Zitto ni kiongozi shupavu

Status
Not open for further replies.
Kizuri chajiuza, kibaya chajitembeza.
Na bado magamba mtahaha sana kupiga madebe...

Sio tu katika kumpigia debe, bali ni jitihada mahususi za kutaka kutengeneza minyukano ya kugombea uongozi ndani ya CDM. Zidhani kama watafanikiwa, watanzania sio wajinga tena.

Pili Tangu issue ya Lwakatare ijitokeze, inaenda sambamba na uyu jamaa kuonyesha Zito ni kiongozi bora (huu ni uzi wa pili ndani ya wiki moja wa kumtangaza zito positive). Nahisi ni preemptive strategy za kumlinda...twendeni taratibu mengi yatajulikana.
 
mkuu umeongea point zzk ni mtu makini sana baadhi ya watu hawataki kuamini namkubali sana mtu huyu endapo akipata nafasi kugombalia 2015 basi chadema watapata kura yangu tofauti na hapo imekula kwao nakumbuka ufanisi wake wa uchapa kazi ulinivutia mimi kumfata dodoma bungeni kuona live ufanisi wake.naamini siku moja atakuwa rais wa nchi ni mtu makini sana much blesed to zzk





 

Umewahi kumsikia akisema neno wakati Chadema kinapata mtikisiko? Mawasiliano yake na Denis Msaky wa gazeti la Mwananchi ambaye sasa yuko kwenye sakata hili la Lwakatare kila mwenye akili utajihoji maswali mengi na siyo kumpamba kama anavyofanya mleta mada au pengine inawezekana mleta mada anamsifia kwa mitikisiko inayotokea Chadema.
 
Wewe sasa umetoa siri lengo kuu la Mhe ZZK NI KUJIKWEZA ETI AWE MAARUFU KULIKO Dr Slaa na Mhe Mbowe!! Kapandikiza wakina Shonza na masalia, kachomeka mambo kibao ndani ya CHEDEMA na marafiki zake kina Jack Zoka TISS!!! Sasa wakati huu baada ya kusuka huu mpango wa kumchafua Dr Slaa kupitia shutuma za kupika za TISS NA WADAU wake anaona alete hapa apime upepo watu wana respond vipi??? Ukiangalia post za watoa mada na wachomekeaji wote ni wapya, kwa hiyo ameunda new team baada ya masalia kukaa kando au wamekuja na ID mpya!!! ZZK anahangaika saana, matokeo yake anadhoofisha chama chetu, badala ya kusonga mbele kwenye ukombozi tubaki tukilumbana na next Prezoo, poor ZITO!!!!

 

Utafiti wa REDET na Synovate hautawasaidia. Umetembelea mikoa mingapi? Muulizeni huyo jamaa mnayempigia debe kwanini baada ya Kikao cha Kamati Kuu Januari alikimbilia Kigoma? Msijipe matumaini hewa
 

Hata wakija na ID mpya 100 sisi ni wale wale tutawadhibiti mpaka mwisho.
 
Utafiti wa REDET na Synovate hautawasaidia. Umetembelea mikoa mingapi? Muulizeni huyo jamaa mnayempigia debe kwanini baada ya Kikao cha Kamati Kuu Januari alikimbilia Kigoma? Msijipe matumaini hewa
Zitto hakubaliki ndani ya vikao vya chama tu (japo si kwawajumbe wote) lakini nje ya vikao hivyo Zitto ni zaidi ya chama chenyewe
 


Historia inaonyesha kua Rwakatare siyo rafiki wa waandishi wa habari, nakumbuka 2005 alifikishwa mahakani kwa kosa la kumpiga mwaandishi wa habari wa ITV/Radio one.
 
Zitto hakubaliki ndani ya vikao vya chama tu (japo si kwawajumbe wote) lakini nje ya vikao hivyo Zitto ni zaidi ya chama chenyewe
Hapa JF pia hakubaliki, nako kuna vikao vya chama? Umbali kwenu ni pale zinapoishia pua zenu?
 
Ndugu zitto kaonesha hekima kubwa sana katika siasa za Tz, ametumia hekima ya kipekee katika mambo yanayomuhusu,
  • yalianza ya kuhisishwa na rushwa hakupaniki akasema uchunguzi ufanyike kumbe hakukuna na uhalisia wa aliyetoa kauli,
  • yakaja mengine ya kutaka kuwekewa sumu na wezake ktk chama akali handle suala hilo kwa hekima kubwa bila ya kujiharibia chochote ,mwisho unaoneka hakuna ukweli au uhakika wa mambo yale.
  • Kubwa na lilinoshangaza ni hili la juzi la mama yake kuvamiwa na kukiri kuwa mmoja wa majambazi hao ni kada wa chadema.Naamini kabisa mwanasiasa mwingine siku hiyo hiyo angerudisha kadi kwani zitto anauwezo wa kuunguruma chama chochote mfano nccr,cuf huko hata urais anaweza pewa agombee bila kupingwa hata ccm anaweza kupewa nafsi kubwa tu LAKINI MUHESHIMIWA ALITAMBUA YAFUATAYO:-

  1. KUNA MAKADA MANGAPI WA CDM KWANZIA MTAA,KATA,WILAYA MPAKA TAIFA?
  2. KWANI MTU KUWA CDM NDIO KAWA MALAIKA ASIRUBUNIWE?
  3. KWANI HAWEZI KUWA KATUMWA NA VYAMA VINGINE KUHARIBU CHAMA?
  4. KATUMWA NA NANI ?JE KATUMWA NA CDM ETI KWA KUWA YEYE NI CDM?.
Baada ya kuweka into consideration yote hayo akatoa kauli kuwa suala lile liko polisi, na ukweli wa yote utajulikana na hatua stahiki zitachukuliwa HIZO NDIO HEKIMA ZA WENYE UWEZO WA KUONGOZA NCHI. sio kupelekwa pelekwa na upepo.
NI MFANO WA KUIGWA.
 
... ni hayo tu ndio yamekufanya uanzishe thread kweli mkuu???????
 
Vijana wa Chadema mnatumika bila kujua kuleta migongano ya viongozi! Unaweza kukuta mwanzisha mada ni Nape kaingia kwa ID bandia anaanzisha mada ambayo anajua kama kawaida ya vijana wa Chadema wataishia kunyukana!
Anzeni kujifunza ku ignore viji thread kama hivi!
 
mkuu whitebl uko sahihi kabisa, wengine tupo na zitto kwenye chama muda mrefu sana, huyu jamaa ni hatari sana, kwnn akisifiwa sana anapoteza mwelekeo kabisa hivyo akipata nafasi kama ya urais wapambe wanaweza kumsifia kwa maslahin yao na akasitukia anauza nchi. anahitaji mtu makini wa kumsimamia ndio anaweza kufanya kazi vizuri.
 

shule zetu za kata hizi; hapo ndo mwisho wako wa kufikiri?
 
ndugu yangu Mwalimu Mzalendo si kila mwandishi wa habari ni mzuri, watu kama akina msacky utaniambia ni mzuri, labda ataonekana mzuri kwasbbu kapewa kazi ya kuvuruga cdm.
 
ndugu yangu KAKADO chadema haihitaji kura chafu ya kwako nenda kampigie zitto jimboni kwake.
 


Picha ya ndugu Zitto ikiwepo kwenye karatasi ya uchaguzi wa Rais 2015 ( Presidaa au Vice kama Ruto),,,Chadema wanachukua nchi kiulaini kabisa:

Zitto ndiyo King au Kingmaker uchaguzi 2015:!!You can take this to the bank!!
 
uko sahihi kabisa Chintu, kuna watu huyu zitto hawamjui kiundani.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…