Zitto: Serikali ya Magufuli wahongwa na mchina ili uzalishaji wa chuma cha Liganga na Mchuchuma usifanye kazi

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Leo nimepata Habari za kustusha sana. Makampuni ya chuma ya China, Urusi na Uturuki yamehonga baadhi ya watendaji wa Serikali ya Awamu ya Tano kuchelewesha Mradi wa Mchuchuma na Liganga mpaka Mradi wa SGR uishe. Lengo ni kuhakikisha nchi hizo zinapata soko la Chuma chao.

Watendaji hao kutoka Wizara ya Fedha, Viwanda na Biashara na Ofisi ya Rais wamekula njama kiasi cha kuwezesha Bunge kutunga sheria kuondoa Kodi zote kwa Mataruma ya Reli yanayoagizwa kutoka nje na kuzuia Mradi wa Mchuchuma na Liganga kupata msamaha wa kodi kuwezesha mradi kuanza

Serikali inaagiza ‘bidhaa’ fulani kutoka kampuni ya ROSOBORONEXPORT kutoka Urusi zenye thamani ya $475m kutoka mkopo wa Benki ya SBERBANK ya huko huko kama sehemu ya mpango Mzima wa hongo za kuzuia nchi yetu isiwe na uwezo wa ndani wa kuzalisha bidhaa za chuma kama Reli

Yote haya yanafanyika chini ya uangalizi wa Rais Rais Maguful kiasi kwamba Rais amelishwa matango pori dhidi ya Mradi muhimu na wa kimkakati kama Mchuchuma na Liganga na yeye Rais anayasema haya matango pori hadharani. Nchi yetu imegeuzwa dampo la kuagiza bidhaa za chuma kihayawani

Mradi wa kuifanya nchi yetu kuwa mzalishaji wa pili wa chuma Afrika na kuweza kujitegemea kwa viwanda vya bidhaa za chuma kama Reli, Mabomba, vipuri, Nondo etc unauwawa kwa maslahi ya wachache. Tena wanasema wameagizwa na namba 1 kutafuta fedha za kampeni 2020.

Kuhujumu Mchuchuma na Liganga ni UHAINI. Baadhi yetu hatutasahau hujuma hii kamwe. Yeyote anayeshiriki atasakwa mpaka kaburini kwake. Ikibidi kuondoa kinga za watu itabidi ziondolewe ili iwe fundisho kwa uhujumu huu wa Uchumi wetu na uhai wa Taifa letu.

Msamaha wa kodi kwa Bomba la Mafuta kutoka Hoima Uganda ni mkubwa na hauna faida kulinganisha na Mradi wa Mchuchuma na Liganga utakaotoa ajira rasmi za kudumu 35,000, kuingiza forex mpaka $4.6bn kwa mwaka na kuifanya nchi yetu kuwa industrial giant. Rais Magufuli hili unahujumu nchi.

Liganga.PNG
 
Zitto ni wachache sana wanaokuelewa, hasa ukizingatia kuwa tayar wengi wetu tuna mahaba ya uvyama na Wala siyo mahaba na nchi.
Ila namshauri rais jpm aikubali hoja yako Kisha akuite ww ikulu uongee naye ana kwa ana kuhusu hao watu. Halafu tuanze kutrac financial records zao. Ikithibitika ni kweli Basi JPM awafunge maisha wote na ayafukuze hayo makampuni kwani yametoa rushwa jambo ambalo no udanganyifu.

Ikiwa kauli hii yako.ni uongo Basi aangize ufungwe milele kwan unaleta taharuki kwa jamii
 
Ndugu Zitto, hao unaowasema ni wafanyikazi wa serekali, wanaweza kuwemo wale civil servant ambao hawahusiani na chama na wale waliochaguliwa na raisi, haimaanishi Raisi magufuli na awamu ya nne ndiyo inayofanya hivyo.

Nina uhakika utakuwa na majina yao, na hutayataja kwa kutaka tuhuma hizi zisimuondoke Magufuli nawe uendelee kupata kiki za kisiasa.

Mara nyingi nimependezwa na jitihada zako na kuziunga mkono hata kukutetea. Lakini kuna wakati wa dharura unajiweka wewe kwanza na Taifa nyuma.

Kama ni tuhuma tuu na huna uhakika nazo, why bring them up, a good politician talk openly on cfrucial matters and detrimental to the state , and one should not look for political milage, ama no yale yale ya Pesa za Switzerland
 
gfsonwin naunga mkono hoja yako kwa 100%. Hatutaki unafiki wala uchochezi. Hili lisiishe hivi hivi hatua madhubuti zichukuliwe kulishughulikia suala hili tena kwa uwazi kabisa.
 
Ndugu Zitto, hao unaowasema ni wafanyikazi wa serekali, wanaweza kuwemo wale civil servant ambao hawahusiani na chama na wale waliochaguliwa na raisi, haimaanishi Raisi magufuli na awamu ya nne ndiyo inayofanya hivyo.

Nina uhakika utakuwa na majina yao, na hutayataja kwa kutaka tuhuma hizi zisimuondoke Magufuli nawe uendelee kupata kiki za kisiasa.

Mara nyingi nimependezwa na jitihada zako na kuziunga mkono hata kukutetea. Lakini kuna wakati wa dharura unajiweka wewe kwanza na Taifa nyuma.

Kama ni tuhuma tuu na huna uhakika nazo, why bring them up, a good politician talk openly on cfrucial matters and detrimental to the state , and one should not look for political milage, ama no yale yale ya Pesa za Switzerland
Hujamuelewa zitto, yy ni mchokonozi. Sasa Kesha chokonoa mada ili ahojiwe. Kisha amwage nondo zake.

Alivyofanya no sahihi zaidi kuliko kuja na majina azue taharuki. Acha Sasa waanze kutapatapa anaujua ukweli kea kiwango gani.

Ishu ya wanyantunzu 100 wenyewe wame nyoosha mikono juu
 
Zitto Kabwe had long lost credibility. Miradi ya Chuma na Makaa ya mawe, Liganga na Mchuchuma imeanza kutajwa tangu enzi za utawala wa Mwlimu Nyerere. Hadi sasa hakuna tangible development plans za kuendeleza/kuzalisha chuma au makaa ya mawe kutoka Liganga au Mchuchuma. Kuhusisha miradi isiyokuwa na mipango wala mikakati ya utekelezaji na mradi wa SGR uliobuniwa miaka ya karibuni na ukiwa unatekelezwa kulingana na feasibility study report pamoja na implementation proposal ni upuuzi wa kiwango cha hali ya juu. Zitto ni mwongo, mzadiki na mpuuzi aliyeshindwa kuhudumia wananchi jimbo la Kigoma Ujiji na sasa akitafuta kiki za kubaki Bungeni bila kuwajibika ipaswavyo jimboni mwake. Apuuzwe.
 
Hujamuelewa zitto, yy ni mchokonozi. Sasa Kesha chokonoa mada ili ahojiwe. Kisha amwage nondo zake.

Alivyofanya no sahihi zaidi kuliko kuja na majina azue taharuki. Acha Sasa waanze kutapatapa anaujua ukweli kea kiwango gani.

Ishu ya wanyantunzu 100 wenyewe wame nyoosha mikono juu
Ndugu GF, nimemuelewa, ila wewe ndiye hukunielewa. Mtu kama Zitto mwenye haiba ya kuweza kuwa Raisi , haweza kuja na vichokonozi, bali anatakiwa kila mara asimame penye ukweli na kuyaweka bayana.
Nimesiki siwezi kuyasema au ninawajua lakini siwataji ina maanisha anaitumia hiyo habari kisiasa ama hana habari kamili ama za ukweli na anajikinga kisheria huku akichocheza. Au wengine wanaweza fikiria anayo majina bali anayatumia kimaslahi yake binafsi hata kuweza kuwakomoa wahusika wakamlipa kifedha kuendesha shughuli zake kisiasa.
 
Back
Top Bottom