Zitto: Sikuondoka CHADEMA bali nilifukuzwa

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,010
9,874
Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo, Zitto Zuberi Kabwe amesema yeye hakuondoka CHADEMA bali alifukuzwa.

Kupitia ukurasa wake wa twitter amesema kuwa alifukuzwa bila kikao cha Halmashauri Kuu, bali ilikuwa barabarani tu.

Amesema anachukulia hilo kama sehemu ya harakati, na hajabeba chuki kwa tukio hilo.

Zitto alihamia ACT-Wazalendo Machi 2015 akitokea CHADEMA ambako walimtuhumu kuwa msaliti.

Zitto.JPG
 
Kweli CHADEMA imebaki na wanaharakati wa kisiasa ni CHADEMA ni kama NGO ya kutafutia ruzuku watu wale maisha yasonge. Lakini mwisho wa jana ni sasa. Bora Mbowe yeye analenga mpunga tu, lakini hii CHADEMA ya Tundu ni asilimia 100% uanaharakati wa kisiasa na inaenda kufa kifo kibaya sana.
 
Kweli Chadema imebaki na wanaharakati wa kisiasa ni Chadema ni kama NGO ya kutafutia ruzuku watu wale maisha yasonge. Lakini mwisho waja na ni sasa. Bora Mbowe yeye analenga mpunga tu, lakini hii Chadema ya TUNDU ni asilimia 100% uanaharakati wa kisiasa na inaenda kufa kifo kibaya sana.
Hivi kwanini wana CCM mnajifanya kuwamaind CDM ?!. Toka lini mkawa na nia njema kwa CDM ?
 
Kweli Chadema imebaki na wanaharakati wa kisiasa ni Chadema ni kama NGO ya kutafutia ruzuku watu wale maisha yasonge. Lakini mwisho waja na ni sasa. Bora Mbowe yeye analenga mpunga tu, lakini hii Chadema ya TUNDU ni asilimia 100% uanaharakati wa kisiasa na inaenda kufa kifo kibaya sana.

Unahangaika sana kaa utulie dawa ikuingie taratibu,Mdee na Genge lake leo wanatupwa nje baada ya kukubali kununuliwa kirahisi.
 
Kweli Chadema imebaki na wanaharakati wa kisiasa ni Chadema ni kama NGO ya kutafutia ruzuku watu wale maisha yasonge. Lakini mwisho waja na ni sasa. Bora Mbowe yeye analenga mpunga tu, lakini hii Chadema ya TUNDU ni asilimia 100% uanaharakati wa kisiasa na inaenda kufa kifo kibaya sana.
Mbona unaongea kama mama mjamzito? Una mimba ya miezi mingapi nikuletee malimao?
 
Naona kamalizia na kauli mbiu ya wananchi.

Daima Mbele Nyuma Mwiko
 
Zitto hakufukuzwa vipi wakati alivunja sheria inayomkataza mwanachama kwenda mahakamani?

Ndio alifukuzwa barabarani kwa sababu alijua kwenda kwake mahakamani kumemuondoa, vinginevyo kama anaona alionewa kwanini asingeenda tena mahakamani kupinga kufukuzwa akiwa barabarani?

Hata hawa kina Mdee na wenzake leo, maamuzi yoyote yakitolewa dhidi yao, halafu wakajipeleka mahakamani, nao watakuwa wamefukuzwa automatically, haijalishi wawe barabarani au bafuni.
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Ndio alifukuzwa, Chadema inatakiwa mbadili kiongozi otherwise hii saccos itapotea . Haiwezekani miaka na miaka mwenyekiti ni mmoja tu. Huu ni udikteta ndani ya chama , na ndo mana wanawake wanawapanda kichwani.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mfukuzeni kwanza mwenyekiti wenu ambae hua anawajibu kwamba itategemea nimeamkaje,mkimalizana nae muwaambie CHADEMA nao wafanye hivyo.
 
Kwani hapo kuna mjadala tena?Yes,alifukuzwa mchana kweupe then anataka nini sasa?Abembelezwe sio?

Yeye ajiandae kuchukua makapi yakina Mdee na wenzake,asianza story za paukwa pakawa,Esopooo.
 
Back
Top Bottom