Zitto: Tutairejesha Meremeta bungeni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zitto: Tutairejesha Meremeta bungeni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Mar 22, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Mar 22, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  MJADALA kuhusu hatma ya kampuni ya Meremeta iliyokuwa inamilikiwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) sasa utarejeshwa tena bungeni katika kikao cha Bunge linaloanza Aprili mwaka huu mara baada ya Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali kukamilisha uhakiki wa hesabu za matumizi ya kampuni hiyo.

  Maelekezo ya Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Zitto Kabwe, yamethibitisha hivyo.

  Meremeta ni moja ya makampuni yaliyotuhumiwa na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willbrod Slaa, kwamba yalifanya wizi mkubwa wa fedha za umma lakini Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, katika Bunge lililopita alizima mjadala juu ya suala hilo akidai kuwa hiyo ilikuwa ni kampuni ya jeshi na kwamba masuala yanayogusa usalama wa nchi hayawezi kujadiliwa hadharani.

  Hata hivyo, Pinda alionekana dhahiri kuwa alikuwa akificha ukweli.

  Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), Zitto Kabwe (CHADEMA), alisema kamati yake imeitaka ofisi ya Msajili Hazina kuhakikisha inatoa ushirikiano kwa CAG ili kukamilisha utarabu wa kufanya hesabu maalum kwa kampuni hiyo kwa haraka.

  Alisema kamati yake ilitoa maagizo kwa CAG kufanya kazi ya ukaguzi lakini kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa katika taarifa yake Msajili Hazina hajatoa ushirikiano wala majibu juu ya hatua hiyo.

  Kufuatia hali hiyo kamati hiyo imelazimika kutaka maelezo ya kina kwa nini hesabu hizo hazijakalimika kwa mujibu wa sheria.

  “Tunahitaji Bunge la Aprili suala la Meremeta liwe limekwisha na kama serikali haitaki kufanya hivyo kupitia kamati yetu tutawaeleza wananchi nini kinachoendelea, Bunge ni chombo chenye mamlaka ya kuisimamia serikali kwa asilimia mia moja”

  “Tunahitaji mgodi wa Buhemba, wapewe Stamico lakini kwa sasa huwezi ukawakabidhi kitu ambacho hakijafanyiwa uhakiki wa hesabu zake …kwa Meremeta serikali ilikuwa ikimiliki hisa asilimia mia moja,” alisema Zitto.

  Kampuni ya Meremeta, ambayo inadaiwa haijasajiliwa chini ya Ofisi ya Hazina kama kampuni au shirika, ilichota malipo tata zaidi ya sh bilioni 215 zilizolipwa na Benki Kuu (BOT) kwa Kampuni ya Nedcor Trade Service, baada ya udhamini wa kampuni yenye hisa ya Triennex (PTY) limited ya Afrika Kusini.

  Hata hivyo, alisema kamati hiyo inahitaji kufahamu hatma ya uuzwaji wa hisa za kampuni ya Zain kwenda kampuni ya simu ya Airtel.

  Alisema kwa mujibu wa maelezo inaonyesha kuwa kuuzwa kwa kampuni hiyo serikali haijanufaika kupata kodi na kuhitaji maelezo ya kina ya Msajili wa Hazina, Kamishna wa TRA.

  “Hisa za Zain zimeuzwa lakini hakuna kodi iliyongia serikalini sasa tunahitaji kupata ufafanuzi wa kina juu ya hali hii kwani ili nchi iweze kujiendesha sio kufanya ujanja; kinachotakiwa Airtel ni kulipa kodi tu,” alisema Zitto.

  Alisema katika kuhakikisha wanasimamia hilo kamati yake imeazimia siku ya Ijumaa kukutana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Ramadhan Kijah, Kamishna Mkuu wa TRA, Hanry Kitilya, na Msajili Hazina.
   
 2. M

  Mutu JF-Expert Member

  #2
  Mar 22, 2011
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  mhhhhhhhhhhhh
   
 3. Gwota

  Gwota JF-Expert Member

  #3
  Mar 22, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 205
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Tuendelee kumuombea kwa mungu kijana wetu zitto arudishe makali yake.
   
 4. M

  Marytina JF-Expert Member

  #4
  Mar 22, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,035
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  simuamin zitto nasikilizia akiweza hili nitarejesha imani kwake
   
 5. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #5
  Mar 22, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Duh? Yaani serikali haijapata kodi ya mapato kwenye mauzo ya Zain na JK ndiye aliyekwenda kuzindua Airtel!? Haya si ndio yale mambo ya kuzindua hotel hapa Ar kumbe fence yake ipo kwenye hifadhi ya barabara? Mr President is acting photogenic by just enjoying to lounch taasis hata za wavunja sheria! My God!? What a President!
   
 6. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #6
  Mar 22, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  Tusubiri tuone.. lakini mimi nimeshapoteza imani na Zitto!
   
 7. Juaangavu

  Juaangavu JF-Expert Member

  #7
  Mar 22, 2011
  Joined: Nov 3, 2009
  Messages: 916
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  "Tunahitaji mgodi wa Buhemba wapewe Stamico lakini kwa sasa huwezi ukawakabidhi kitu ambacho hakijafanyiwa uhakiki wa hesabu zake" Eeh! Kwanini Stamico! Je ni jukumu la kamati kuamua ktk hili? Na ni kwa kiasi gani?
   
 8. Naloli

  Naloli JF-Expert Member

  #8
  Mar 22, 2011
  Joined: Aug 26, 2010
  Messages: 416
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Tusubiri na kuona hiyo APRIL, muda wa kupeana matumaini umekwisha tunaitaji vitendo.
   
 9. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #9
  Mar 22, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Zitto zubery sina imani na wewe,ilishanitoka kitambo ila namna ulivozungumza nimefurahi sana kama kweli mtafanya hivo na ukakomaa mwanzo mwisho ntarudisha imani kwako. nilikuwa nakukubali lkn ulivoanza ukinyonga flani siku za kati hapa nilikuwa nafaidhaishwa sana. nakuombea ktk hili. go! go! plz
   
 10. wazolawiki

  wazolawiki New Member

  #10
  Mar 22, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Zito! Sijui. Ngoja tuone:hand:
   
 11. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #11
  Mar 22, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,903
  Likes Received: 5,364
  Trophy Points: 280
  simuamini zitto,..nahisi kama kuna mchezo na ccm wanaupanga ili kwenda kuisafisha hiyo kashfa ili aonekane dr slaa alikurupuka kusema kuna ufisadi meremeta,..nahisi mwisho mbaya kwa hili.zitto uh huh sina imani naye,..something fishy is smelling
   
 12. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #12
  Mar 22, 2011
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,180
  Likes Received: 1,182
  Trophy Points: 280
  Mmh! Huyu kabwe zito ALIYE BEMENDWA NA NA CCM? siyo rahis kuzaliwa upya, labda kuna ki2 nyumaye, binafsi sina iman naye tena!
   
 13. m

  mzambia JF-Expert Member

  #13
  Mar 22, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 885
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Kwani huyo si mkwere jamani mlitaka afanye nini na zitto anajikomba kwa mkwere si ulisikia kuwa alimwangukia ili ampe uenyekiti wa hiyo kamati? Hiyo, ni janja ya nyani kula nyama mbichi tu hakuna kitu hapo.
   
 14. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #14
  Mar 22, 2011
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Let's be fair
   
 15. Mshindo

  Mshindo JF-Expert Member

  #15
  Mar 22, 2011
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 479
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Aaah mie sio kijana wangu huyu,period! kama litakua na manufaa kwa taifa basi itakua ni kwa chance au mistake....Haswa haswa Mistake,..yes...bahati mbaya yaani! Kwamba ishu libumbuluke hukoo mara beneficiaries ndo tuwe sie! But if all goes well...Let's wait and see!
   
 16. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #16
  Mar 22, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,499
  Likes Received: 5,728
  Trophy Points: 280
  Zitto achen usanii
  ungekuwa nyu kwenye kamati nisngepiga kelele...nyie kaen kimya msitafute umaarufu kama mmeushindwa hottym watu wanataaka ukweli sasa wala atuuitaji tena mkahongane
   
 17. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #17
  Mar 22, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,499
  Likes Received: 5,728
  Trophy Points: 280
  Kama uko sirias na meremeta kamuulize mboma..akupe siri yake@@@na ule kile kiwanja anapoishi mbezi beach
   
 18. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #18
  Mar 22, 2011
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  meremeta ya nini bana....!

  nendeni mkajadili maswala yenye tija kwa maslahi ya taifa kwa ujumla wake!meremeta iliweza kuvuka kigingi kikubwa cha riport ya mwanakijiji MTAWEZA NINYI?

  jadilini
  -inflations
  -namna ya kuboresha viwango vya elimu
  -namna ya kuboresha miundo mbinu
  -namna ya kuboresha huduma za jamii kama maji,umeme,hospitali n.k
  -namna ya kuboresha maisha ya mpiga kura
   
 19. p

  plawala JF-Expert Member

  #19
  Mar 22, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 627
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Meremeta?Kama imeibuka safari hii lazima tuwe na dought,nakumbuka Pinda alishawahi kusema kwamba hatakubali meremeta ichunguzwe kwa sababu ni kampuni iliyokuwa inamilikiwa na jeshi
  Sasa kitu gani kimebadilika?Kama ni kwa wema twashukuru,lakini tusubiri muda uje
   
 20. F

  FUSO JF-Expert Member

  #20
  Mar 22, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,866
  Likes Received: 2,340
  Trophy Points: 280
  Itarudishwa bungeni may be 2015 wakati mama Anna na Pinda wameshaondoka. Napendekeza hiyo irudishwe wa wananchi kuliko kuipeleka kwenye bunge la CCM ambapo ni kama kupoteza muda. Walishasema hiyo haitakaa ijadiliwe au Zitto ameamua kutufurahisha?
   
Loading...