Zitto: Tunapata maduhuli na si "gawio"

Zitto: Tunapata maduhuli na si "gawio"

Zitto

Former MP Kigoma Urban
Joined
Mar 2, 2007
Posts
1,562
Reaction score
10,890
Na Zitto Kabwe

Kwamba Mashirika ya umma nchini yanamkabidhi Rais cheki za magawio (dividends) ya faida zao ni ama Ofisi ya Rais inafanya Siasa au hawajui maana ya gawio.

Tukiwa Bunge la 9, Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma (POAC na baadaye PAC) ililishauri Bunge kufanya marekebisho ya Sheria ya baadhi ya mashirika ya umma Ili kiwango fulani cha Mapato ghafi (turnover) kitolewe Serikalini kama maduhuli ya Serikali.

Serikali ya wakati huo ilikubali na Sheria zikabadilishwa na kutenga 15% ya Mapato ghafi ya Taasisi za Umma kuwa Mapato ya Serikali kuingia Mfuko Mkuu wa Hazina. SIO FAIDA maana mashirika haya mengi hayana faida. Faida ya TCRA ni nini? Ama EWURA? Ama TANROADS?

Kusema Rais anakabidhiwa gawio la faida ya mashirika ya umma ni ulaghai ambao hauna maana yeyote, kwani Taarifa za Ukaguzi za Mashirika hayo zitaonyesha kuwa hakuna faida (na hivyo hakuna gawio), na hivyo kuumbuka kwa Serikali yenyewe.

Kinachotolewa ni nini? Haya ni maduhuli tu, ama ni kodi maalumu ambayo imewekwa kwa mashirika kwa kiwango cha 15% ya Mapato ghafi. Maduhuli au kodi hii imekuwa ikilipwa miaka yote ya nyuma. Sielewi ni kwanini sasa Rais amewaleta mbele wakuu wa mashirika Eti kutoa gawio! Gharama za kuwaleta hao wakuu wa hizi taasisi hazikupaswa kuingiwa kabisa, kwani kodi hizo hukatwa moja kwa moja kuingia Mfuko Mkuu wa Serikali. Sielewi hizi hadaa ni za Nini?

Ni muhimu pia kueleza kuwa kuna hoja ya Ukaguzi ya CAG kuhusu makato haya kwa baadhi ya taasisi. Kwamba makato haya yanapaswa kuwa ‘Tax deductibles’ - yaani wakati wa kukokotoa kodi ya Mapato ya baadhi ya Mashirika malipo haya yanapaswa kuondolewa kwanza.

Hata hivyo TRA wamekuwa hawafanyi hivi na hivyo kukuta mashirika kama TANAPA, NCAA, TPA nk yanalipa Fedha zaidi ya yanavyopaswa kulipa na kusababisha shughuli zao za msingi kushindwa kutekelezwa.

Watanzania msihadaiwe leo, hatupokei gawio, bali tunapokea maduhuli tu.

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama, ACT Wazalendo
Julai 23, 2018.
 
Asante Zito Barbarosa mwengeso YEHODAYA MISULI
 
Zito utakula risasi sasa hivi....Mwenzio hataki hiivyo....anataka akisema gawio wote tuseme gawio....Kwa Lisu ilikuwa hivihivi, jamaa anataka aonekane anapiga kazi na kukusanya faida...ukimwambia ukweli tu risasi zinakuhusu....

Cha msingi we achana nae, akusanye gawio akusanye maduluhu atajua mwenyewe sisi hayatuhusu, Maana hata hela zenyewe ndo kwanza anatumia kujengea mahekalu huko chato na kununua mijidege ambayo haina faida.
 
Sasa mbona kuna mengine hayajatoa hayo masuhuli kama yapo kisheria...Kwa hiyo hayana chochote cha kutoa?... Zityo hebu fafanua vizuri
 
Kwa hiyo yeye kaona tcra tu sio
 
Sasa kama siyo gawio bali ni maduhuli kwanini ofisi ya Rais imeruhusu hili kufanyika tena kwa mbwembwe nyingi mno? Nani mkweli katika hili, ni Zitto au Rais?

Kama Rais anadanganya, lengo lake ni kumdanganya nani?? Na kama Zitto hayuko sahihi lengo lake ni nini?? Mimi nafikiri tunahitaji ufafanuzi wa kina kuhusu hili jambo.

Cc. Pascal Mayalla
 
Kama ningekuwa rais zitto ningempa nafasi fulani asaidie kuyafanya mawazo yako mengi mazuri ktk utendaji. Zitto why are you always appear to be right? Simaanishi ktk hili tu. Mara nyingi huwa ni kama mtoa mawazo mbadala.
Je hutumiki vizuri ktk bunge na serikali? Hizi gvt organs huwa hawakutani na interest groups kupata insights zao au huwa unasubiri wakosee au unajua lazima watakosea mahali then uwakosoe?
 
Zitto nahisi hakusikiliza vizuri kakimbilia kuandika na kupotosha watu. Imesemwa wazi, kuna walio toa gawio hasa wenye muundo wa kampuni na shareholding structure mf. Kadco. Baada ya hapo ikatangazwa yanakuja mashirika yanayotoa maduhuri mf. Tcra, ewura na wengine. Tofauti imesemwa wazi kwa waliosikiliza na ikatajwa kuwa ni 15% ya mapato kulingana na sheria. Zitto hoja huna tena.
 
Zito utakula risasi sasa hivi....Mwenzio hataki hiivyo....anataka akisema gawio wote tuseme gawio....Kwa Lisu ilikuwa hivihivi, jamaa anataka aonekane anapiga kazi na kukusanya faida...ukimwambia ukweli tu risasi zinakuhusu....

Cha msingi we achana nae, akusanye gawio akusanye maduluhu atajua mwenyewe sisi hayatuhusu, Maana hata hela zenyewe ndo kwanza anatumia kujengea mahekalu huko chato na kununua mijidege ambayo haina faida.
KABISA!!!!!
 
Zitto nahisi hakusikiliza vizuri kakimbilia kuandika na kupotosha watu. Imesemwa wazi, kuna walio toa gawio hasa wenye muundo wa kampuni na shareholding structure mf. Kadco. Baada ya hapo ikatangazwa yanakuja mashirika yanayotoa maduhuri mf. Tcra, ewura na wengine. Tofauti imesemwa wazi kwa waliosikiliza na ikatajwa kuwa ni 15% ya mapato kulingana na sheria. Zitto hoja huna tena.
Zitto yuko sahihi !!!!!!!
 
Back
Top Bottom