GE2025 Mafunzo yatolewwa kulinda wanasiasa wanawake Mtandaoni

GE2025 Mafunzo yatolewwa kulinda wanasiasa wanawake Mtandaoni

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,116
Reaction score
3,496
Taasisi ya Pollicy Data Institute Agosti 15, 2025 imeendesha mafunzo kwa waandishi wa habari nchini Tanzania, yakilenga mbinu za kuandika habari zisizowabagua wanawake, hasa wale wanaojihusisha na siasa. Mafunzo haya ni sehemu ya mradi wa kimataifa unaoitwa Vote Women, unaolenga kuongeza ushiriki wa wanawake katika uongozi na siasa

Kwa mujibu wa Brenda Namata, Meneja wa Programu wa Pollicy Data Institute, mradi wa Vote Women ulianzishwa mwaka 2021 na ulitekelezwa pia nchini Kenya wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2022. Mradi huo uliwasaidia wanawake waliogombea nafasi mbalimbali kukabiliana na changamoto, hususan zile zinazotokana na ubaguzi wa kijinsia

Programu hii ambayo sasa imeanza rasmi Tanzania inawaleta pamoja wanawake waliowahi kugombea nafasi za kisiasa ili kujadiliana, kubadilishana uzoefu na kujua namna ya kukabiliana na changamoto zinazowakabili

Miongoni mwa changamoto zilizotajwa ni pamoja na matusi na lugha za kudhalilisha mitandaoni, upotoshaji wa taarifa na mashambulizi ya kisaikolojia. Mafunzo haya pia yanawapa elimu ya afya ya akili ili kuwasaidia wanawake hao kukabiliana na msongo wa mawazo unaotokana na mashambulizi hayo

Aidha, mafunzo haya yameendeshwa na wataalamu mbalimbali wakiwemo Bonnita Pyamwire, Mkurugenzi wa Utafiti wa Policy Data Institute, na Farati H. Fomily, mkufunzi wa mradi huo


 
Ukitaka kumuua mbwa mpe jina baya. Ukitaka kubadili jambo na kureplace na kitu kipya then hilo jambo lifanye kuonekana ni baya.

Wanawake kwenye mitandao wakati wa siasa hawapitii ubaguzi wa kijinsia, wanachopitia kinaitwa mchujo au initiation ya kisiasa.

Wanaume wapya pia katika siasa wanapitia hali kama hii kwa sura nyingine mfano watahoji elimu yake,hostoria yake,au mtu atasema jambo la kumshushia hadhi huyo mgombea na kadhalika.

Wanawake sio special case kwenye siasa. Wanachoexpect ni urahisi ule ule wa freeloader kwenye mahusiano waende nao popote wanapokwenda huku wakijipatia maslahi yao sawa na wanaume ambao hawalalamiki wala kudeka.

Unapoingia vita kwenye uwanja wa tope expect kuchafuka kwa tope mwili mzima na sio kulalamika kuwa unachafuliwa sasa wewe ulikuja kufanya nini hapo matopeni.

Siasa za siku hizi ni za maji taka, kuchafuana ni kawaida. Watu watatafuta kitu chochote cha kusema au kuonyesha dhidi yako ili tu kudhihirisha na kukupima kama unaweza kuwa imara kama unavyosema.

Sasa wanawake kupenda utelezi wanaenda kwa mabwana zao ulaya na kuomba kuwekewa special privileges ili wasipate changamoto za kawaida kabisa kwenye siasa. Komaeni ili sasa muone maana halisi ya uongozi sio kuwa vigeugeu.

Kama hamuwezi it means mlivamia kitu kisichowahusu. Na kila siku hapa tunakataza wanawake kupewa nafasi kubwa za uongozi sababu ya poor handling ya situations na pia uwezo mdogo wa kuchambua mambo kwa muktadha na faida ya jamii kwa ujumla.
 
Back
Top Bottom