Lady Whistledown
JF-Expert Member
- Aug 2, 2021
- 1,183
- 2,100
Akionekana kutofurahia baadhi ya kauli, picha na maandiko mbalimbali mitandaoni, kwenye kile alichokiita kama Makelele ya mwenye siasa na yenye kuwahusu wanawake wanasiasa, Mwanasiasa Zitto Kabwe ambaye pia ni mtia nia ya Ubunge kupitia ACT Wazalendo kwenye uchaguzi Mkuu wa 2025, ametuma Ujumbe mtandaoni, akitahadharisha kuepuka kufanya mambo kwa kuzungumza ama kuandika ambayo yanaweza kutafsiriwa kama Udhalilishaji kwa wanawake.
Amesisitiza kywa hata ikiwa ipo tofauti yoyote miongoni mwao, ni muhimu kuutunza utu wao na kufanya mambo, ikiwemo mizaha, ukosoaji na kadhalika kwa kutanguliza mbele heshima akisisitiza kuwa wanawake kwenye siasa wanahitaji kulindwa na kuthaminiwa.
"(...) Nakusihi kutofanya mambo ikatafsirika unadhalilisha wanawake. Political banters are good but ni muhimu sana kufanya kwa namna ambayo unalinda heshima ya wanawake. Wanawake kwenye siasa wanahitaji kulindwa na kuthaminiwa UTU wao. Tusitweze utu wao kwa sababu ya tofauti zetu." Ameandika Zitto akimjibu mtumiaji wa Mtandao wa X.
Kwa siku za hivi karibuni kumekuwa na maneno na machapisho kadhaa mtandaoni yenye kuambatana na lugha mbalimbali ambazo zimekuwa zikionekana kuwakera wanawake ambao wamekuwa miongoni mwa mamia ya wanachama wa Chadema ambao wamekuwa wakitangaza kuondoka ndani ya Chama hicho, huku wanawame hao wakidai kutukanwa, kudhalilishwa na kuvunjiwa heshima mitandaoni.
Chanzo: Jambo Tv