Zitto sasa unakera

Retired, analeta hoja zisizo na msingi ; zenye lengo la kupotosha umma na; kuonyesha watu wengine umuhimu wao ni mdogo katika jamii- TAKE HOME- UMBEYA
Fine, umbeya ni nini? Kusema ukweli au kusema uongo. Kati ya hivyo anafanya kipi?
Huku mitaani UMBEYA ni kusema ukweli usiokuhusu! Namkuta mtu anazini natangaza, ni ukweli lakini haunihusu. Does this example hold true for Zito?
 
chige, wakurugenzi wanalipwa mishahara na makampuni yao; kwa vile wanalipwa mishahara wanakatwa PAYE; na kwa kuwa wanamiliki makampuni makampuni waliyoyaanzisha kwa mitaji yao wanalipa kodi ya makampuni nk
Huyo Mkurugenzi aliye kwenye payroll anaingia kwenye kundi la WAFANYAKAZI wote Tanzania ambao ndio hao wanachangia 75% lakini biashara yake inaingia kwenye kundi la biashara zote Tanzania ambazo kwa ujumla wao ndo wanachangia hiyo 25%!

So, hoja ya Zitto, hata huyu Mkurugenzi anaposimama kama Mfanyakazi; nae anastahili kupunguziwa huu mzigo wa PAYE!

Lakini kwa upande wa pili; kama kuna ujanja ujanja huwa anafanya kwenye biashara yake basi aache huo ujanja ujanja na aanze kulipa kodi stahili za biashara zake ili biashara yake yeye na zingine zote Tanzania; wawe wanalipa kodi kubwa zaidi... ili, let's say, ipande from 25% ya sasa to 65%!!

Lakini kama hakuna janja janja yoyote; basi azalishe zaidi na auze zaidi ili hatimae aweze kulipa kodi kubwa zaidi kupitia hiyo biashara!

Of course, kwa hiyo hoja ya mwisho kutimia panahitaji factors zaidi ya moja!

But all in all, hoja ya Zitto inamaanisha jambo moja la msingi: kwamba, mchango wa kodi unaotoka moja kwa moja kwenye mauzo ya makampuni ni mdogo... inawezekana wengi wanakwepa kulipa kodi au ufanisi wa biashara ni mdogo au yote kwa pamoja! Matokeo yake, mlipa kodi mkubwa ni Mfanyakazi kwa sababu yeye hana namna ya kukwepa kodi kama ambavyo Mkurugenzi uliyemtaja anavyofanya kukwepa kulipa kodi stahiki ya biashara yake!

Anything missing?!
 
Zitto ni moja ya wapika data wazuri, usipokuwa msomaji na mfuatiliaji wa mambo utamwamini kwa 100%.

Ukweli ni kuwa zitto ni moja ya wapiga hela wakubwa wa nchi hii.

Hana credibility ya kukosoa ujinga wa serikali.
All are the same.
Sina imani naye na ndo maana binafsi sina muda wa kumsikiliza. Zitto anahangaika kusoma data za wengine. Yeye mwenyewe hajawahi hata siku moja kutengeneza data. Yupo wa pili Bashe ambaye pia sasa ni kila siku data za internet na contradiction kibao!
 
chige, UNAONGELEAJE MSHAHARA NJE YA MWAJIR?
 
Bakhresa na Mengi wanaingia humo kwa mishahara ya sekta binafsi. Ni uonevu kutowapandishia wafanyakazi mishahara miaka minne mfululizo. TUCTA hawafanyi yanayowapasa. Wamekuwa kama idara ya Serikali!
 
Sasa hujaelewa nini?..... Makampuni ya Bakhresa na Mengi yamo kwenye hiyo 25% na Wafanyakazi wao wamo kwenye 75% fullstop!
Nashukuru kumwelewesha japo kwa ufupi sana...makampuni ya madini haya ambayo wanayaita ya mapepari wa Lisu kipindi cha nyuma tulipiga kelele sana kuwa wanalipa kodi kidogo ukilinganisha na kodi wanayolipa wafanyakazi wa o, tunahitaji zaidi tujikite hapa tuone uhalisi kulingana na uchambuzi wa kitaalam
 
Zitto ni moja ya wapika data wazuri, usipokuwa msomaji na mfuatiliaji wa mambo utamwamini kwa 100%.

Ukweli ni kuwa zitto ni moja ya wapiga hela wakubwa wa nchi hii.

Hana credibility ya kukosoa ujinga wa serikali.
All are the same.
Kaka si uthibishe kwa kuchambua alichoandika? So simple. Hao waliotishia kumkamata mbona hawajafnya hivyo mpaka sasa?
 
Mjulishe pia kama kampuni imepata hasara hailipi corporation tax
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…