#COVID19 Zitto: Waziri wa Afya afukuzwe kazi sababu haaminiki na aliongoza kampeni ya watu kunywa sumu

Dorotia mambo yake valuvalu sana,hii wizara na naibu wake huwa hawaeleweki.

Taarifa hazijitoshelezi kwa umma.

Kama vipi wapitishie taarifa kwa msemaji wa serikali ili amdadisi kwanza kabla ya walaji.
Pale tulipigwa
 
Sio kazi ya Zitto kutoa takwimu. Ila zinapotolewa takwimu na mamlaka husika na kwa uelewa wake akaona zina kasoro (fake), ana haki na wajibu wa kutujulisha. Zitto ni kiongozi anayeheshimika ktk jamii, na kama unaona amekengeuka, au unaona waziri yuko sahihi tupe ushahidi utakuwa umesaidia.
Wakutoa ushahidi ni nyie msioamini tamko la waziri
Namba hujibiwa kwa namba
 
Tatizo la Zitto ni kujifanya anajua kila kitu Tanzania aipimi COVID ndani ya nchi. Na COVID sio ugonjwa hatari ivyo for under 50 hadi uende hospitali ni baadhi ya ile risk age groups (over 50 ndio wakipata wanakuwa hospitalised).

Sasa it’s possible kabisa kwa sasa kuna watu 400 na ushee waliojitokeza (mostly ni ile age group au wenye magonjwa yanayopunguza kinga ya mwili) na kati yao 69% ndio wenye kutumia mitungi. Ni takwamu ndogo sana ya wagonjwa kusema nchi ina tatizo la COVID.

Nchi za ulaya nyingi washapiga dose mbili watu wote over 50 na karibia over 40 wote washapigwa dose moja au mbili ya vaccine; baada ya kumaliza hayo makundi ndio sasa wanafungulia nchi aina maana COVID imeisha kabisa.

Kwa U.K. nadhani week hii pekee kuna watu zaidi ya 30000 na number inaweza kuwa kubwa maana wengine awapimi wameambukizwa lakini usikii kelele tena kwa sababu wanaopata ni vijana na wengi (under 40) wanajitibia wenyewe majumbani wakishapomwa; wazee wanaopata na kwenda hospitali ni wale waliokuwa wakaidi awakwenda kupigwa chanjo na idadi yao ni ndogo sana na vifo pia ni vidogo sana.

Sasa kwa nchi kama Tanzania ambayo aikuwa na lockdown, COVID itakuwa tatizo kweli leo watu wengi wameshapata COVID sema aikuwa na madhara; na bado ipo lakini sio kama serikali inavyoikuza leo.
kama unalazimisha tuamini hivi ,hunatofauti na aliyesema watanzania mniamini Mimi amekufa kwa ajali

Sent from my TECNO F2 using JamiiForums mobile app
 
kama unalazimisha tuamini hivi ,hunatofauti na aliyesema watanzania mniamini Mimi amekufa kwa ajali

Sent from my TECNO F2 using JamiiForums mobile app
Mjomba kama wewe unajijua miaka yako 50+ we jivalie barakoa; hiyo COVID waachie vijana waambukizane.

Boris Johnson mwenzako anaona rate ya 30000 kwa week kwenye maambukizi wakati wanaopata ni vijana tu siku hizi aitoshi; tarehe 19 week ijayo anafuta COVID restrictions zote na ma disco yarudi kama kawa ili vijana waambukizane vizuri elfu thelasini kwa week wanawachelewesha ili gonjwa kupita.

COVID aina madhara kwa vijana hao wanaoenda hospitali Tanzania ni wazee; na Tanzania kwa sababu atupimi mpaka uende hospitali takwimu za wagonjwa ndani ya nchi ndio hizo hizo za hospitali; sasa hapa cha kumbishia waziri kiko wapi.

Zitto kaishiwa kisiasa siku hizi hajui ata anasimamia nini we mambo ya Tigris wakati audience yake ni watanzania yanamuhusu nini kama sio anaanza kuwa mental case na yeye kama wale mashangazi wa Twitter.
 
Anaandika Mh Zitto Kabwe:

69% ya wagonjwa wote wakisaidiwa kwa mashine?

1) Hizi takwimu sio za kweli kwa maana wagonjwa ni wengi zaidi ya hao.

2) Waziri kaamua kusema Hata kwenye idadi ya wanaosaidiwa kupumua.

3) Huyu Waziri haaminiki kwa sababu aliongoza Kampeni ya Watu kunywa Sumu. AFUKUZWE KAZI

Katika kila wagonjwa wa UVIKO-19 nchini, 7 wanatumia mitungi ya Gesi! Hii ni rekodi ya Dunia. Haiwezekani, wagonjwa ni wengi zaidi. Kama wenye kutumia msaada wa Gesi ni hao basi wagonjwa ni mara 600 ya hao wanaotajwa.

Tuendelee kujilinda
Mtafuta attention pamoja anasema mambo ya kweli Ila I don't trust this son of Jezebel
 
Acheni kumsingizia Dorothy, ni Magufuli na maaskofu na Mashehe waliotuambia tuombe, tufunge na tujifukize.
Naomba uwe specific kwa maaskofu, gwajiboy na yule sheikh wa mkoa mkuu, hao wengine usiwasingizie. Wapo maaskofu wengine mpaka walitoa likizo za ibada mpaka mwendazake akawachukia
 
Kiukweli hili tatizo halihitaji waziri mwenye ndimi mbili, waziri huyuhuyu aliwadanganya watu na sasa anakuja vingine, back Ummy Mwalimu, aliitumikia nafasi yake vilivyo
Niliandika post ya hivi,mods wakabarn,is it not partiality?
 
Zito alete takwimu zake, alizofanya utafiti sio kupiga makelele. Yeye na waziri wa afya nani mwenye haki yakutoa takwimu za uviko-19

Takwimu zinatolewa na mamlaka maalum ni kinyume Cha sheria kila mtu kutoa takwimu....
Zito ana haki ya kutoa maoni.
 
Binafsi waziri wa afya na yule wa mambo ya nje siwaelewi kabisa hata jinsi wanavyoongea,
 
Takwimu zinatolewa na mamlaka maalum ni kinyume Cha sheria kila mtu kutoa takwimu....
Zito ana haki ya kutoa maoni.
Alichotoa zitto sio maoni ni kaja na takwimu zake ambazo hazina tafiti. Kusema Kuna wagonjwa zaidi ya... hii ni takwimu/idadi
 
Back
Top Bottom