Zitto: Nitafanya uamuzi mgumu

Status
Not open for further replies.

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
52,209
Reaction score
162,786
Zitto amekaririwa na gazeti la Mtanzania la leo Jumamosi ya tarehe 14/03/2015 akisema kuwa atachukua uamuzi mgumu kuhusu hatima yake ndani ya CHADEMA.
====================


Chanzo:Mtanzania
 
Kila siku .. Kila siku.. "Nitafanya nitafanya..'" Unadhani maamuzi Magumu MCHEZO..!

1: ukiamua kujitoa CDM.. Utaendapi... ?!,. ADC?!? Ambao wameanza kutimuana, Ccm ishawatupia kipande Cha mfupa wamechakazana majuzi, utakuja TADEA!?, CUF?!(UKAWA).. Au utaendapi Mwenye muchknow Wetu..

2: utang'angania Bunge limkingie kifua .. Lakini Ndo kweishney .. Unajua watu wengi njaa zinatusumbua.. Kila Mtu ana njaa Yake.. Kiongozi njaa kila siku maslahi Yake atayatanguliza..
 
Looser huyo,akafie mbele huko.
 
Hatima yake ilishatoka ipo nje ya chadema kwa kuwa alishafukuzwa,labda aseme maamuzi magumu ndani ya act
 
Chukua uamuzi, haraka, ndo ujue kuchukua uamuzi wa kujiondoa madarakani unavyokuwa mgumu. Hahahaahaha haya yamekufika onyesha mfano
 
Huyo hataki kupoteza mafao ya ubunge ndo mana anambwelambwela.
Chezea 200m wewe!
 
Too late and too low.
Maamuzi ya nini tena wakati ameshafukuzwa CHADEMA? Kama kumwaga, CHADEMA walianza kumwaga mboga, Zitto akaendelea kusita kumwaga Ugali, CHADEMA juzi wamemwaga na ugali kabisa. Sasa hakuna msosi tena. Zitto kwisha habari yake kabisa.
 
Uamuzi mgumu nadhani ni wakubaki na kung'ang'ania kuendelea kubaki na kuwa mwanachama wa Chadema even if, Chadema imemfukuza. Huo ndio uamuzi mgumu, tofauti na hapo nadhani ni rahisi tu hakuna ugumu wowote.

Ajipange kweli kweli..

BACK TANGANYIKA
 
lazima zito atambue jambo moja kuwa hakuna mtu ambaye muhimu sana mahali popote iwe ni ndani ya vyama, ndani ya serikali au katika familia.

kila jumuia ina maadili yake na kila anayekiuka maadili lazima kanuni na taratibu zichukue mkondo wake.

tusijiweke mbele kama watu wenye mitizamo ya kubadili uozo ulioko katika jamii huku sisi wenyewe tukifanya madudu.

vyama vya upinzani vinahitaji kukua lakini kukua kwa afya ya kutojenga viburi ndani ya vyama.

popote mwananchama wa kawaida akikiuka taratibu basi anahukumiwa na viongozi hivyo hivyo.

hivyo si busara kwa mijadala hii kama aliyotuhumiwa ni ya kweli.

siasa ni kuwa na wananchi wa kukusapoti hivyo hakuna haja ya kugangania chama kama unadhani unayoyafanya yana wafuasi wengi nyuma yako kwa maana siasa siku hizi ni huria hata mgombea binafsi unasimama kutafuta uraisi.

lakini kama unaona nguvu iko kwenye chama hicho basi kuwa mpole kwenye kanuni za chama.
 
Hakuna Uamuzi Mwingine Mgumu ambao ni makini anaopaswa kufanya zaidi ya Kuomba Radhi kwa wapenzi na wanachama wa CHADEMA na kusonga mbele

Kwenda chama Kingine itakua uamuzi mgumu lakini sio makini

Na pia uamuzi mwingine mgumu ni kuachana na siasa. Aliwahi kukaririwa kipindi fulani kuwa anataka kuwa mhadhiri wa uchumi katika mojawapo ya vyuo vilivyopo, huenda ndio anataka kufanya hivyo.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…