Zitto: Wanasheria tazameni namna ya kuwajibisha ofisi ya DPP kwa uonevu wa Lema na wananchi wengine

TLS ni chama cha mwanasheria hakina nguvu wala uwezo wa kumwajibisha yeyote nje ya chama zaidi ya wanachama wao acha porojo Na kampeni zililizo chini ya kiwango
Sipigi kampeni na wala hakuna sehemu niliyosema Lisu atawawajibisha!!

Point muhimu hapa ni kuwa inaonekana hata wanasheria akili zao zimeshikwa na CCM kiasi kwamba wamesahau haki zao kama wanasheria na raia wa nchi!!

Kama watapata kiongozi atakayewakumbusha na kufanya kazi kwa madhumuni ya uanzishwaji wa TLS basi utaelewa.

Sasa kama wanasheria wanaogopa ............ vipi raia wa kawaida huko mtaani!!?
 
Mnamkamata mtu kwa kosa lenye dhamana. Mahakama Kuu inaruhusu dhamana. Serikali inakataa rufaa kuzuia dhamana. Mtu anakaa jela miezi 4, tena mwakilishi wa watu. Siku ya hukumu kuhusu dhamana Serikali inaondoa shauri mbele ya jopo la majaji 3.

Lengo? Kumkomoa mtu. Siasa za ukomoaji zinajenga chuki kwenye jamii na chuki inazaa visasi.

Haitoshi majaji kukemea Ofisi ya DPP. Mfumo wetu lazima uweke uwezo wa waendesha mashtaka wa aina ya kesi ya Mbunge wa Arusha Mjini kuwajibishwa. Wanasheria tazameni namna ya kuwajibisha ofisi ya DPP kwa uonevu wa makusudi dhidi ya wananchi

zito kama vile amerukwa na AKILI vilema dpp anahusikaje kwenye kutoa dhamana mwendesha mashtaka anayohaki ya jupinga dhamana ya mshtakiwa na mahakama ikajiridhisha na mashiko ya ya kutokutoa dhamana shida iko wapi
 
Nadhani mahakama ifate sheria tu.
Kesi inahusu kosa ambalo dhamana ipo wazi basi...watoe dhamana na DPP asiwe yeye ndo kama jaji.
Ruhsa hii inatumiwa kisiasa sana na utaona ni kesi za kisiasa ndo kinatumiwa. Katiba imeshaweka wazi haki ya dhamana basi kusiwe na kisingizio wala pressure...
Au ushauri wa Zitto ipingwe mahakamani uwezo huo wa Dpp .
 
Mnamkamata mtu kwa kosa lenye dhamana. Mahakama Kuu inaruhusu dhamana. Serikali inakataa rufaa kuzuia dhamana. Mtu anakaa jela miezi 4, tena mwakilishi wa watu. Siku ya hukumu kuhusu dhamana Serikali inaondoa shauri mbele ya jopo la majaji 3.

Lengo? Kumkomoa mtu. Siasa za ukomoaji zinajenga chuki kwenye jamii na chuki inazaa visasi.

Haitoshi majaji kukemea Ofisi ya DPP. Mfumo wetu lazima uweke uwezo wa waendesha mashtaka wa aina ya kesi ya Mbunge wa Arusha Mjini kuwajibishwa. Wanasheria tazameni namna ya kuwajibisha ofisi ya DPP kwa uonevu wa makusudi dhidi ya wananchi
Sitegemei maendeleo zaidi ya kurudi nyuma kimaendeleo kama tu mwendo wenyewe utakuwa wa hvi(chuki)
 
huyu dppp alichaguliwa kwa sababu alikuwa anaishi jirani na mahakama .lakini alikula kiapo sijui cha kumdanganya nani ? mungu?
 
Naunga mkono hoja, hata kama hakuna hatua zitakazochukuliwa lakini wananchi watazidi kufahamu jinsi gani awamu hii ya tano inaongoza kwa kukiuka sheria.
 
Tusubiri TLS watawapa adhabu gani hao mawakili wa DPP/AG waliotumia mfumo kumwonea mtu. Hapo ndio tutajua TLS ipokwa ajili ya haki na wanyonge
Mawakili WA Serikali hawapo TLS! WAO WAPO CHINI YA ATTORNEY GENERAL! INGAWA A.G HUWA Wakili Namba 1 kwa wote!
 
Back
Top Bottom