Akae huko huko huyu msaliti, anataka aingie UKAWA anusenuse mikakati ya UKAWA kisha aende TISS apeleke habari nyeti za ndani ya UKAWA. Huyu si mtu wa kuaminika hata kidogo UKAWA wasifanye makosa ya kumkaribisha huyu. Usaliti alioufanya ndani ya CHADEMA umetosha na hadi hii leo hataki kuomba radhi kwa usaliti mkubwa alioufanya.
BAK nitatofautiana na wewe.Kama atashirikiana na UKAWA na wote wakawa na NIA na LENGO moja la kuitoa CCM madarakani,basi UKAWA wanatakiwa wakubaliane naye.Kwani MSIHIRIKI wa mambo yetu ni mwenzetu.
Hata Yesu alisema,ukiona anahubiri na kufanya kama tufanyavyo basi msikataze ni MWENZETU.Cha msingi anatakiwa ajue na ajitoe kabisa.
Ila alikosea sana kujiunga ACT ,nafuu angeenda CUF au NCCR.
Wasaliti mara nyingi huwa hawabadiliki, kama angekuwa anataka kweli kubadilika basi angeomba radhi kwa CHADEMA na kutubu dhambi zake kuhusu usaliti alioufanya. Kutokuwa tayari kuomba radhi ni ishara ya wazi kabisa kwamba hajutii matendo yake na anaweza kuyafanya tena. Itakuwa ni kosa kubwa kwa UKAWA kumkaribisha huyu, haya ndiyo maoni yangu.
BAK kuomba radhi ni BUSARA ambayo si kila mtu anazaliwa nayo.Huyo mwenzetu hana.Tumvumilie.Ninauhakika kajifunza kiasi kidogo,na ninajua anajua BILA UKAWA hatoki.Umenipata BAK?
Tusubiri tuone, lakini mtu ambaye amejifunza kwamba katenda makosa basi hataona ugumu wa kuwaomba radhi wale aliowakosea lakini huyu jamaa hayuko tayari kufanya hivyo. Usaliti alioufanya anaona ni kitu ambacho alipaswa kukifanya.
Zitto anajiona yeye ndio yeye hana tofauti na Augustine mrema aliejifanya mpinzani wa kweli lkn sasa anaipigia magoti ccm. Huyo ndio amekwisha tena.
Zitto kama mwanasiasa hana tatizo na ukawa, kwani chadema si wamekula matapishi yao, yaani wameungana na waliberal CUF ilikupata nguvu kwenye Bunge la katiba na chaguzi za serikali za mitaa, wakisha maliza uchaguzi mkuu CUF watatelekezwa na kutukanwa kama awali
Kaka BUSARA haipatikani tu bali mtu huiomba toka kwa aliyemuumba.Hebu nikukumbushe mfalme Suleiman aliomba BUSARA na si UTAJIRI,lakini ndiyo alikuwa tajiri zaidi uliwenguni kwa enzi zake.
BUSARA ni kitu ambacho viongozi wengi wa KIAFRIKA hawana,Mara zote wanafikiri kutumia nguvu ndiyo silaha.Hawana BUSARA ndiyo maana hawajui kutumia japo AKILI ndogo tu waliyonayo au waliopewa.
Waweza kuwa na AKILI ndogo lakini ukawa na BUSARA nado ukaongoza vyema sana tu.
Hayo yote nayakubali lakini naamini pia mwenye busara anapokosea basi hutumia busara zake kuwaomba samahani wale aliowakosea, hayo ni matumizi mazuri ya busara ili kuweza kuondoa kutoelewana kulikotokea kwa makosa yaliyofanywa na mkosaji. Ikiwa mkosaji huyo haoni hata umuhimu wa kuwaomba samahani wale aliowakosea basi hatumii busara zake kama anazo vile inavyopaswa. Hivyo yeye na wake aliowakosea itakuwa vigumu sana kukaa meza moja kupanga mikakati yoyote ile ya maana kwani tayari kuna kiwingu cha huyo mkosaji kutokuwa mwaminifu kwa wenzie.
Acha uwongo, angekuwa haungi mkono UKAWA mbona alikwenda kwenye mikutano ya CUF kule Lindi na Mtwara baada ya kualikwa na Prof. Lipumba ambae yuko UKAWA? Kwenye hilo bunge la katiba mbona hata yeye hakuudhia sehemu ya mwisho iliyopitsha katiba pendekezwa!
Umeshasema HANA BUSARA,na ndiyo maana viongozi wa UKAWA wanatakiwa kuamua kwa BUSARA kufanya kazi naye upo kaka BAK,siyo lazima kila kitu ajue bali ile tu namna ya kusaidiana kuwatoa CCM kwa madaraka.Upo?Nina uhakika anajua kuwa bila UKAWA hana chake.NA tafanya kila jitihada kuwa pamoja na UKAWA.Na mind you hata hao akina Mwigamba wasitegmee kusaidiwa kupata au kupigiwa kampeni na Zitto sababu yeye mwenyewe itabidi awasubiri UKAWA wamsaidie kupiga debe.
Hivyo walimuingiza ACT ndiyo wameingia CHAKA kaka BAK
kumuelewa zitto inahitaji uwe umevuta ganja kubwa kuliko vidole vya kingkong.
Dada yangu Tetty nakubaliana nawe kila kitu unachoandika lakini hila ya huyu mtu kutokuwa tayari kukaa meza moja na Dr Slaa, Makamanda Mbowe, Tundu Lissu na Mnyika na kuwaomba radhi kwa aliyowahi kuyafanya ndani ya CHADEMA na pia kuwaomba yaliyopita si ndwele tugange yajayo basi kamwe hastahili kuaminiwa kwa lolote lile.
Tumeona juzi habari ya kupewa sumu kwa Dr Slaa katika mazingira kama haya ya watu wa ndani kutumiwa ili kutaka kumdhuru Dr Slaa basi mimi msimamo wangu ndio huo dada yangu bila mtu kuomba samahani basi asipewe nafasi ya kukaa meza moja na UKAWA.
Nafurahia uwezo wako mkubwa wa kujenga hoja nzito kuhusu mjadala huu na mingineyo pia.
Tunasaidiana na kuelimishana.Ila ukumjua mbaya wako ni rahisi kuishi naye.Na ukiijua tabia ya mtu wala hupotezi muda naye.