Zitto: Ujenzi wa CHADEMA imara - Fuata misingi!

Zitto: Ujenzi wa CHADEMA imara - Fuata misingi!

Status
Not open for further replies.

Mzizi wa Mbuyu

JF-Expert Member
Joined
May 15, 2009
Posts
7,467
Reaction score
7,258
MWAKA 1995 Tanzania ilifanya Uchaguzi Mkuu wa kwanza tangu irejeshe mfumo wa vyama vingi na Chama cha CHADEMA kilikuwa kimeshiriki uchaguzi huu bila ya kuweka mgombea urais hivyo kulazimika kumuunga mkono mgombea wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Augustino Lyatonga Mrema.

Katika uchaguzi huu wa mwaka 1995 CHADEMA ilipata asilimia sita ya kura zote za wabunge nchini na kupata majimbo matatu ya Kigoma Mjini, Karatu na Rombo. Kilishika nafasi ya tatu katika vyama vya upinzani baada ya Chama cha Wananchi (CUF) na NCCR-Mageuzi.

Mwaka huo CHADEMA iliingia kwenye uchaguzi chini ya viongozi waasisi wa chama mzee Edwin Mtei kama Mwenyekiti, Brown Ngwilulupi kama Makamu Mwenyekiti na Bob Nyanga Makani kama Katibu Mkuu.

Mwaka 2000 Tanzania ilifanya uchaguzi Mkuu wa pili, na CHADEMA kilikuwa kimeshiriki uchaguzi huu kwa mara nyingine bila ya kuweka mgombea urais. CHADEMA ilishirikiana na CUF kuweka mgombea mmoja Prof. Ibrahim Lipumba.

Mwaka huo chama chetu kilipata asilimia tatu ya kura za wabunge na jumla ya wabunge wanne na kushika nafasi ya nne katika vyama vya upinzani baada ya vyama vya CUF, TLP na UDP.

Katika uchaguzi wa mwaka 2000 Mzee Makani alikuwa Mwenyekiti, Dk. Willibrod Slaa Makamu Mwenyekiti na Dk. Amani Kabourou kama Katibu Mkuu. Miongoni mwa wabunge wapya wa CHADEMA waliochaguliwa mwaka 2000 ni pamoja na Freeman Mbowe kutoka Jimbo la Hai.

CHADEMA ilipoteza Jimbo la Rombo, ikaongeza Hai na Moshi Mjini na kulinda Karatu na Kigoma Mjini. Ni vema ieleweke kuwa tangu mfumo wa vyama vingi uanze mikoa ya Kigoma, Arusha na Kilimanjaro imeweka rekodi ya kutoa mbunge angalau mmoja wa chama hiki. Karatu ni wilaya iliyoweka rekodi ya kuchagua CHADEMA mara nne mfululizo tangu mfumo wa vyama vingi uanze.

Mazingira haya ya chama cha tano kwa wingi wa kura katika vyama vyote vya siasa nchini ndiyo mazingira iliyoingia nayo CHADEMA katika uchaguzi wa mwaka 2005. Mazingira ya kukatisha tamaa, kwani ujanja mjini haukuwa kwa CHADEMA; bali CUF au TLP na zaidi CCM. Mazingira ya kijana ukisema upo CHADEMA vijana wenzako wanakuangalia jicho la mshangao na hata kuchekwa.

Haya ndiyo mazingira ambayo alirithi Freeman Mbowe, kama mwenyekiti wa CHADEMA.

Mbowe alianza harakati zake za kuimarisha CHADEMA kwa kukusanya vijana mbalimbali, wanachama wa CHADEMA na wasio wanachama, kutoka makundi mbalimbali ya jamii kama wanafunzi wa vyuo vikuu, waandishi wa habari, wanasiasa kutoka vyama vingine na hata vijana wanaharakati katika NGOs nk.

Moja ya msingi wa CHADEMA ni ‘kujenga chama chenye kutoa fursa ambapo kila mtu, bila kujali asili na hali yake, anaweza kutimiza na kufanikiwa kadiri ya vipaji vyake. Kwa mwanasiasa mwingine yeyote nafasi hii ilikuwa ni nafasi nzuri ya kujitengenezea fursa yeye mwenyewe kwa kuhamasisha ufuasi wa watu badala ya ufuasi wa misingi ya chama. Badala yake, Mbowe alitoa fursa kwa kila mwanachama kuchangia katika kuendesha na kuimarisha chama. Na hii ndiyo ilikuwa kauli ya Mbowe kila wakati kwamba ‘chama ni fursa'.. Tuone ni namna gani Mbowe alitumia misingi ya CHADEMA kwa kujenga na kuimarisha chama.

Kazi hii ya kukusanya watu mbalimbali na mikakati ya kuanza kusambaza chama kwa kufanya ziara za wabunge na baadhi ya viongozi wa chama ilianza mwaka 2003 ambapo wanasiasa wengi vijana waliokata tamaa na siasa za vyama vyao walianza kuona matumaini ndani ya CHADEMA.

Mwaka 2004 mwezi Machi, Mbowe akachaguliwa kuwa mwenyekiti wa tatu wa CHADEMA, hivyo kuwa na mamlaka zaidi ya kuleta mabadiliko katika chama. Wanasiasa vijana kama Shaibu Akwilombe, Antony Komu na Msafiri Mtemelwa (aliyekuwa Mwenyekiti wa Taifa wa Vijana wa NCCR-Mageuzi) walijiunga na CHADEMA.

Wanasiasa wanataaluma kama Mwesiga Baregu nao pia walijiunga na CHADEMA kipindi hiki. Kuna kipindi tulikuwa tunajiita ‘Real Madrid' maana tulikusanya ‘mastaa' wote kutoka vyama vya upinzani.

Chama, kwa kupitia misingi yake, kiliwapa wanachama hawa nafasi kubwa sana ya kuchangia kwa mawazo katika kuimarisha chama na Mbowe alijitahidi sana kutoa fursa hii kwa kila mwanachama aliye tafuta nafasi ya kuchangia.

Hata Mbunge wa sasa wa Mtera, Livingstone Lusinde, alijiunga na CHADEMA kipindi hiki. Freeman Mbowe aliifanya kazi hii ili kutoa fursa kwa Watanzania wengine kujenga chama imara cha siasa nchini ili si tu kuimarisha demokrasia nchini bali pia kutoa mbadala kwa chama tawala na hata vyama vingine vya upinzani. Utekelezaji wa msingi huu wa chama umelipa. Haikuwa kazi rahisi, bali ni kazi makini yenye ujasiri wa kuepuka kujifanya Mbowe ndiye chama na badala yake kujenga chama taasisi ambapo wanachama wanaweza kusema demokrasia ndiyo CHADEMA.

Chini ya uongozi wake, Mbowe ameshirikiana na viongozi wenzake kupandisha chama kutoka chama cha tano mwaka 2000 mpaka chama cha pili mwaka 2010. Miongoni mwa Watanzania waliopata fursa ya kuchangia mabadiliko katika nchi kupitia juhudi hizi za Mbowe ni pamoja na mwandishi wa makala hii na makumi ya wabunge katika Bunge la Kumi, mamia ya madiwani walio katika halmashauri mbalimbali nchini na maelfu ya viongozi katika serikali za vijiji sehemu mbalibali nchini. Sisi kama wanachama tulipewa nafasi nzuri ya kukichangia chama kwa mawazo mbalimbali, na ni umoja wa mawazo yetu yote, matendo yetu sote, kila mmoja kwa nafasi yake, kwa uwezo wake, ndio ulisaidia chama kwenda mbele.

Wakati huo, na hadi leo, vyama mbalimbali vilionekana kuwazuia wanachama wao kutoa maoni huru kuhusu uendeshaji wa chama au hata uendeshaji wa taifa. CHADEMA kilikubalika kama chama chenye demokrasia, na haki za kila mwanachama ziliheshimika. Haki ya kupendekeza maoni binafsi na kuyatetea hadi mwisho ni haki ya msingi inayochangia katika kutofautisha CHADEMA na vyama vingi nchini.

Pamoja na kwamba haki hizi zipo katika misingi ya asili ya CHADEMA, ni haki ambazo ziliimarishwa zaidi katika kipindi cha Mwenyekiti wa tatu wa CHADEMA, Mbowe. Hii ndiyo misingi ambayo kila mwanachama wa CHADEMA anapaswa kujivunia na kuiendeleza ili kuendelea kutoa fursa kwa Watanzania kujenga upya nchi yao kupitia CHADEMA.

Iwapo Mbowe angeendekeza ufuasi wa watu au angetumia nafasi yake kama mwenyekiti kuwashawishi wanachama wawe na ufuasi wa watu, angepofuka na kamwe asingeweza kufikia mafanikio makubwa na ya kutiliwa mifano kama haya ya kujenga asasi imara ya chama cha siasa. Mifano dhahiri ipo kwenye vyama fulani fulani hapa nchini ambapo vyama vilipoanza tu kuwa ‘chama mtu' badala ya ‘chama asasi' vilianza kuporomoka mporomoko usiozuilika.

Dhumuni mojawapo la kisiasa la CHADEMA, kwa mujibu wa katiba yake ni kuendeleza na kudumisha demokrasia katika mfumo wa vyama vingi vya siasa, kujenga utamaduni wa demokrasia katika jamii kwa kutambua haki za wengi katika maamuzi na pia kutambua haki za wachache kusikilizwa, kuheshimiwa na kulindwa, sambamba na kukubali ushindani huru, wa haki na wa wazi katika uchaguzi.

Dhumuni hili ni ushahidi tosha wa nia ya CHADEMA kujenga taifa la kidemokrasia lenye uvumilivu wa kisiasa na kurutubisha mawazo tofauti. Msingi huu na msingi wa ‘fursa' imekuwa nguzo kubwa sana iliyoifikisha CHADEMA katika mwelekeo usiosimama wa kilele cha mafanikio ya chama cha siasa, kushika dola kufanya mabadiliko makubwa yenye maendeleo kwa wananchi wa Tanzania. CHADEMA, kama chama kinachopendekeza misingi hii kinajivunia pia kua mstari wa mbele katika vyama vinavyoendeshwa kwa kuheshimu misingi hii.

Utekelezaji wa dhumuni na misingi hii na misingi iliyoelezwa katika makala zilizotangulia (kuhakikisha rasilimali za nchi zinawafaa wananchi, kupinga ufisadi) unahitaji uumini wa misingi na si uumini wa watu. Ujasiri wa kuamini misingi ya chama na kuitekeleza kwa vitendo kama alivyofanya Freeman Mbowe ni ujasiri wa kuigwa na mwana demokrasia yeyote mwenye uzalendo, umakini, uadilifu na utu kwa Tanzania.

Chama kilichojaa ufuasi wa watu kitapasuliwa na nyufa za uongo, fitna, chuki, majungu na kujipendekeza. Chama cha misingi ndiyo chama tunachopaswa kujenga na kujivunia nacho.

Ni ujasiri wa kufuata misingi ndiyo unaweza kumfanya kiongozi mwenye timu iliyojaa watu wenye vipawa mbalimbali na uwezo mkubwa wa kuvutia ‘wafuasi' kama CHADEMA kuweza kumudu jahazi na kuliendesha vema. Freeman Mbowe ameuweza mtihani huu mpaka sasa na kuendelea kufaulu mtihani huu ni moja ya silaha kubwa kwa CHADEMA katika juhudi zake za kuchukua uongozi wa taifa letu.

Misukosuko ya hapa na pale, inayosababishwa na wafuasi wa watu badala ya wafuasi wa misingi ya chama, haitakwisha. Hata hivyo, kipimo cha uwezo wa uongozi ni namna kiongozi anavyoshughulikia misukosuko. Ufuasi wa misingi ya chama ndio dawa ya kukabili misukosuko. Ufuasi wa watu ni sumu ya kukimaliza chama.

Makala inayo fuata itazungumzia namna gani CHADEMA ilishinda uchaguzi mdogo wa madiwani na ubunge wa Arumeru kwa kupitia misingi ya chama.

Makala hii ni sehem ya tatu juu ya sita (3 out of 6) ya series za "fuata misingi sio watu"

Link to sehem ya kwanza : Kutetea rasilimali za nchi (Inayomuongelea Ndugu Halima Mdee) (1 out of 6)
Link to sehem ya pili: Vita dhidi ya Ufisadi (Inayomuongelea Dk Slaa)(2 out of 6)

**********************
Hiyo ni makala ya Zitto katika Tanzania daima gazieti la leo tarehe 6,jimapili 2013.....

Mie naona bado Zitto ana kitu moyoni!...ilikuwaje aliutaka Uenyekiti wa CHADEMA ilhali anajua kuwa Mwenyekiti alienae anafaa mno? Kweli mafanikio haya ni ya mwenyekiti tu au ni timu nzima? sasa hapa nai mfuasi wa watu yeye kwa mwenyekiti au?
Mtu unaedhani watu wanaufuasi dhidi yake huoni kama unamuonea tu....? Mbona yeye hakupigi kabisa vijembe?
 
Zitto anamchukia Dr.Slaa? Mbona mwanzoni aliwataja Wenyeviti na Makatibu wao Wakuu kwa kuwasifu lakini kwa CHADEMA ya sasa anamsifu Mbowe pekee.Hajui kuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA,Dr.W.P.Slaa ndiye Mtendaji Mkuu wa chama?

Umeona ee!! wala huwa hajifichi, lakini pia hasemi hasa sababu za msingi za yeye kufanya hivyo! Hivi CCM wanavyomuwinda Dr Slaa na wakafanikiwa kumuua kweli, atalia huyu?!
 
Nina mashaka sana na makala hii, ni kweli Mh. Mbowe amekijenga chama, lakini kwa mtu mkweli na asiye na malice haweze
Kumsahau Dr. Slaa kumhusisha na nguvu ya Chadema iliyopo sasa. Ufuasi wa watu anaongolea Mh. Zito ni pamoja na kumshabikia mtu bila
Sababu za msingi au kutotambua juhudi za mtu bila sababu (kama anavyo onyesha Mh. Zito juu ya Mh. Dr. Slaa). Tutaenda mbele kama
tunaheshimiana wala sio kwa kupuuza juhudi za wazi za wengine kwa kusifia baadhi ili watunge mkono.

Nadhani pumba zitajichuja hata kama zilianza kutoka mashineni kabla ya mchele, na tutafika salama tu.
 
Zitto anamchukia Dr.Slaa? Mbona mwanzoni aliwataja Wenyeviti na Makatibu wao Wakuu kwa kuwasifu lakini kwa CHADEMA ya sasa anamsifu Mbowe pekee.Hajui kuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA,Dr.W.P.Slaa ndiye Mtendaji Mkuu wa chama?
jamani hizi makali zitaendelea kila jumapili,hebu subirini,mwachine raisi mtarajiwa apumue.
 
Ni vizuri watu mkakumbushwa historia ya CHADEMA ili mnapojadili hoja mjue wapi mlikotoka na mnaelekea wapi!
 
Zitto pia kwa nafasi yake kavuta watu wengi sana Chadema, mie nikiwa mmoja wapo...niliifahamu chadema na kuipenda kupitia kwa Zitto, japo nasikitika kabadilika kijana wangu..
 
Zitto anamchukia Dr.Slaa? Mbona mwanzoni aliwataja Wenyeviti na Makatibu wao Wakuu kwa kuwasifu lakini kwa CHADEMA ya sasa anamsifu Mbowe pekee.Hajui kuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA,Dr.W.P.Slaa ndiye Mtendaji Mkuu wa chama?
ZZK anakipenda zaidi chama kuliko watu!, angemchukia Dr, saa hizi, Dr na kibaraka wake, wangekuwa wapi kwa njama za kupanga mauaji kupitia sumu ya panya?!. ZZK kupitia "sixth sense" iling'amua mpango huo, akakwepa katakata kukutana na huyo kibaraka!. ZZK as "bright as he is!", angeweza kukubali kukutana na huyo "assasin" na kujiavail himself ili ile sumu iwekwe, then angeondoka na sample!, unadhani madhalimu hao wangekuwa wapi?!.

Sikatai kuwa Dr amefanya and still anafanya kazi kubwa sana na nzuri ndani ya Chadema kuongoza M4C, ila Dr naye ni binadamu na sio malaika hivyo "he can make mistakes", tatizo ninaloliona hapo ni kwa baadhi ya watu kuabudu watu wakidhania watu fulani ni malaika!. Kembe no, ZZK haabudu watu ila "he is a human being", kosa lake kubwa ni kuwa "too frank!" na "too straight!", hakubalali kupelekwa pelekwa tuu kama "ling'ombe" hata kufanya kile asichokiamini!.

ZZK is a fighter anaeamini katika "head on collision" by "taking the bull by its horns" kwa kupambana naye face to face, and "not by the tail" kwa kuzunguka zunguka, na kupambana kwa kususa, kugoma, kutoka nje na kujidai hawamtambui JK! but at the end of the day, ni "Chai Ikulu", hawezi kutamka wazi kuwa "sometimes Chadema are wrong!" ila vitendo na kauli zitawajulisha wenzeke kuwa hakubaliani nao!, japo kisiasa ni kosa kwenda against "collective responsibilities" but you better stand alone on the right track kuliko kuswagewa kwenye collective resiponsibility na kuishia kuizamisha meli yote!.

I still stand with ZZK no matter what "that's what friends are there for!"
Pasco.
 
Nina mashaka sana na makala hii, ni kweli Mh. Mbowe amekijenga chama, lakini kwa mtu mkweli na asiye na malice haweze
Kumsahau Dr. Slaa kumhusisha na nguvu ya Chadema iliyopo sasa. Ufuasi wa watu anaongolea Mh. Zito ni pamoja na kumshabikia mtu bila
Sababu za msingi au kutotambua juhudi za mtu bila sababu (kama anavyo onyesha Mh. Zito juu ya Mh. Dr. Slaa). Tutaenda mbele kama
tunaheshimiana wala sio kwa kupuuza juhudi za wazi za wengine kwa kusifia baadhi ili watunge mkono.

Nadhani pumba zitajichuja hata kama zilianza kutoka mashineni kabla ya mchele, na tutafika salama tu.

ninachokiaona hapa ni kwa baadhi yetu hasa wana chadema kuwa washabiki wa watu na si falsafa na itikadiya chama kama zitto anavyosema. na ni ukweli usiopingika kuwa chadema kimesheheni viongozi nguli na wenye maono;mbowe, slaa, zitto, mnyika, Dr.kitine, prof. baregu, mdee kwa uchache. wote hawa ni viongozi muhimu ndani ya chadema. kwa hiyo basi mtu anapoelezea wasifu wa kiongozi na mchango wake katika chama si lazima amtaje yule ambaye wewe na mimi tunawataka hata kama kazi yake ni kubwa kuliko aliyesiyetajwa (slaa). ninajojiuliza ni kwa nini kila viongozi wa chadema wanappotajwa bila Dr. slaa kuwepo inakuwa ni kosa. tuache chuki dhidi ya watu zaidi sana mtu kwani zitto mwenyewe aliwahi kukaririwa kabla ya uchaguzi wa mwaka 2010 kuwa anamkubali Dr. slaa na Ahmad Rashid na angekuwa tayari kumpigia debe mmoja kati ya yao kama angeteuliwa kugomea urais. hivyo sioni ni wapi zitto anamtazamo hasi na dr. slaa kama katibu mkuu wa chadema. sisi tumekuwa na watu wetu kwenye chama ambao wakati wote tunataka watajwe kila inapopatikana fursa na hii haijengi afya ya chama chenye mshikamano.
 
CDM humu jf, daima hamtaki kujadili jambo muda wote mnamjadili mtu. nimesoma maelezo hayo marefu yanayomfaa kila mpenda siasa wa nchi hii, yanajieleza wazi chama chenu hoi mpaka hai, ilikuwaje hoi mpaka kikawa hai. kulikuwa na vyama vingine hai na sasa viko hoi, sababu ya kuwa hoi nini? jibu lipo wazi SIASA za WATU. ZZK anatoa sifa kwa mwenyekiti wake kwa kusimamia vyema taasisi yake na kuifanya kuwa hai yenye sura ya CHAMA WANACHAMA haikuwa rahisi kukifikisha hapo amepitia misukosuko mingi na anahitaji kuungwa mkono na kusonga mbele kuimarisha CHAMA WANACHAMA si CHAMA MTU kwani sasa kuna wanachama wanataka kuirudisha nyuma taasisi hii kwa kuleta siasa za watu ambazo ni hatari kwa ustawi wa chama mifano ni mingi hapa kwetu MH AUGUSTINO LYATONGA MREMA alikuwa kiongozi wa siasa za mtu, akiamini/wakiamini bila yy hakuna chama mwishowe vyama vyote alivyopitia viko hoi. mh LIPUMBA nao CUF mawazo yao yako hivyohivyo bila yy hakuna URAIS , hawataki majadiliano ni amri. mwisho sasa CUF iko hoi. CDM mmeasisiwa vzr saana na hm MBOWE mkiwa taasisi kubwa na bora yenye wafuasi wengi mithili ya CCM. MMETOKA MKIWA CDM WANACHAMA mkiamini nguvu ya pamoja lkn sasa mnaamini nguvu ya mtu hamtaki teena majadiliano ,mmejaa dhihaka mkipuuza umoja wenu alioujenga mh MBOWE mnaanza kulewa na kufuata njia ya MH LIPUMBA na LYATONGA kuelekea chama hoi
 
Naona na wewe mambo ya sumu unayajua kiundani zaidi

hahahahahahahahahaha

ZZK anakipenda zaidi chama kuliko watu!, angemchukia Dr, saa hizi, Dr na kibaraka wake, wangekuwa wapi kwa njama za kupanga mauaji kupitia sumu ya panya?!. ZZK kupitia "sixth sense" iling'amua mpango huo, akakwepa katakata kukutana na huyo kibaraka!. ZZK as "bright as he is!", angeweza kukubali kukutana na huyo "assasin" na kujiavail himself ili ile sumu iwekwe, then angeondoka na sample!, unadhani madhalimu hao wangekuwa wapi?!.

Sikatai kuwa Dr amefanya and still anafanya kazi kubwa sana na nzuri ndani ya Chadema kuongoza M4C, ila Dr naye ni binadamu na sio malaika hivyo "he can make mistakes", tatizo ninaloliona hapo ni kwa baadhi ya watu kuabudu watu wakidhania watu fulani ni malaika!. Kembe no, ZZK haabudu watu ila "he is a human being", kosa lake kubwa ni kuwa "too frank!" na "too straight!", hakubalali kupelekwa pelekwa tuu kama "ling'ombe" hata kufanya kile asichokiamini!.

ZZK is a fighter anaeamini katika "head on collision" by "taking the bull by its horns" kwa kupambana naye face to face, and "not by the tail" kwa kuzunguka zunguka, na kupambana kwa kususa, kugoma, kutoka nje na kujidai hawamtambui JK! but at the end of the day, ni "Chai Ikulu", hawezi kutamka wazi kuwa "sometimes Chadema are wrong!" ila vitendo na kauli zitawajulisha wenzeke kuwa hakubaliani nao!, japo kisiasa ni kosa kwenda against "collective responsibilities" but you better stand alone on the right track kuliko kuswagewa kwenye collective resiponsibility na kuishia kuizamisha meli yote!.

I still stand with ZZK no matter what "that's what friends are there for!"
Pasco.
 
Hata asifu chama kizima sito nasa kwenye mtego huu!
 
ninachokiaona hapa
ni kwa baadhi yetu hasa wana chadema kuwa washabiki wa watu na si
falsafa na itikadiya chama kama zitto anavyosema. na ni ukweli
usiopingika kuwa chadema kimesheheni viongozi nguli na wenye
maono;mbowe, slaa, zitto, mnyika, Dr.kitine, prof. baregu, mdee kwa
uchache. wote hawa ni viongozi muhimu ndani ya chadema. kwa hiyo basi
mtu anapoelezea wasifu wa kiongozi na mchango wake katika chama si
lazima amtaje yule ambaye wewe na mimi tunawataka hata kama kazi yake
ni kubwa kuliko aliyesiyetajwa (slaa). ninajojiuliza ni kwa nini kila
viongozi wa chadema wanappotajwa bila Dr. slaa kuwepo inakuwa ni kosa.
tuache chuki dhidi ya watu zaidi sana mtu kwani zitto mwenyewe aliwahi
kukaririwa kabla ya uchaguzi wa mwaka 2010 kuwa anamkubali Dr. slaa na
Ahmad Rashid na angekuwa tayari kumpigia debe mmoja kati ya yao kama
angeteuliwa kugomea urais. hivyo sioni ni wapi zitto anamtazamo hasi na
dr. slaa kama katibu mkuu wa chadema. sisi tumekuwa na watu wetu kwenye
chama ambao wakati wote tunataka watajwe kila inapopatikana fursa na
hii haijengi afya ya chama chenye mshikamano.

Tunapo elekea nikuanza kuulizana na mwenye kuimiliki CHADEMA .Nadiriki kusema hivyo kwani inaonekana wazi kila mtu anataka umaaharufu na kutambuliwa zaida kuliko chama.
We have to be free from this mase CDM.
 
ZZK anakipenda zaidi chama kuliko watu!, angemchukia Dr, saa hizi, Dr na kibaraka wake, wangekuwa wapi kwa njama za kupanga mauaji kupitia sumu ya panya?!. ZZK kupitia "sixth sense" iling'amua mpango huo, akakwepa katakata kukutana na huyo kibaraka!. ZZK as "bright as he is!", angeweza kukubali kukutana na huyo "assasin" na kujiavail himself ili ile sumu iwekwe, then angeondoka na sample!, unadhani madhalimu hao wangekuwa wapi?!.

Sikatai kuwa Dr amefanya and still anafanya kazi kubwa sana na nzuri ndani ya Chadema kuongoza M4C, ila Dr naye ni binadamu na sio malaika hivyo "he can make mistakes", tatizo ninaloliona hapo ni kwa baadhi ya watu kuabudu watu wakidhania watu fulani ni malaika!. Kembe no, ZZK haabudu watu ila "he is a human being", kosa lake kubwa ni kuwa "too frank!" na "too straight!", hakubalali kupelekwa pelekwa tuu kama "ling'ombe" hata kufanya kile asichokiamini!.

ZZK is a fighter anaeamini katika "head on collision" by "taking the bull by its horns" kwa kupambana naye face to face, and "not by the tail" kwa kuzunguka zunguka, na kupambana kwa kususa, kugoma, kutoka nje na kujidai hawamtambui JK! but at the end of the day, ni "Chai Ikulu", hawezi kutamka wazi kuwa "sometimes Chadema are wrong!" ila vitendo na kauli zitawajulisha wenzeke kuwa hakubaliani nao!, japo kisiasa ni kosa kwenda against "collective responsibilities" but you better stand alone on the right track kuliko kuswagewa kwenye collective resiponsibility na kuishia kuizamisha meli yote!.

I still stand with ZZK no matter what "that's what friends are there for!"
Pasco.

Nawe umekuwa mpambe siku hizi?
 
Hyu ZZZK ni mnafiki hana lolote hata anapokuja hapa nje huwa tunamsikiliza anavyoongea ila kwa kufanya uchunguzi wa maneno yake utajua anakinyongo fulani. Cha msingi Mboye, Dr Slaa, Nyerere, Mnyika, Lema, Milya na wengine wengi ni majembe yakutosha hatumuhitaji yeye. Hapa nje sisi tunajipanga nakuona ni jinsi gani tunaweza kukisaidia chama hasa wakati wa uchaguzi. Wenzangu wote mlioko nje ya nchi mtakubaliana na mimi kwamba tukishikimana kwa kukisaidia chama tutashinda. Ee Mungu tusaidie.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom