Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,500
Mgombea Ubunge Jimbo la Kigoma Mjini kupitia Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amewataka wasimamizi wa uchaguzi kuhakikisha zoezi la upigaji kura linakuwa la wazi kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi mkuu.
"Ninajua watu wanahofu na uchaguzi, wengine wanauliza tukikupa kura hawa watu hawatoyafanya ya 2020? Nataka kuwahakikishia watu wa Lusimba na Ujiji, hakutokuwa na atakayeiba kura wala kuleta kura feki na atatangazwa atayeshinda.
Hivyo tarehe 29 kazi ni moja tu katika jimbo hili ni kwenda kupiga kura, na nendeni mkapige kura kwa wingi na kwa amani hakutokuwa na vurugu yoyote" amesema Zitto
Zitto alisema hayo wakati akizungumza kwenye mkutano wake wa Kampeni uliofanyika katika Kata ya Rusimbi Mkoani Kigoma, jana Oktoba 22, 2025.