Zitto Zuberi Kabwe ni Mchochezi. Akamatwe, Ashitakiwe kwa Uchochezi, adai Rais Magufuli ni...

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,513
113,640
Wanabodi,

Akizungumza kwenye mahojiano ya live kwenye kipindi cha Clouds 360 kinachorushwa na kituo cha TV cha Clouds TV, akizungumzia kuhusu ndege mpya za Bombadier, (Wakati Rais Magufuli akizizindua, rais alisema ndege hizo ni mpya kabisa na zimenunuliwa kwa direct sale kutoka kiwandani, bila kupitia kwa madalali), Mbunge wa Kigoma Mjini, Mhe. Zitto Zuberi Kabwe, ametangazia umma kupitia Clouds 360 kuwa ndege hizo sii mpya, bali ni ndege za mtumba wa kiwandani!, ya kuwa zilitengenezwa kwa ajili ya shirika la ndege la Kazakhstan, na sio kwa ajili ya Tanzania, tena akasema order ya Kazakhstani ni ndege 10, biashara ya kuuziwa Tanzania, imefanywa kupitia kwa madalali, na kilichokuwa kikifanyika, ilikuwa ni kuzipaka rangi tuu kwa kuchubua rangi ya Kazakhstan na kuzipaka rangi ya Tanzania ili zionekane ni mpya!.

Rais kama mkuu wa nchi na amiri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama, kauli yoyote ya rais, ndio kauli ya ukweli na ndio kauli ya mwisho, hivyo kama rais ameishasema kuwa ndege ni mpya, na zimenunuliwa kwa cash direct kutoka kiwandani, haiwezekani tena akaibuka Mtanzania mwingine yoyote wa kumbishia rais nchi, tena kwa kusema wazi, tena live kwenye TV, kuwa ndege zile ni mtumba na kwenye biashara hiyo kulikuwa na madalali!, huku ni kumuaibisha rais wetu, kutaka kuonyesha rais wetu amesema uongo, na yeye Zitto ndio anayesema ukweli, hivyo nashauri kwa hiki alichokisema Mhe. Zitto, akamatwe kwa haraka na kushitakiwa kwa uchochezi, wa kutoa maneno ya kashfa, yatakayopelekea kumkashifu na kumdhalilisha rais wetu kuonekana rais ni muongo!, na kufuatia jinsi mbunge huyu kijana, Zitto, alivyo na ushawishi mkubwa kwa kada ya vijana, vijana wa Tanzania, wanaweza kumuamini Zaidi Zitto badala ya rais wao na hivyo kumuona rais wao kama vile ni muongo, kitu ambacho sii kweli, wakati ukweli halisi, ni Zitto ndio atakuwa muongo na siku zote rais ndie mkweli daima.

Akisisitiza kuhusu ndege hizo, Mhe. Zitto pia amepingana na kauli ya rais kuwa gharama za ndege hizo ni siri za kibiashara kati ya shirika hilo la ndege na serikali ya Tanzania, Zitto anadai kuwa kwenye manunuzi ya umma, public procurement, hakuna siri yoyote ya biashara katika ununuzi wa manunuzi ya umma yanayotumia rasilimali za taifa, na kudai Watanzania wana haki ya kujua matumizi yote ya kila senti ya fedha za umma kwa ukweli na uwazi!, ndio maana kila senti ya matumizi ya umma yazima iwasilishwe bungeni, bunge liyapitishe, ndipo yatumike, lakini Fedha ya manunuzi ya ndege hizi, hazikuidhinishwa na Bunge, hivyo amehoji serikali inawezaje kufanya manunuzi makubwa hivi bila kuidhinishwa na Bunge?.

Huu pia ni uchochezi!, kama rais wa nchi ndie mkuu wa nchi na ndie mmiliki wa Fedha zote za umma, kuna ubaya gani akichota kiasi chochote kununulia chochote ambacho ni mali ya umma bila idhini ya Bunge?, tena amesema bei ya ndege ni ndogo ila ni siri ya kibiashara, halafu anaibuka mtu na kutofautiana na rais kuwa kwenye matumizi ya fedha za umma, yatatakiwa kufanyika kwa ushindani wa wazi, na hata kwenye restricted tendering, bado hakuna siri yoyote. Bunge lazima lijue, Watanzania wana haki ya kujua matumizi ya fedha zote za umma, maana ni fedha zao na ni kodi zao, na hata kama serikali itakopa, Bunge linapaswa ujulishwa, na Watanzania wajue deni la taifa, kwa sababu, wanaozilipa ni Watanzania!. Huku pia ni kutaka kumdhalilisha rais!, hivyo Zitto akamatwe ashitakiwe kwa uchochezi.

Rais kasema tumenunua ndege mpya moja kwa moja kutoka kiwandani na hakuna dalali, Zitto anasema tumenunua ndege mtumba za Kazakhstan toka kiwandani ambazo
hizo hizo fedha tulizolipa, tumepitia kwa dalali na hazikulipwa direct kiwandani, bali zimelipwa kupitia kwa dalali na zimekwenda sio kiwandani, bali kwa mwenye ndege Kazakhstan!.

Hata hivyo, huyu Zitto anaakili sana, ili kuepuka kushitakiwa kwa uchochezi, amesema japo ni kweli ndege hizo tayari zilikuwa ni mali ya shirika la ndege la Kazakstan na ziliishapakwa rangi ya Kazakstan, hivyo zimebadilishwa tuu rangi kupakwa rangi za Tanzania na vile zilikuwa bado hazijakabidhiwa Kazakhstan, then kwa Tanzania ni mpya . Hivyo ameitaka serikali iseme kweli, pesa zimelipwa kwa dalali gani na amelipwa nani kati ya kiwandani na mwenye ndege zake! . "Seek the truth and the truth will set you free" emphasis mine!.

Ukiondoa hoja ya upya au uutumba wa ndege hiyo, Mhe. Zitto ameupongeza uamuzi wa Serikali kufufua ATC na amempongeza rais Magufuli kwa uamuzi wa kununua ndege hizo na kueleza zitaleta unafuu mkubwa sana kwa usafiri wa anga japo ameshangaa kwa nini tununue kwa cash wakati option ya hire purchase ilikuwepo?!.

My Opinion, inawezekana ni kweli ndege zilikuwa za Kazakhstan ila wamezinunua mpya kutoka kiwandani kwa malipo ya hire purchase, ila kwa vile Tanzania imelipa cash, ikaamuliwa ndege mbili za Kazakhstan zibadilishwe rangi tupewe Tanzania wenye cash cash in hand hivyo tumewapiga tanchi wa Kazakhstan kwa ujanja kuwahi.

Zitto akasisitiza kuwa yeye ni mkweli daima Magufuli na serikali ya CCM wakifanya mambo mazuri anawaunga mkono na kuwapongeza hadharani ila wakifanya mambo ya hovyo hovyo kama kuzuia mikutano ya hadhara ya kisiasa, anawapinga bila kuogopa.

My Take.
Wanabodi, hoja sio nani ni mkweli na nani ni muongo kati ya Mhe. Zitto na rais Magufuli, but automatically rais Magufuli ndio mkweli na Zitto atakuwa ndie muongo, anastahili akamatwe, ashitakiwe kwa uchochezi!.

NB. Ukiona mtu amesema hadharani kuwa rais Magufuli amedanganya, na mtu huyo hajachukuliwa hatua zozote, lakini kwa vile rais hawezi kudanganya, then wenye akili lazima wajiulize kitu hapo, mkweli ni nani?!.
Paskali
 
Upinzani siku hizi umekuwa kimya mpaka unaboa.Bora Zitto kajitokeza.

Ajira zinapigwa danadana wapinzani kimya,madawa utata wako kimya,kuna watu elimu zao zinazua maswali wao wako kimya,n.k.

Upinzani badilikeni zamani hamkuwa hivyo.

Kuhusu Zitto,badala ya kumbuguzi,wampeleke mahakamani akathibitishe madai yake na wakishindwa kumshitaki basi wakubali yaishe.

Pasco wengi hawatakuelwa wakidhani unatetea kumbe uko tofauti.

Kuhusu usiri wa bei,je huenda ni kutokana na bei ya ndege labda kuwa ni ya ku-negotiate baina ya mteja na kampuni hivyo kampuni inataka iwe siri ila kila mteja anaekuja anunue kwa bei ya maelewano?

Kama bei ya ndege hizi ni fixed,sababu ya usiri huu ni nini hasa?

Alafu na zile bei tulizokuwa tunazisikia,zilitoka wapi?
 
Wewe Pasco ndo mchochezi namba moja. Mbona zitto kasema mambo mengi tu, wewe hilo ndo umeshika tu?? IPTL mbona hukuitaja kwenye huu uzi wako. La msingi tupigane na hoja za msingi, si kukimbia na kuanza kusema zitto ashtakiwe, kwa kipi? Hoja hutetewa kwa hoja, si majungu kama haya unayoleta hapa
 
Rais hawezi kusema uongo hata siku moja.Siku zote kauli ya Rais ni sawa na kauli ya Mungu kwakuwa yeye ni chaguo la Mungu na nimwakilishi wa Mungu hapa Tanzania kupingana au kupishana na kauli zake ni kumkosea Mungu na hivyo kujiongezea mzigo wa dhambi maradufu.

Hata kama ndege ni mtumba maadamu Rais kasema ni mpya ni bora kufuta kauli ya Rais ili kuepuka kubeba mzigo wa dhambi.
 
Wanabodi,

Akizungumza kwenye mahojiano ya live kwenye kipindi cha Clouds 360 kinachorushwa na kituo cha TV cha Clouds TV, akizungumzia kuhusu Ndege Mpya za Bombadier, (Wakati Rais Magufuli akizizindua alisema ndege hizo ni mpya na zimenunuliwa kwa direct sale kutoka kiwandani, bila kupitia kwa madalali), Mbunge wa Kigoma Mjini, Mhe. Zitto Zuberi Kabwe, ametangaza kuwa ndege hizo ni mtumba, zilinunuliwa na shirika la ndege la Kazakstan zikiwa ni ndege 10, biasharra imefanywa kupitia kwa madalali, na kilichokuwa kikifanyika, ilikuwa ni kuzipaka rangi tuu ili zionekane ni mpya!.

Kauli yoyote ya rais, ndio kauli ya ukweli na ndio kauli ya mwisho, hivyo kama rais ameishasema ndege ni mpya, na zimenunuliwa toka kiwandani, haiwezekani tena akaibuka Mtanzania mwingine na kusema wazi, tena live kuwa ndege zile ni mtumba na kwenye biashara hiyo kulikuwa na madalali!, huku ni kumuaibisha rais wetu, kutaka kuonyesha rais amesema uongo, na yeye Zitoo ndio anayesema kweli, hivyo nashauri Mhe. Zitto akamatwe kwa haraka na kushitakiwa kwa uchochezi, kufuatia ushawishi mkubwa alionao mbunge huyu kwa kada ya vijana, wanaweza kumuamini Zitto na kumuona rais wetu ni muongo, wakati ukweli halisi, Zitto ndio atakuwa muongo!.

Akisisitiza kuhusu ndege hizo, Mhe. Zitto pia amepingana na kauli ya rais kuwa ngarama za ndege hizo ni siri za kibiashara, Zitto anadai kuwa hakuna siri yoyote ya biashara katika ununuzi wa rasilimali za taifa, Watanzania wana haki ya kujua matumizi ya kila senti ya fedha za umma!, huu pia ni uchochezi!, kama rais amesema bei ya ndege ni siri ya kibiashara, halafu mtu anaibuka na kutofautiana na rais kuwa kwenye matumizi ya fedha za umma, hakuna siri yoyote!, huku ni kutaka kumdhalilisha rais!, akamatwe ashitakiwe kwa uchochezi.

Rais kasema tumenunua ndege mpya moja kwa moja kutoka kiwandani na hakuna dalali, Zitto anasema tumenunua ndege mtumba kutoka Kazastan na tumepitia kwa dalali, hivyo hizo fedha zimekwenda kwa mwenye ndege!.

Hata hivyo, huyu Zitto anaakili sana, ili kuepuka kushitakiwa kwa uchochezi, amesema japo ni kweli ndege hizo tayari zilikuwa ni za shirika la ndege la Kazakstan ziliishapakwa rangi za nchi hiyo, ila inawezekana zilikuwa bado mpya kweli ila kwa vile ziliishapakwa rangi ya Kazakstan, hivyo zimebadilishwa tuu rangi kuguswa za Tanzania . Hivyo ameitaka serikali iseme kweli, Pesa zimelipwa kwa dalali gani na amelipwa nani kati ya kiwandani na mwenye ndege zake! . "Seek the truth and the truth will set you free" emphasis mine!.

Hapa hoja sio nani ni mkweli na nani ni muongo kati ya Mhe. Zitto na rais Magufuli, but automatically rais Magufuli ndio mkweli na Zitto atakuwa ndie muongo, akamatwe, ashitakiwe kwa uchochezi! .

Pasco
Daaaaah haya mambo ni magumu sana lakini ingawa Nina wasi wasi bado siwezi mwamini Zitto mpaka alete vielelezo vya Tuhuma zake .

Ni kwa Mara ya pili sasa anauma na kupuliza kama si kweli basi huyu ndiye haini namba moja nchini..
 
Rais hawezi kusema uongo hata siku moja.Siku zote kauli ya Rais ni sawa na kauli ya Mungu kwakuwa yeye ni chaguo la Mungu na nimwakilishi wa Mungu hapa Tanzania kupingana au kupishana na kauli zake ni kumkosea Mungu na hivyo kujiongezea mzigo wa dhambi maradufu.

Hata kama ndege ni mtumba maadamu Rais kasema ni mpya ni bora kufuta kauli ya Rais ili kuepuka kubeba mzigo wa dhambi.
Ni kweli kabisa, unajua mimi mpaka leo naamini saddam hussein ni rais wa Kuwait, maana ni kauli ya rais na hajawahi kubadili
 
upload_2016-10-6_10-18-58.png
 
Wanabodi,

Akizungumza kwenye mahojiano ya live kwenye kipindi cha Clouds 360 kinachorushwa na kituo cha TV cha Clouds TV, akizungumzia kuhusu Ndege Mpya za Bombadier, (Wakati Rais Magufuli akizizindua alisema ndege hizo ni mpya na zimenunuliwa kwa direct sale kutoka kiwandani, bila kupitia kwa madalali), Mbunge wa Kigoma Mjini, Mhe. Zitto Zuberi Kabwe, ametangaza kuwa ndege hizo ni mtumba, zilinunuliwa na shirika la ndege la Kazakstan zikiwa ni ndege 10, biasharra imefanywa kupitia kwa madalali, na kilichokuwa kikifanyika, ilikuwa ni kuzipaka rangi tuu ili zionekane ni mpya!.

Kauli yoyote ya rais, ndio kauli ya ukweli na ndio kauli ya mwisho, hivyo kama rais ameishasema ndege ni mpya, na zimenunuliwa toka kiwandani, haiwezekani tena akaibuka Mtanzania mwingine na kusema wazi, tena live kuwa ndege zile ni mtumba na kwenye biashara hiyo kulikuwa na madalali!, huku ni kumuaibisha rais wetu, kutaka kuonyesha rais amesema uongo, na yeye Zitoo ndio anayesema kweli, hivyo nashauri Mhe. Zitto akamatwe kwa haraka na kushitakiwa kwa uchochezi, kufuatia ushawishi mkubwa alionao mbunge huyu kwa kada ya vijana, wanaweza kumuamini Zitto na kumuona rais wetu ni muongo, wakati ukweli halisi, Zitto ndio atakuwa muongo!.

Akisisitiza kuhusu ndege hizo, Mhe. Zitto pia amepingana na kauli ya rais kuwa ngarama za ndege hizo ni siri za kibiashara, Zitto anadai kuwa hakuna siri yoyote ya biashara katika ununuzi wa rasilimali za taifa, Watanzania wana haki ya kujua matumizi ya kila senti ya fedha za umma!, huu pia ni uchochezi!, kama rais amesema bei ya ndege ni siri ya kibiashara, halafu mtu anaibuka na kutofautiana na rais kuwa kwenye matumizi ya fedha za umma, hakuna siri yoyote!, huku ni kutaka kumdhalilisha rais!, akamatwe ashitakiwe kwa uchochezi.

Rais kasema tumenunua ndege mpya moja kwa moja kutoka kiwandani na hakuna dalali, Zitto anasema tumenunua ndege mtumba kutoka Kazastan na tumepitia kwa dalali, hivyo hizo fedha zimekwenda kwa mwenye ndege!.

Hata hivyo, huyu Zitto anaakili sana, ili kuepuka kushitakiwa kwa uchochezi, amesema japo ni kweli ndege hizo tayari zilikuwa ni za shirika la ndege la Kazakstan ziliishapakwa rangi za nchi hiyo, ila inawezekana zilikuwa bado mpya kweli ila kwa vile ziliishapakwa rangi ya Kazakstan, hivyo zimebadilishwa tuu rangi kuguswa za Tanzania . Hivyo ameitaka serikali iseme kweli, Pesa zimelipwa kwa dalali gani na amelipwa nani kati ya kiwandani na mwenye ndege zake! . "Seek the truth and the truth will set you free" emphasis mine!.

Hapa hoja sio nani ni mkweli na nani ni muongo kati ya Mhe. Zitto na rais Magufuli, but automatically rais Magufuli ndio mkweli na Zitto atakuwa ndie muongo, akamatwe, ashitakiwe kwa uchochezi! .

Pasco

shikamoo afande Sele. umemkurupusha bosi wako naona!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom