Zitto ni bora uondoke zako chadema u have nothing to lose!

A

assadsyria3

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2013
Messages
6,733
Likes
2,303
Points
280
Age
38
A

assadsyria3

JF-Expert Member
Joined Apr 9, 2013
6,733 2,303 280
HIVI karibuni nilishuhudia mmoja wa rafiki zangu hapa Shanghai akiachwa na mpenzi wake kupitia ‘skype’ pale alipoambiwa na mpenzi wake huyo kuwa amekutana na kumpenda mwanamume mwingine.
Binti yule anayeishi Italia, alimwambia kuishi mbalimbali kunafanya uhusiano wao huo kutowezekana. Wawili hawa walikutana Afrika Kusini wakati wote wakiishi huko na baadaye walitawanyika, mmoja China mwingine Italia kwa ajili ya masomo.
Rafiki yangu, Michael, alishtuka kwani hakutegemea hilo, alimjibu binti kwa huzuni,“Nakupenda sana, ila nataka uwe na furaha na kwa sababu hiyo siwezi kuwa kikwazo katika kuitafuta furaha yako. Nakutakia kila la kheri. Niko radhi”.
Huenda hivi ndivyo ambavyo Zitto Kabwe anapaswa kufanya katika muktadha wa mgogoro uliojitokeza karibuni katika uhusiano wake na chama chake cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Mgogoro huo, uliouza magazeti, uliisukuma Kamati Kuu ya Chama hicho kumvua mwanasiasa huyo kijana nyadhifa zake zote za uongozi ndani ya chama ikiwemo unaibu katibu mkuu na kumpa siku 14 kujieleza kwa nini asivuliwe uanachama.
Kutokana na uamuzi huo wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Zitto alikutana na waandishi wa habari na kutangazia kuwa anaipenda CHADEMA kiasi kwamba angependa hata mwanawe siku moja naye aje kuwa mwanachama.
Lakini, busara za Zitto katika uamuzi zilitofautiana na za rafiki yangu Michael. Zitto ameamua kung’ang’ania na kukataa kutalikiana na CHADEMA licha ya kukiri kuipenda. Kwa maneno yake anasema atakuwa wa mwisho kutoka CHADEMA kwa hiari.
Kutoka katika mtazamo wa mchambuzi huru, nisiye na upande, naamini Zitto kama kweli anaipenda CHADEMA, uamuzi sahihi ulikuwa ni kutoka na sio kubaki.
Swali la msingi la kujiuliza, kufuatia maoni ya viongozi waandamizi wa CHADEMA ni kwanza, je kwa Zitto kuendelea kuwepo ndani ya CHADEMA kutaisaidia au kuiangamiza CHADEMA? na pili, je, kwa hali ilivyo ndani ya CHADEMA, ndoto za Zitto za kuitumikia nchi yake na kufikia malengo yake binafsi ya kisiasa zinaweza kufanikiwa?
Ni wazi kuwa hisia, chuki na upinzani ndani ya CHADEMA dhidi ya Zitto, falsafa yake na walio nyuma yake ni kubwa na dhahiri. Baadhi ya viongozi waandamizi, wakiwemo wabunge wanamkosoa kila wanapopata jukwaa zuri la kufanya hivyo.
Unaweza kusema makundi na watu kutofautiana mitazamo ni kawaida katika vyama. Lakini inapofikia hatua ya kuitana ‘mnafiki’, ‘mzandiki’, ‘mhaini’, ‘msaliti’, ‘mchonganishi’, ‘mzushi’, ‘muongo’ na mengine mengi ni ishara ya uadui na kutoaminiana. Kwenye ndoa hizi ni tofauti zisizosuluhishika.
Katika akaunti yake ya Facebook, Joseph Mbilinyi, Mbunge wa Mbeya Mjini aliandika, “Big up sana kamati kuu CDM...there should be no room for SNITCHES (wazandiki) huku Peter Msigwa akiandika “…kila harakati huzalisha mashujaa kwa ajili ya cause, pia huzalisha wasaliti, lakini mara zote historia inaonyesha wasaliti walishindwa.”
Ingawa hakukutajwa majina, wote tunaelewa nani analengwa katika muktadha wa yanayotokea ndani ya chama hicho.
Zitto, kwa upande wake amewaita wapinzani wake kuwa ni wahafidhina, wabadhirifu na watukuzao siasa majitaka huku mwenyewe na kundi lake wakijitambulisha kama wapenda demokrasia, waumini wa uwajibikaji na wapenda siasa safi. (Rejea waraka taarifa yake yakujibu tuhuma).
Kutoaminiana na hisia hizi za kuwa kundi moja ni la wasaliti, wahaini inafanya tofauti ya mitazamo kuwa kubwa mno. Aina hii ya tofauti, ambayo hujitokeza mara kwa mara katika siasa za Tanzania sio tena chachu ya maendeleo bali ni nguvu hasi ya kukirudisha nyuma chama.
Ni kwa kuzingatia hilo ndio maana Zitto anapaswa kutoka CHADEMA, bila kujali kama atafukuzwa ama laa. Kwa kutoka, Zitto atakuwa amedhihirisha mapenzi yake kwa hicho. Kutoka kwake kutaleta utulivu. Uwepo wake ndani ya CHADEMA hautosaidia chama hicho ambacho ni wazi kuwa viongozi, wanachama na wafuasi wengi hawana imani naye tena.
Zitto anapaswa kufuata maono na ushauri wa mama yake ambaye baada ya Zitto kuvuliwa uanachama alinukuliwa akishukuru akiamini ni hatua nzuri kwa usalama wa mwanawe. Shida Salum, kama ambavyo anajulikana ambaye naye amekuwa ni miongoni mwa viongozi walio mstari wa mbele wa CHADEMA, alinukuliwa akisema kilichomkuta mwanaye kimefunika mabaya mengi yaliyopangwa afanyiwe ili amalizwe. Maoni haya yanatoa msukumo zaidi kwa Zitto kuona umuhimu wa kukaa pembeni.
Na ieleweke kuwa waraka wa siri ni moja tu kati ya shida nyingi zinazofanya mgogoro wa ndoa ya Zitto na CHADEMA uwe hausuluhishiki.
Zipo shutuma kuwa ushiriki wa Zitto katika shughuli za chama ni hafifu na kwamba kwenye matukio muhimu yenye maana ambayo ni ya kukijenga chama haonekani. Inatolewa mifano ya matukio makubwa ya uchaguzi Tarime na mikutano iliyoishia katika fujo na kuua watu huko Arusha, Iringa, Morogoro. Kuna tuhuma za kuuza majimbo, kuna tuhuma za kununuliwa na kwa kutumika na CCM na Idara ya Usalama wa Taifa ili kuhujumu CHADEMA na sasa hili la waraka wa siri!
Zitto amekuwa akijaribu kutoa changamoto ya kutolewa ushahidi wa tuhuma hizo, lakini nilitegemea akiwa mwanasiasa mzoefu, anapaswa kujua kuwa kwenye siasa, mtazamo ya watu ni muhimu kuliko ushahidi. Kama huaminiki, hakuna aina ya ushahidi itaondolea tuhuma.
Katika mkutano wa waandishi wa habari uliotumika kujibu hoja za Zitto na Dk. Kitila Mkumbo, mwanasheria wa CHADEMA Tundu Lissu na John Mnyika walijibu utetezi na madai ya Zitto na Dk. Kitila Mkumbo na kuwaita waongo na wazushi. Kwa waliyoyasema, ni wazi kuna uwezekano mkubwa wa CHADEMA kumfukuza uanachama Zitto ama sivyo, Zitto atakayebaki CHADEMA atakuwa ni mzigo kuliko msaada kwa chama na hata yeye binafsi hatoweza kutimiza ndoto zake.
Mustakabali wa Zitto
Zitto akitaka kubaki CHADEMA anachoweza kufanya ni kuomba radhi (bila kujali kama makosa anayotuhumiwa yana ushahidi au hapana) na pia kukubali kuachana na dhamaira yake ya kugombea uenyekiti au nafasi nyingine za juu za uongozi katika chama hicho.
Hili likitokea litafurahisha wengi hususan sauti za busara ndani ya chama kama Profesa Mwesiga Baregu, ambaye amesikitika akitahadharisha uongozi ufikirie mara mbili kabla ya kuchukua hatua zaidi dhidi ya Zitto na wenzake hasa ukizingatia pamoja na mapungufu yao wamekifanyia mengi chama.
Lakini kiuhalisia haileti maana Zitto kuomba radhi na kukubali kuachana na ndoto zake za kuleta mageuzi ya kiungozi. Zitto atakuwa anauishi uongo ukizingatia kuwa ni wazi anaamini kuwa uongozi wa sasa hautoshi na una mapungufu mengi na makubwa mno.
Kwa maana nyingine ni kwamba Zitto na Kitila hata wakiomba radhi hawawezi kuacha harakati za mapambano yao wanayoyaita ya kuleta “mabadiliko makubwa katika uongozi wa juu wa chama na kuleta demokrasia”. Harakati zozote za namna hiyo, kutokana na mtazamo wa wanachama kwao - wahaini, wanafiki, wasaliti, wahujumu, wazandiki - itakuwa ni nguvu hasi ya kuharibu chama kuliko kukijenga.
Vinginevyo kama Zitto hawezi kuomba radhi, ni vema ajiandae kwa maisha nje ya CHADEMA aidha kwa kufukuzwa au kutoka mwenyewe atakapoona ndoto zake za kisiasa hazitatimia, ingawa kilicho bora ni kutoka kwa hiari ili athibitishe mapenzi yake kwa chama hicho. Wanasema umpendae utamlinda.
Nitamuelewa Zitto iwapo akiamua kuing’ang’ania CHADEMA ili asipoteze ‘neema mbalimbali’ ambazo msingi wake ni uanachama, kama ubunge na uongozi wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC). Kupoteza vyeo hivyo kunaweza kumpoteza katika siasa. Kwa maana hiyo hesabu za kung’ang’ania CHADEMA kwa sasa akinunua muda zinalipa.
Nje ya CHADEMA, Zitto ana uchaguzi wa aina nne. Aache siasa, ajiunge na CCM, aunde chama chake ama ajiunge na vyama vingine vya upinzani. Kuacha siasa si rahisi, itakuwa ni kukubali kushindwa kirahisi. Kujiunga na CCM litakuwa kosa kubwa kwani atakuwa amethibitisha dhana iliyojengeka kuwa ni mtu wao. Kuanzisha chama kutampotezea muda mwingi.
Chaguo lenye mantiki ni kuhamia chama kingine cha upinzani. Miongoni mwa vyama vya upinzani, huenda Zitto akaishia NCCR Mageuzi. Akienda CUF anaweza kwa urahisi kumrithi Profesa Ibrahim Lipumba lakini atajitwisha jukumu zito la kuondoa dhana kuwa ni chama cha Waislamu.
Athari kwa CHADEMA?
Wanaoamini kuwa CHADEMA itaathirika kwa kuondoka Zitto wanakosea kwani athari za mvutano uliopo sasa ni mbaya kuliko wanachama itakaowapoteza kwa kuondoka Zitto.
Hata hivyo, baada ya mnyukano huu kupita na hususan baada ya kujiuzulu kwa Makamu Mwenyekiti, Said Arfi, CHADEMA inapaswa kupambana zaidi ili kukubalika maeneo ya Waislamu wengi ili iweze kuondoa dhana kuwa ni chama wa Wakrito. Kadhalika, CHADEMA itapaswa kutafuta uwiano mzuri katika safu yake ya uongozi ili kuondoa fikra kuwa chama hicho ni cha kikanda.
Katika minyukano hii ya kisiasa, jambo moja muhimu tunalojifunza ni kuwa dini na ukanda ni uhalisia ulipo katika siasa zetu na ni bora tuvikubali kama vigezo muhimu vya uchambuzi wa utendaji wa siasa zetu. Tukiukubali ukweli huu mapema ni faida yetu. Tanzania hii si ile ya Mwalimu Nyerere.
Nimalize kwa kuhoji kuhusu njia iliyotumika kuukamata waraka wa siri wa Mwigamba, Kitila na wenzake. Kama habari kuwa alinyang’anywa laptop yake ni kweli, hivi tukinyang’anya laptop za viongozi wote wa CHADEMA au vyama vya siasa na kupekua, kuna atakayesalimika na uhaini, uhujumu, mbinu chafu na kadhalika?
BY Njonjo Mfaume
 
sir mushi

sir mushi

Senior Member
Joined
May 26, 2013
Messages
144
Likes
4
Points
0
sir mushi

sir mushi

Senior Member
Joined May 26, 2013
144 4 0
waziiiiiii afaandeeeeee
 
A

assadsyria3

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2013
Messages
6,733
Likes
2,303
Points
280
Age
38
A

assadsyria3

JF-Expert Member
Joined Apr 9, 2013
6,733 2,303 280
Siasa za babu za ubaguzi chuki visasi kulipiza angalia dogo wasije wakakuchacha wangwe
 
T2015CCM

T2015CCM

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2012
Messages
7,936
Likes
382
Points
180
Age
86
T2015CCM

T2015CCM

JF-Expert Member
Joined Sep 13, 2012
7,936 382 180
HIVI karibuni nilishuhudia mmoja wa rafiki zangu hapa Shanghai akiachwa na mpenzi wake kupitia ‘skype' pale alipoambiwa na mpenzi wake huyo kuwa amekutana na kumpenda mwanamume mwingine.
Binti yule anayeishi Italia, alimwambia kuishi mbalimbali kunafanya uhusiano wao huo kutowezekana. Wawili hawa walikutana Afrika Kusini wakati wote wakiishi huko na baadaye walitawanyika, mmoja China mwingine Italia kwa ajili ya masomo.
Rafiki yangu, Michael, alishtuka kwani hakutegemea hilo, alimjibu binti kwa huzuni,"Nakupenda sana, ila nataka uwe na furaha na kwa sababu hiyo siwezi kuwa kikwazo katika kuitafuta furaha yako. Nakutakia kila la kheri. Niko radhi".
Huenda hivi ndivyo ambavyo Zitto Kabwe anapaswa kufanya katika muktadha wa mgogoro uliojitokeza karibuni katika uhusiano wake na chama chake cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Mgogoro huo, uliouza magazeti, uliisukuma Kamati Kuu ya Chama hicho kumvua mwanasiasa huyo kijana nyadhifa zake zote za uongozi ndani ya chama ikiwemo unaibu katibu mkuu na kumpa siku 14 kujieleza kwa nini asivuliwe uanachama.
Kutokana na uamuzi huo wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Zitto alikutana na waandishi wa habari na kutangazia kuwa anaipenda CHADEMA kiasi kwamba angependa hata mwanawe siku moja naye aje kuwa mwanachama.
Lakini, busara za Zitto katika uamuzi zilitofautiana na za rafiki yangu Michael. Zitto ameamua kung'ang'ania na kukataa kutalikiana na CHADEMA licha ya kukiri kuipenda. Kwa maneno yake anasema atakuwa wa mwisho kutoka CHADEMA kwa hiari.
Kutoka katika mtazamo wa mchambuzi huru, nisiye na upande, naamini Zitto kama kweli anaipenda CHADEMA, uamuzi sahihi ulikuwa ni kutoka na sio kubaki.
Swali la msingi la kujiuliza, kufuatia maoni ya viongozi waandamizi wa CHADEMA ni kwanza, je kwa Zitto kuendelea kuwepo ndani ya CHADEMA kutaisaidia au kuiangamiza CHADEMA? na pili, je, kwa hali ilivyo ndani ya CHADEMA, ndoto za Zitto za kuitumikia nchi yake na kufikia malengo yake binafsi ya kisiasa zinaweza kufanikiwa?
Ni wazi kuwa hisia, chuki na upinzani ndani ya CHADEMA dhidi ya Zitto, falsafa yake na walio nyuma yake ni kubwa na dhahiri. Baadhi ya viongozi waandamizi, wakiwemo wabunge wanamkosoa kila wanapopata jukwaa zuri la kufanya hivyo.
Unaweza kusema makundi na watu kutofautiana mitazamo ni kawaida katika vyama. Lakini inapofikia hatua ya kuitana ‘mnafiki', ‘mzandiki', ‘mhaini', ‘msaliti', ‘mchonganishi', ‘mzushi', ‘muongo' na mengine mengi ni ishara ya uadui na kutoaminiana. Kwenye ndoa hizi ni tofauti zisizosuluhishika.
Katika akaunti yake ya Facebook, Joseph Mbilinyi, Mbunge wa Mbeya Mjini aliandika, "Big up sana kamati kuu CDM...there should be no room for SNITCHES (wazandiki) huku Peter Msigwa akiandika "…kila harakati huzalisha mashujaa kwa ajili ya cause, pia huzalisha wasaliti, lakini mara zote historia inaonyesha wasaliti walishindwa."
Ingawa hakukutajwa majina, wote tunaelewa nani analengwa katika muktadha wa yanayotokea ndani ya chama hicho.
Zitto, kwa upande wake amewaita wapinzani wake kuwa ni wahafidhina, wabadhirifu na watukuzao siasa majitaka huku mwenyewe na kundi lake wakijitambulisha kama wapenda demokrasia, waumini wa uwajibikaji na wapenda siasa safi. (Rejea waraka taarifa yake yakujibu tuhuma).
Kutoaminiana na hisia hizi za kuwa kundi moja ni la wasaliti, wahaini inafanya tofauti ya mitazamo kuwa kubwa mno. Aina hii ya tofauti, ambayo hujitokeza mara kwa mara katika siasa za Tanzania sio tena chachu ya maendeleo bali ni nguvu hasi ya kukirudisha nyuma chama.
Ni kwa kuzingatia hilo ndio maana Zitto anapaswa kutoka CHADEMA, bila kujali kama atafukuzwa ama laa. Kwa kutoka, Zitto atakuwa amedhihirisha mapenzi yake kwa hicho. Kutoka kwake kutaleta utulivu. Uwepo wake ndani ya CHADEMA hautosaidia chama hicho ambacho ni wazi kuwa viongozi, wanachama na wafuasi wengi hawana imani naye tena.
Zitto anapaswa kufuata maono na ushauri wa mama yake ambaye baada ya Zitto kuvuliwa uanachama alinukuliwa akishukuru akiamini ni hatua nzuri kwa usalama wa mwanawe. Shida Salum, kama ambavyo anajulikana ambaye naye amekuwa ni miongoni mwa viongozi walio mstari wa mbele wa CHADEMA, alinukuliwa akisema kilichomkuta mwanaye kimefunika mabaya mengi yaliyopangwa afanyiwe ili amalizwe. Maoni haya yanatoa msukumo zaidi kwa Zitto kuona umuhimu wa kukaa pembeni.
Na ieleweke kuwa waraka wa siri ni moja tu kati ya shida nyingi zinazofanya mgogoro wa ndoa ya Zitto na CHADEMA uwe hausuluhishiki.
Zipo shutuma kuwa ushiriki wa Zitto katika shughuli za chama ni hafifu na kwamba kwenye matukio muhimu yenye maana ambayo ni ya kukijenga chama haonekani. Inatolewa mifano ya matukio makubwa ya uchaguzi Tarime na mikutano iliyoishia katika fujo na kuua watu huko Arusha, Iringa, Morogoro. Kuna tuhuma za kuuza majimbo, kuna tuhuma za kununuliwa na kwa kutumika na CCM na Idara ya Usalama wa Taifa ili kuhujumu CHADEMA na sasa hili la waraka wa siri!
Zitto amekuwa akijaribu kutoa changamoto ya kutolewa ushahidi wa tuhuma hizo, lakini nilitegemea akiwa mwanasiasa mzoefu, anapaswa kujua kuwa kwenye siasa, mtazamo ya watu ni muhimu kuliko ushahidi. Kama huaminiki, hakuna aina ya ushahidi itaondolea tuhuma.
Katika mkutano wa waandishi wa habari uliotumika kujibu hoja za Zitto na Dk. Kitila Mkumbo, mwanasheria wa CHADEMA Tundu Lissu na John Mnyika walijibu utetezi na madai ya Zitto na Dk. Kitila Mkumbo na kuwaita waongo na wazushi. Kwa waliyoyasema, ni wazi kuna uwezekano mkubwa wa CHADEMA kumfukuza uanachama Zitto ama sivyo, Zitto atakayebaki CHADEMA atakuwa ni mzigo kuliko msaada kwa chama na hata yeye binafsi hatoweza kutimiza ndoto zake.
Mustakabali wa Zitto
Zitto akitaka kubaki CHADEMA anachoweza kufanya ni kuomba radhi (bila kujali kama makosa anayotuhumiwa yana ushahidi au hapana) na pia kukubali kuachana na dhamaira yake ya kugombea uenyekiti au nafasi nyingine za juu za uongozi katika chama hicho.
Hili likitokea litafurahisha wengi hususan sauti za busara ndani ya chama kama Profesa Mwesiga Baregu, ambaye amesikitika akitahadharisha uongozi ufikirie mara mbili kabla ya kuchukua hatua zaidi dhidi ya Zitto na wenzake hasa ukizingatia pamoja na mapungufu yao wamekifanyia mengi chama.
Lakini kiuhalisia haileti maana Zitto kuomba radhi na kukubali kuachana na ndoto zake za kuleta mageuzi ya kiungozi. Zitto atakuwa anauishi uongo ukizingatia kuwa ni wazi anaamini kuwa uongozi wa sasa hautoshi na una mapungufu mengi na makubwa mno.
Kwa maana nyingine ni kwamba Zitto na Kitila hata wakiomba radhi hawawezi kuacha harakati za mapambano yao wanayoyaita ya kuleta "mabadiliko makubwa katika uongozi wa juu wa chama na kuleta demokrasia". Harakati zozote za namna hiyo, kutokana na mtazamo wa wanachama kwao - wahaini, wanafiki, wasaliti, wahujumu, wazandiki - itakuwa ni nguvu hasi ya kuharibu chama kuliko kukijenga.
Vinginevyo kama Zitto hawezi kuomba radhi, ni vema ajiandae kwa maisha nje ya CHADEMA aidha kwa kufukuzwa au kutoka mwenyewe atakapoona ndoto zake za kisiasa hazitatimia, ingawa kilicho bora ni kutoka kwa hiari ili athibitishe mapenzi yake kwa chama hicho. Wanasema umpendae utamlinda.
Nitamuelewa Zitto iwapo akiamua kuing'ang'ania CHADEMA ili asipoteze ‘neema mbalimbali' ambazo msingi wake ni uanachama, kama ubunge na uongozi wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC). Kupoteza vyeo hivyo kunaweza kumpoteza katika siasa. Kwa maana hiyo hesabu za kung'ang'ania CHADEMA kwa sasa akinunua muda zinalipa.
Nje ya CHADEMA, Zitto ana uchaguzi wa aina nne. Aache siasa, ajiunge na CCM, aunde chama chake ama ajiunge na vyama vingine vya upinzani. Kuacha siasa si rahisi, itakuwa ni kukubali kushindwa kirahisi. Kujiunga na CCM litakuwa kosa kubwa kwani atakuwa amethibitisha dhana iliyojengeka kuwa ni mtu wao. Kuanzisha chama kutampotezea muda mwingi.
Chaguo lenye mantiki ni kuhamia chama kingine cha upinzani. Miongoni mwa vyama vya upinzani, huenda Zitto akaishia NCCR Mageuzi. Akienda CUF anaweza kwa urahisi kumrithi Profesa Ibrahim Lipumba lakini atajitwisha jukumu zito la kuondoa dhana kuwa ni chama cha Waislamu.
Athari kwa CHADEMA?
Wanaoamini kuwa CHADEMA itaathirika kwa kuondoka Zitto wanakosea kwani athari za mvutano uliopo sasa ni mbaya kuliko wanachama itakaowapoteza kwa kuondoka Zitto.
Hata hivyo, baada ya mnyukano huu kupita na hususan baada ya kujiuzulu kwa Makamu Mwenyekiti, Said Arfi, CHADEMA inapaswa kupambana zaidi ili kukubalika maeneo ya Waislamu wengi ili iweze kuondoa dhana kuwa ni chama wa Wakrito. Kadhalika, CHADEMA itapaswa kutafuta uwiano mzuri katika safu yake ya uongozi ili kuondoa fikra kuwa chama hicho ni cha kikanda.
Katika minyukano hii ya kisiasa, jambo moja muhimu tunalojifunza ni kuwa dini na ukanda ni uhalisia ulipo katika siasa zetu na ni bora tuvikubali kama vigezo muhimu vya uchambuzi wa utendaji wa siasa zetu. Tukiukubali ukweli huu mapema ni faida yetu. Tanzania hii si ile ya Mwalimu Nyerere.
Nimalize kwa kuhoji kuhusu njia iliyotumika kuukamata waraka wa siri wa Mwigamba, Kitila na wenzake. Kama habari kuwa alinyang'anywa laptop yake ni kweli, hivi tukinyang'anya laptop za viongozi wote wa CHADEMA au vyama vya siasa na kupekua, kuna atakayesalimika na uhaini, uhujumu, mbinu chafu na kadhalika?
BY Njonjo Mfaume
ZITTO kusema atakuwa wa mwisho kuhama CHADEMA alikuwa na maana yake. Anajua nafasi yake ndani ya CHADEMA. Kama kweli SLAA na MBOWE wanajiamini, basi na wamfukuze kama ambavyo waliahidi, siku kumi na nne hazijaisha?
ZITTO kawatega hao madikteta aone watachukua hatua jambo ambalo hawawezi kuthubutu hata kwa sekunde moja.
 
Kibanga Ampiga Mkoloni

Kibanga Ampiga Mkoloni

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2007
Messages
16,595
Likes
3,150
Points
280
Kibanga Ampiga Mkoloni

Kibanga Ampiga Mkoloni

JF-Expert Member
Joined Aug 9, 2007
16,595 3,150 280
USHAHURI MZURI. hongera kwa KUJITAMBUA!
 
manning

manning

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2013
Messages
3,528
Likes
116
Points
160
manning

manning

JF-Expert Member
Joined Apr 1, 2013
3,528 116 160
ZITTO kusema atakuwa wa mwisho kuhama CHADEMA alikuwa na maana yake. Anajua nafasi yake ndani ya CHADEMA. Kama kweli SLAA na MBOWE wanajiamini, basi na wamfukuze kama ambavyo waliahidi, siku kumi na nne hazijaisha?
ZITTO kawatega hao madikteta aone watachukua hatua jambo ambalo hawawezi kuthubutu hata kwa sekunde moja.
mamba ana nguvu akiwa majini akiondoka kazi kwisha. Na kwa tamaa na utata wa ZZK namtabilia kuptea kabisa katika siasa kama Masumbuko Lamwai.
 
M

Malili

Member
Joined
Aug 17, 2011
Messages
48
Likes
0
Points
13
M

Malili

Member
Joined Aug 17, 2011
48 0 13
Aondoke tu, na kuisha kama Walidi Kabul, Nswansugwako ......................na wengine atapotea tu. na aende kwa amani
 
Ruttashobolwa

Ruttashobolwa

JF-Expert Member
Joined
Feb 22, 2012
Messages
45,871
Likes
16,329
Points
280
Ruttashobolwa

Ruttashobolwa

JF-Expert Member
Joined Feb 22, 2012
45,871 16,329 280
Sitoki chadema labda wao wanifukuze-zitto.

Mnataka zitto atoke ili slaa akope tena bila riba na hakuna wa kuhoji?

Mnataka zitto atoke chadema sababu mmeandaa wa kuwatonya?
 
F

Farudume

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2013
Messages
3,916
Likes
2,947
Points
280
Age
32
F

Farudume

JF-Expert Member
Joined Jan 10, 2013
3,916 2,947 280
ZITTO kusema atakuwa wa mwisho kuhama CHADEMA alikuwa na maana yake. Anajua nafasi yake ndani ya CHADEMA. Kama kweli SLAA na MBOWE wanajiamini, basi na wamfukuze kama ambavyo waliahidi, siku kumi na nne hazijaisha?
ZITTO kawatega hao madikteta aone watachukua hatua jambo ambalo hawawezi kuthubutu hata kwa sekunde moja.
Mpaka dakika hii Zitto hana tena Madhara kwa CDM ni sawa na Shibuda.
 
M

mjogoro

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2011
Messages
248
Likes
27
Points
45
Age
34
M

mjogoro

JF-Expert Member
Joined Feb 18, 2011
248 27 45
ZITTO kusema atakuwa wa mwisho kuhama CHADEMA alikuwa na maana yake. Anajua nafasi yake ndani ya CHADEMA. Kama kweli SLAA na MBOWE wanajiamini, basi na wamfukuze kama ambavyo waliahidi, siku kumi na nne hazijaisha?
ZITTO kawatega hao madikteta aone watachukua hatua jambo ambalo hawawezi kuthubutu hata kwa sekunde moja.
naon unaharishaharisha tu, vp ulimpigia kura ktk ile poll ya hapa jf? mbona mmemuacha zitto anadhalilika kiasi kile?
 
F

fikirikwanza

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2012
Messages
6,590
Likes
663
Points
280
F

fikirikwanza

JF-Expert Member
Joined Jan 25, 2012
6,590 663 280
Aende huku kwa bwana wakubwa zake
 
Masanilo

Masanilo

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2007
Messages
22,300
Likes
230
Points
160
Masanilo

Masanilo

JF-Expert Member
Joined Oct 2, 2007
22,300 230 160
Fukuuuuza kiiiima huyo
 
waza_makubwa

waza_makubwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 9, 2012
Messages
216
Likes
47
Points
45
waza_makubwa

waza_makubwa

JF-Expert Member
Joined Jul 9, 2012
216 47 45
HIVI karibuni nilishuhudia mmoja wa rafiki zangu hapa Shanghai akiachwa na mpenzi wake kupitia ‘skype’ pale alipoambiwa na mpenzi wake huyo kuwa amekutana na kumpenda mwanamume mwingine.
Binti yule anayeishi Italia, alimwambia kuishi mbalimbali kunafanya uhusiano wao huo kutowezekana. Wawili hawa walikutana Afrika Kusini wakati wote wakiishi huko na baadaye walitawanyika, mmoja China mwingine Italia kwa ajili ya masomo.
Rafiki yangu, Michael, alishtuka kwani hakutegemea hilo, alimjibu binti kwa huzuni,“Nakupenda sana, ila nataka uwe na furaha na kwa sababu hiyo siwezi kuwa kikwazo katika kuitafuta furaha yako. Nakutakia kila la kheri. Niko radhi”.
Huenda hivi ndivyo ambavyo Zitto Kabwe anapaswa kufanya katika muktadha wa mgogoro uliojitokeza karibuni katika uhusiano wake na chama chake cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Mgogoro huo, uliouza magazeti, uliisukuma Kamati Kuu ya Chama hicho kumvua mwanasiasa huyo kijana nyadhifa zake zote za uongozi ndani ya chama ikiwemo unaibu katibu mkuu na kumpa siku 14 kujieleza kwa nini asivuliwe uanachama.
Kutokana na uamuzi huo wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Zitto alikutana na waandishi wa habari na kutangazia kuwa anaipenda CHADEMA kiasi kwamba angependa hata mwanawe siku moja naye aje kuwa mwanachama.
Lakini, busara za Zitto katika uamuzi zilitofautiana na za rafiki yangu Michael. Zitto ameamua kung’ang’ania na kukataa kutalikiana na CHADEMA licha ya kukiri kuipenda. Kwa maneno yake anasema atakuwa wa mwisho kutoka CHADEMA kwa hiari.
Kutoka katika mtazamo wa mchambuzi huru, nisiye na upande, naamini Zitto kama kweli anaipenda CHADEMA, uamuzi sahihi ulikuwa ni kutoka na sio kubaki.
Swali la msingi la kujiuliza, kufuatia maoni ya viongozi waandamizi wa CHADEMA ni kwanza, je kwa Zitto kuendelea kuwepo ndani ya CHADEMA kutaisaidia au kuiangamiza CHADEMA? na pili, je, kwa hali ilivyo ndani ya CHADEMA, ndoto za Zitto za kuitumikia nchi yake na kufikia malengo yake binafsi ya kisiasa zinaweza kufanikiwa?
Ni wazi kuwa hisia, chuki na upinzani ndani ya CHADEMA dhidi ya Zitto, falsafa yake na walio nyuma yake ni kubwa na dhahiri. Baadhi ya viongozi waandamizi, wakiwemo wabunge wanamkosoa kila wanapopata jukwaa zuri la kufanya hivyo.
Unaweza kusema makundi na watu kutofautiana mitazamo ni kawaida katika vyama. Lakini inapofikia hatua ya kuitana ‘mnafiki’, ‘mzandiki’, ‘mhaini’, ‘msaliti’, ‘mchonganishi’, ‘mzushi’, ‘muongo’ na mengine mengi ni ishara ya uadui na kutoaminiana. Kwenye ndoa hizi ni tofauti zisizosuluhishika.
Katika akaunti yake ya Facebook, Joseph Mbilinyi, Mbunge wa Mbeya Mjini aliandika, “Big up sana kamati kuu CDM...there should be no room for SNITCHES (wazandiki) huku Peter Msigwa akiandika “…kila harakati huzalisha mashujaa kwa ajili ya cause, pia huzalisha wasaliti, lakini mara zote historia inaonyesha wasaliti walishindwa.”
Ingawa hakukutajwa majina, wote tunaelewa nani analengwa katika muktadha wa yanayotokea ndani ya chama hicho.
Zitto, kwa upande wake amewaita wapinzani wake kuwa ni wahafidhina, wabadhirifu na watukuzao siasa majitaka huku mwenyewe na kundi lake wakijitambulisha kama wapenda demokrasia, waumini wa uwajibikaji na wapenda siasa safi. (Rejea waraka taarifa yake yakujibu tuhuma).
Kutoaminiana na hisia hizi za kuwa kundi moja ni la wasaliti, wahaini inafanya tofauti ya mitazamo kuwa kubwa mno. Aina hii ya tofauti, ambayo hujitokeza mara kwa mara katika siasa za Tanzania sio tena chachu ya maendeleo bali ni nguvu hasi ya kukirudisha nyuma chama.
Ni kwa kuzingatia hilo ndio maana Zitto anapaswa kutoka CHADEMA, bila kujali kama atafukuzwa ama laa. Kwa kutoka, Zitto atakuwa amedhihirisha mapenzi yake kwa hicho. Kutoka kwake kutaleta utulivu. Uwepo wake ndani ya CHADEMA hautosaidia chama hicho ambacho ni wazi kuwa viongozi, wanachama na wafuasi wengi hawana imani naye tena.
Zitto anapaswa kufuata maono na ushauri wa mama yake ambaye baada ya Zitto kuvuliwa uanachama alinukuliwa akishukuru akiamini ni hatua nzuri kwa usalama wa mwanawe. Shida Salum, kama ambavyo anajulikana ambaye naye amekuwa ni miongoni mwa viongozi walio mstari wa mbele wa CHADEMA, alinukuliwa akisema kilichomkuta mwanaye kimefunika mabaya mengi yaliyopangwa afanyiwe ili amalizwe. Maoni haya yanatoa msukumo zaidi kwa Zitto kuona umuhimu wa kukaa pembeni.
Na ieleweke kuwa waraka wa siri ni moja tu kati ya shida nyingi zinazofanya mgogoro wa ndoa ya Zitto na CHADEMA uwe hausuluhishiki.
Zipo shutuma kuwa ushiriki wa Zitto katika shughuli za chama ni hafifu na kwamba kwenye matukio muhimu yenye maana ambayo ni ya kukijenga chama haonekani. Inatolewa mifano ya matukio makubwa ya uchaguzi Tarime na mikutano iliyoishia katika fujo na kuua watu huko Arusha, Iringa, Morogoro. Kuna tuhuma za kuuza majimbo, kuna tuhuma za kununuliwa na kwa kutumika na CCM na Idara ya Usalama wa Taifa ili kuhujumu CHADEMA na sasa hili la waraka wa siri!
Zitto amekuwa akijaribu kutoa changamoto ya kutolewa ushahidi wa tuhuma hizo, lakini nilitegemea akiwa mwanasiasa mzoefu, anapaswa kujua kuwa kwenye siasa, mtazamo ya watu ni muhimu kuliko ushahidi. Kama huaminiki, hakuna aina ya ushahidi itaondolea tuhuma.
Katika mkutano wa waandishi wa habari uliotumika kujibu hoja za Zitto na Dk. Kitila Mkumbo, mwanasheria wa CHADEMA Tundu Lissu na John Mnyika walijibu utetezi na madai ya Zitto na Dk. Kitila Mkumbo na kuwaita waongo na wazushi. Kwa waliyoyasema, ni wazi kuna uwezekano mkubwa wa CHADEMA kumfukuza uanachama Zitto ama sivyo, Zitto atakayebaki CHADEMA atakuwa ni mzigo kuliko msaada kwa chama na hata yeye binafsi hatoweza kutimiza ndoto zake.
Mustakabali wa Zitto
Zitto akitaka kubaki CHADEMA anachoweza kufanya ni kuomba radhi (bila kujali kama makosa anayotuhumiwa yana ushahidi au hapana) na pia kukubali kuachana na dhamaira yake ya kugombea uenyekiti au nafasi nyingine za juu za uongozi katika chama hicho.
Hili likitokea litafurahisha wengi hususan sauti za busara ndani ya chama kama Profesa Mwesiga Baregu, ambaye amesikitika akitahadharisha uongozi ufikirie mara mbili kabla ya kuchukua hatua zaidi dhidi ya Zitto na wenzake hasa ukizingatia pamoja na mapungufu yao wamekifanyia mengi chama.
Lakini kiuhalisia haileti maana Zitto kuomba radhi na kukubali kuachana na ndoto zake za kuleta mageuzi ya kiungozi. Zitto atakuwa anauishi uongo ukizingatia kuwa ni wazi anaamini kuwa uongozi wa sasa hautoshi na una mapungufu mengi na makubwa mno.
Kwa maana nyingine ni kwamba Zitto na Kitila hata wakiomba radhi hawawezi kuacha harakati za mapambano yao wanayoyaita ya kuleta “mabadiliko makubwa katika uongozi wa juu wa chama na kuleta demokrasia”. Harakati zozote za namna hiyo, kutokana na mtazamo wa wanachama kwao - wahaini, wanafiki, wasaliti, wahujumu, wazandiki - itakuwa ni nguvu hasi ya kuharibu chama kuliko kukijenga.
Vinginevyo kama Zitto hawezi kuomba radhi, ni vema ajiandae kwa maisha nje ya CHADEMA aidha kwa kufukuzwa au kutoka mwenyewe atakapoona ndoto zake za kisiasa hazitatimia, ingawa kilicho bora ni kutoka kwa hiari ili athibitishe mapenzi yake kwa chama hicho. Wanasema umpendae utamlinda.
Nitamuelewa Zitto iwapo akiamua kuing’ang’ania CHADEMA ili asipoteze ‘neema mbalimbali’ ambazo msingi wake ni uanachama, kama ubunge na uongozi wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC). Kupoteza vyeo hivyo kunaweza kumpoteza katika siasa. Kwa maana hiyo hesabu za kung’ang’ania CHADEMA kwa sasa akinunua muda zinalipa.
Nje ya CHADEMA, Zitto ana uchaguzi wa aina nne. Aache siasa, ajiunge na CCM, aunde chama chake ama ajiunge na vyama vingine vya upinzani. Kuacha siasa si rahisi, itakuwa ni kukubali kushindwa kirahisi. Kujiunga na CCM litakuwa kosa kubwa kwani atakuwa amethibitisha dhana iliyojengeka kuwa ni mtu wao. Kuanzisha chama kutampotezea muda mwingi.
Chaguo lenye mantiki ni kuhamia chama kingine cha upinzani. Miongoni mwa vyama vya upinzani, huenda Zitto akaishia NCCR Mageuzi. Akienda CUF anaweza kwa urahisi kumrithi Profesa Ibrahim Lipumba lakini atajitwisha jukumu zito la kuondoa dhana kuwa ni chama cha Waislamu.
Athari kwa CHADEMA?
Wanaoamini kuwa CHADEMA itaathirika kwa kuondoka Zitto wanakosea kwani athari za mvutano uliopo sasa ni mbaya kuliko wanachama itakaowapoteza kwa kuondoka Zitto.
Hata hivyo, baada ya mnyukano huu kupita na hususan baada ya kujiuzulu kwa Makamu Mwenyekiti, Said Arfi, CHADEMA inapaswa kupambana zaidi ili kukubalika maeneo ya Waislamu wengi ili iweze kuondoa dhana kuwa ni chama wa Wakrito. Kadhalika, CHADEMA itapaswa kutafuta uwiano mzuri katika safu yake ya uongozi ili kuondoa fikra kuwa chama hicho ni cha kikanda.
Katika minyukano hii ya kisiasa, jambo moja muhimu tunalojifunza ni kuwa dini na ukanda ni uhalisia ulipo katika siasa zetu na ni bora tuvikubali kama vigezo muhimu vya uchambuzi wa utendaji wa siasa zetu. Tukiukubali ukweli huu mapema ni faida yetu. Tanzania hii si ile ya Mwalimu Nyerere.
Nimalize kwa kuhoji kuhusu njia iliyotumika kuukamata waraka wa siri wa Mwigamba, Kitila na wenzake. Kama habari kuwa alinyang’anywa laptop yake ni kweli, hivi tukinyang’anya laptop za viongozi wote wa CHADEMA au vyama vya siasa na kupekua, kuna atakayesalimika na uhaini, uhujumu, mbinu chafu na kadhalika?
BY Njonjo Mfaume

asante kwa maono yako, pia kuna waraka mwngne unasambazwa, ukiupata itapendeza urudie uchambuzi
 
Mchoraji Cyper255

Mchoraji Cyper255

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2012
Messages
1,476
Likes
5,161
Points
280
Mchoraji Cyper255

Mchoraji Cyper255

JF-Expert Member
Joined Nov 21, 2012
1,476 5,161 280
Huyu Jamaa ni ----- na ni shabiki wa CHADEMA wa dhati Kabisa.
Eti atoke!!😀
Je, Mandela baada ya kuwekwa lupango Kisha akahachana na Siasa angekuwa Rais wa Kwanza wa S A?
Hizo ni Changamoto kuelekea kwenye Mafanikio. Acha apigane mpaka ashike uenyekiti.
 
Mchoraji Cyper255

Mchoraji Cyper255

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2012
Messages
1,476
Likes
5,161
Points
280
Mchoraji Cyper255

Mchoraji Cyper255

JF-Expert Member
Joined Nov 21, 2012
1,476 5,161 280
Unapopigania kitu na ukionyesha kufanikiwa hakuna anaependa. Watakuwekea vikwazo vya kushindwa. Hupaswi kukata tamaa Kabisa. Ongeza juhudi na utafanikiwa.

SIO USEME 'ATOKE'. AKITOKA HALAFU IWEJE SASA.
 
Forum statistics

Threads 1,251,618
Members 481,811
Posts 29,777,965