndege zimetengenezwa 2015 na zilikuwa hazijawahi kumilikiwa na shirika lolote zaidi ya watengenezaji ndio maana hata huku kwetu zilikuja na namba za kiwandani. Sasa yeye Zitto kusema ndege zilikuwa zinamilikiwa na Kazakstan ni uongo ulio wazi kabisa. Na anafanya hivyo kwa maksudi ya kumchafua Mh. Rais pamoja na serikali yake. Tatizo watu wanapokosa hoja za msingi wanabaki kutunga uongo kama huu. Ndege ni za Kazakstan iweje Bombadier ndio wafanye delivery kwetu? Iweje Bombadier wafanye publication kwenye website yao kwamba wameiuzia serikali ya Tanzania ndege mbili mpya? Ina maana Zitto anataka kutuambia kuwa Bombadier na serikali wameshirikiana kuudanganya umma? Jamani wanasiasa hebu ifike mahali tuache kujivua nguo kwa kusema uongo kwa vitu ambavyo ukweli wake upo hadharani. Kwani ukimpongeza mheshimiwa Rais na serikali yake kwa kazi nzuri wanayoifanya katika kufufua ATCL kuna tatizo gani? Mimi nizidi kumuomba Mh. Rais na serikali yake kwamba wasilegeze Kamba, waendelee na moyo huohuo wa kuwatumikia watanzania. Kazi nzuri wanayoifanya isikatishwe tamaa na wanasiasa wanaopenda kukosoa kila kitu.