mcubic
JF-Expert Member
- Mar 3, 2011
- 10,307
- 6,514
Kwenye ukurasa wake wa FB ameainisha haya
"Ni muhimu kufungamanisha sekta ya Kilimo na Sekta ya Viwanda. Uongezaji wa thamani wa bidhaa za kilimo kuanzia vijijini kwa kuwa na viwanda vidogo vidogo ndio njia sahihi ya kuanzia. Ni muhimu kujifunza 'sequencing'. Huwezi kutamka tu VIWANDA na vikashuka. Lazima kufanya kazi ya kitaalamu ya kufikiri. Uongozi sio matamko tu bali ni kuweka dira na kusimamia kuona mikakati ya kufikia Dira hiyo inatekelezwa. Tunaweza kuwa Nchi ya Viwanda. Tunaweza. Lakini ni lazima tuondoke kwenye propaganda na kujielekeza kwenye kufikiri na kutenda. Mahala pa kuanzia ni shambani. Kwanini hatulimi miwa wa kutosha ili tuuze nje sukari badala ya kuagiza sukari. Kwanini hatulimi Pamba ya kutosha ili viwanda vya nguo viwe kila kanda ya nchi na kuuza nje nguo? Kwanini tunashindwa teknolojia rahisi kabisa ya kubangua korosho vijijini ili wakulima wapate fedha zaidi? Tuache propaganda. Tuishi tunayoyahubiri. Hotuba zitoshe tuone kazi ikifanyika."
Nionavyo:
Siasa za masuala ndio hizi, unakosoa huku unatoa na njia za kufikia suluhisho....na si kupayuka tu.