Zitto usipeleke hoja Jumatatu; be strategic...

Nadhani Zitto anganza na kutafuta ushawishi wa kura za kuto kuwa na imani na spika halafu akipatikana mtu kama Sita pale kwenye kiti suala la kupiga kura za kutokuwa na imani na PM pamoja na boss wake ni kama kumsukuma mlevi na hapo ndio bunge litavunjwa kiulaini.
 

BIG POINT Mzee Mwanakijiji......................tunachohitaji ni kumwondoa JK na wala siyo PM.......tulimwondoa Lowassa na baadhi ya mawaziri na matatizo bado yako palepale...............sasa anayefaa kuondoka ni JK.....................ashitakiwe sasa khalafu mengineyo yatafuata................nchi hii maisha yamekuwa magumu kupita kiasi na ni yeye tu wa kushikishwa adabu........
 
Inabidi uje bungeni na wewe sasa, kudandia au ku-improvove hoja za watu si vizuri sana na hasa unapoongelea impossibilities...

you have written utopia

wewe uko bungeni? kwanini unafikiri watu wengi wanapenda kuingia Bungeni?
 

I am 99% right... don't doubt me.
 
Short-term apeleke. Long-term asipeleke.

A qstn: btn CHOICE and STRATEGIES what should come first here?
 

Mkuu hiyo sababu ya kuidhalilisha ofisi ya Rais imekaa vibaya; sijui mtu atai prove vipi na kumfanya Spika akubali hoja kujadiliwa. Hiyo ndio nyepesi kulinganisha na zingine. Lakini kwa Waziri Mkuu kuna hii ya kushindwa kuisimamia serikali. Hiyo iko wazi kama mawaziri wanashutumiwa na kutuhumiwa kwa wizi si ina maana hawasimamiwi vizuri! Msimamiaji wao kashindwa na kwa mujibu wa Katiba msimamiaji ni Waziri Mkuu. Zitto ameona kitu ndio maana akataka aanze kuimong'onyoa serikali kuanzia shinani asikimbilie kwenye mzizi kwa kuwa mzizi ni mgumu kidogo kulinganisha na shina na matawi yake. Mizizi ikikosa hewa na chakula inaweza kunyong'onyea. Hiyo sababu ya kusimamia ingekuwa pia ndiyo mojawapo ya sababu za kumshtaki Rais bungeni mbona Zitto angeenda moja kwa moja tu na kutafuta saini 70 kwa ajili ya kumshtaki Rais.
 
Mi nadhani wacha tuanze na hili tumbo joto la waziri mkuu kwanza, ili watanzania waone kama haya mambo yanawezekana...unajua watanzania wanatakiwa wafumbuliwe macho kwanza
 
lakini zitto si alitoa ultimatum;? kwamba mpaka kufika J3 kama mawaziri waliotajwa na CAG hawajajiuzulu atapeleka hoja bungeni? sasa si wamejiuzulu!

Wako wapi waliojiuzulu? na kama wamejiuzulu, jee Rais aliyewateua kakubali? Tafakari, usisikie udaku wa JF ukajuwa ndio ukweli.
 
Kaka au Dada (sielewi ipi sahihi) unaejiita MzeeMwanakijiji, ngoja chama chako cha CCK ndio ukipe ushauri huo. Zitto anapeleka Jumatatu na yeye anakijuwa akifanyacho zaidi yako. Ushauri wako hauna mshiko.

Now, Kikwete akipenda just to outplay everybody atatangaza tu kuvunja baraza na akaunda baraza jipya chini ya PInda huyo huyo. Halafu itabidi ipigwe kura ya kumkubali kama waziri mkuu (namna nyingine ya kuwalazimisha watu kupiga kura ya kuwa na imani naye au la).. It is a war, na vita vinapiganwa kwa strategy! Thats all I'm saying. Hii hoja ikipelekwa j'tatu the oppossion WILL lose the argument ya change.

Mkuu Ribosme, soma vizuri hayo maelezo ya mwisho ya Mwanakijiji. Mimi naona yana uzito fulani hasa hapo kwenye red. Tafakari.
 
I am 99% right... don't doubt me.

...Ni kweli kabisa, upo sahihi sio kwa 99% bali ni kwa 100% kabisa lakini ni kwenye "ulimwengu wa ndoto" tu usiowezekana katika mazingira ya Tanzania ya sasa, naamini unaijua hii reality vizuri sana lakini unapinga tu for the sake of debating kama class mate wa Salma2015....


...Katika hoja hii, atleast approach ya Zitto inaweza kuleta matokeo chanya lakini approach yako ni kama "the bridge to NoWhere"...
 
Napenda kuwakumbusha wana bodi, tusidhani CCM nao wamelala kwenye hili! Kama kweli mawaziri wameanza kujiuzuru, hoja itapoteza mashiko!!

Nina uhakika kura 178 za kumuondoa PM hazitapatikana...wait and see.
 
Binafsi naamini kama kweli mawaziri watajiuzulu inavyosemwa itaharibu kwa kiasi hoja ya kutikuwa na imani na waziri mkuu. Think about it!

hapa kunahitajika plan B iwepo ambayo lazima ifikie lengo la awali na isije kujikuta inaishia hewani na kukosa maana halisi .. maana baada ya kujiuzuru kila mtu ataamini wanatakiwa wapewe muda kwa ajili ya kuona matokeo ya hayo mabadiliko lakini bado hao watakaochaguliwa hawatasaidia chochote kwani kwenye hizi wizara kuna makatibu wakuu n.k ... je hili watu wanalitazamaje?
 
ndugu MWANAKIJIJI kwa kiasi una hoja japokuwa unasahau kuwa kuelekea 2015 CCM ina wadau ambao hawana cha kupoteza(waadilifu wasiotaka kugombea tena) na ambao wakichekelea watapata hasara(vijana waadilifu ambao kimsingi wanakubalika kwa wapiga kura na wana nia ya kuendelea) na wapo mafisadi ambao wanajua siyo tu kuwa hawakubaliki lakini hata hatari ya kuingia jela inawakabili.CDM ikipeleka hoja ya kumtoa Pinda hatari kubwa iko kwa Pinda maana kimsingi ana dalili zote za kuwa MBABAISHAJI na kwa hiyo CDM na CCM-2015 + watampa kichapo, jumlisha na waoga, wazee waadilifu na wanamtandao waliowekwa kando na kuitwa magamba,zisipotimia za kumchinjia baharini Pinda bado zitaweka historia dhidi ya Pinda JK na wabadhirifu wote kuywa hawawezi kufanya hayo yote and get away with it!
 
Ninakubalina nawe Mwanakijiji kwa kiasi kikubwa. Lakini pia ninatofautiana nawe kwa sehemu fulani. Labda nitoe hoja zangu kwanza kisha nitaeleza ni kwa namna gani tunatofautiana, na similarities will take care themselves.

Ikumbukwe kuwa kumuwajibisha kiongozi wa nchi kidemokrasia ni kama ni tukio la kipekee. Labda hata hizo fikra hazijawahi kuwepo achilia mbali uthubutu. Hii ndio imepelekea viongozi wengi, hasa katika ngazi ya uwaziri kujifanyia mambo watakavyo, ilimradi tu wana-uswahiba na Rais. Mara kadhaa tumemsikia Pinda akisema Mamlaka yangekuwa yangu ningemuondoa huyo mtu leo. Kwamba yupo mtu juu yake ambaye ni rafiki wa mkosefu huyu na ndiye aliye muweka. Mimi sina jeuri ya kumuwajibisha.

Maana yake ni hii. Watendaji wakuu kama Makatibu wakuu kwa upande mmoja, na Mawaziri kwa upande mwingine, maadam wana-uswahiba na rais, kamwe hawatafiria kuwajibika kwa maslahi ya taifa. Watafanya kazi kwa maslahi yao binafsi au kikundi kidogo cha watu.

Hoja kama hii ya Zitto, kwa kiasi fulani inawakumbusha hawa miungu watu, ikiwa ni pamoja na Rais kuwa kuna uwezekano wa kuwaondoa kama watu watachoshwa kabisa na madudu wanayoyafanya. Hii walau italeta nidhamu na kuongeza ufanisi.

Wakati tunahitaji mabadiliko makubwa ya kimfumo (ambayo ndiyo ndugu yangu Mwanakijiji unayalenga), tunahitaji pia kuonyesha nini kinawezekana kwa sasa. Lengo letu kuu ni kuwa na taifa bora, lenye kutumia rasilimali zake kwa manufaa ya wananchi wote. Ikiwa tendo kama hili linaweza kubadilisha mwelelkeo wa watawala, na kuwa na ufanisi, hilo tunalikubali. Ikiwa hakuna mabadiliko, we go for the great change. The good thing is we have all we need for both. Immediate and planned great future change.

Kwahiyo tofauti zetu Mkuu mwanakijiji ni kuwa, kile kidogo kinachowezekana, na kifanyike sasa wakati tunajipanga kufanya makubwa zaidi. Who knows, inawezekana hata hiki kidogo kikalipa!
 
mh zitto siku zote natambua uwezo wako kifikra,kiutendaji na msimamo wako kiutendaji na wabunge wote wa chadema ninachoweza kusema ni kwamba watanzania tumeona juhudi zenu nadhani wengi watakubaliana nami kuwa wabunge mmeacha itikadi zenu ili kutetea maslahi ya watanzania hii inaleta faraja, natoa pongezi za dhati kwake filikunjombe lugola na wabunge wote wa ccm waliokuunga mkono wewe zitto,huu komaa na kura hizo kwa manufaa ya wana wa tanzania naamini viongozi wabovu na wazembe wa kufannya maamuzi mwisho wao umefika.:A S shade:
 
mh zitto siku zote natambua uwezo wako kifikra,kiutendaji na msimamo wako kiutendaji na wabunge wote wa chadema ninachoweza kusema ni kwamba watanzania tumeona juhudi zenu nadhani wengi watakubaliana nami kuwa wabunge mmeacha itikadi zenu ili kutetea maslahi ya watanzania hii inaleta faraja, natoa pongezi za dhati kwake filikunjombe lugola na wabunge wote wa ccm waliokuunga mkono wewe zitto,huu ni mwanzo mzuri komaa na kura hizo kwa manufaa ya wana wa tanzania naamini viongozi wabovu na wazembe wa kufannya maamuzi mwisho wao umefika.:A S shade:
 

Namba moja ni sawa, lakini namba 2; hata kama watakatifu wote na malaika watapiga magoti kukiombea chama tawala kijikosoe - HAIWEZEKANI. CCM ni janga la kitaifa, halina dawa, hata kiungo kikishambuliwa na kansa madaktari huwa wanashauri kikatwe tu!
 
Kwa mara ya kwanza kabisa nimeshuhudia makundi makubwa sana ya watu sehemu ambazo zina tv.Makundi ambayo nimezoea kuyaona wakati wa mechi za soka.Jambo ambalo sijalijua ni sababu ya watu kufanya hivyo!Kuhusu mada hii ya MM Mwanakijiji nakubaliana nayo,tulishashuhudia kujiuzulu kwa mawaziri lakini hakukua na mpya.Tatizo ni serikali haina mpya na imeshindwa kutimiza majukumu yake kama serikali,hili liko wazi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…