Lekanjobe Kubinika
JF-Expert Member
- Dec 6, 2006
- 3,019
- 580
Mimi sina tatizo na uhuru wa mawazo. Sina tatizo kabisa na kauli ya zito. Ni haki yake kikatiba na nina heshimu mawazo yake. TATIZO KUBWA NILILOKUWA NAO NI MUDA ZITTO ANAOTUMIA KUTOA MAWAZO YAKE. Chunguza utaliona hili. Zitto anapenda kutoa kauli zake kipindi ambacho chama chake kipo kwenye harakati fulani. ALIWAHI PIA KUTOA KAULI YA URAISI KWENYE JIMBO LAKE WAKATI BADO UCHAGUZI WA RAISI UNAENDELEA 2010. kwa hili watu wote wenye kupenda kuchambua na kuangalia vitu kwa undani si walaumi kwa KUMUITA HUYU JAMAA MNAFIKI. Angalia hata kampeni za uraisi 2010 alishiri kwa kiasi gani?
ndio maana nikasema anapayuka alfajiri sana.....achilia mbali kauli aliyotoa kipindi cha uchaguzi 2010..kuna ile nyinge alitoa wakati wa msiba wa regia....na hii ya sasa.....anautaka uraisi huku akiwanga wengine ..eti mnyika alikuwa haipendi chadema kabisa na hata kujiunga nayo alikuwa hataki......haya si maneno mazuri ya kusema......mrafi tu
Mimi sina tatizo na uhuru wa mawazo. Sina tatizo kabisa na kauli ya zito. Ni haki yake kikatiba na nina heshimu mawazo yake. TATIZO KUBWA NILILOKUWA NAO NI MUDA ZITTO ANAOTUMIA KUTOA MAWAZO YAKE. Chunguza utaliona hili. Zitto anapenda kutoa kauli zake kipindi ambacho chama chake kipo kwenye harakati fulani. ALIWAHI PIA KUTOA KAULI YA URAISI KWENYE JIMBO LAKE WAKATI BADO UCHAGUZI WA RAISI UNAENDELEA 2010. kwa hili watu wote wenye kupenda kuchambua na kuangalia vitu kwa undani si walaumi kwa KUMUITA HUYU JAMAA MNAFIKI. Angalia hata kampeni za uraisi 2010 alishiri kwa kiasi gani?
Mtoa mada yupo sahihi zito hafai
Mbunge mahiri na machachari kutoka chama makini Zitto Zuberi Kabwe ameweka wazi kuwa anautaka uraisi lakini akiwa atapata ridhaa kutoka kwa chama chake na wananchi kwa ujumla wao,
CHANZO: UDADISI: Rethinking in Action: ZITTO: "NDIO NATAKA KUWA RAIS"
huwezi kuamka asubuhi kabla hata hujapiga mswaki unaanza kupayuka..''mimi ni mpole''mimi ni mtu mwema sana, ninafaa.. nimekijenga chama toka nina miaka 16..mimi ndio nimekifikisha hapo kilipo ...ni mimi na mbowe tu ndio tuliokuwa tunakesha...nafaa jamani...wanaokuona ndio wanaweza kusema hivyo kama wewe ni mpole au mkali, jasiri au muoga......kama zitto anafaa hakuna haja ya kusimama kwenye kingo za barabara juu ya kilima alfajiri yote hii na kuanza kupayuka kuwa yeye ni mtu mwema na anafaa kuwa rais wa nchi......
hizi ni dalili za urafi ulipindukia...zitto hufai kuwa rais...take it or leave it
Lakini kusema kwa Kabwe kuhusu hamu yake ya kuwa rais ina ubaya gani? Kila mtu anayo ndoto yake, wengine hukaa kimya na ndoto zao na wengine huropoka hadharani. Hata aliyeko madarakani alikuwa na ndoto ya urais, ndio maana baba wa taifa alimnyamazisha baada ya kuona anasemasema kuutaka urais wakati huo baba wa taifa alishaona muda bado na kumbe ni kweli, si mnaona anachofanya sasa? Ni rafiki yake sana Kabwe, kwa hiyo akiukwaaa urais sitaona tofauti na aliyepo sasa, watabaki kulindana na kuhamasishana utundu wa kuchanga karata za kuiona siku inapita hata kama kwa mazingaombwe.
Kama alivyotumia haki yake kuongea Kabwe, huyo Yeriko naye katumia haki yake kutoa uchambuzi juu ya mambo yaliyoanikwa na Kabwe ili yachambuliwe kwa faida ya walaji ambao ni umma. Wabaya sio wanaoomba bali wabaya ni wale wawapao waombaji ambao wanaonekana wazi kwamba hawahitajiki kupewa sasa. Urais sio kuwa msomi ingawa inasaidia, lakini wapo wasomi wengi wanavurunda kila kukicha. Tusipendelee kusikia yale tunayoyataka tu, siasa ni pamoja na kuvumiliana kwa kusikia yanayotuumiza. Cha msingi ni kujenga hoja na kuhakikisha hoja yako yenye mshiko inapita.
Huyu yericko naye ni mmoja wa wanafamilia ya nyerere?
jibu swali ,inawezekana wewe ni mkenya umetumwa tutajuajeSwali lako halina mafaa kwa taifa! Jadili hoja iliyombele yetu!
Hatimaye sasa nimejiridhisha pasipo na shaka ni kwa nini zitto Kabwe ni swahiba mkubwa wa Deputy Director wa Usalama wa Taifa ndugu Jacky Nzoka, Zitto aje hapa kuuelezea umma wa JF ni sababu zipi za msingi zilizokuwa zinamfanya awe na mawasiliano ya mara kwa mara wakati chama chake kiko katika uchaguzi mkuu na Idara ya usalama wa Taifa ndiyo ilikuwa inaihujumu CHADEMA? hapa sitalajii jibu rahisi kwa swali gumu.
Pili Ben Saanane nimekuwa nikifuatilia mabandiko yako kwa makini sana na kuna kipindi nilidhani huwa unaonewa, kumbe nilikuwa najidanganya, humu jamvini umejipambanuwa kwamba wewe ndio unayejuwa siasa na yeyote ambaye atakuwa kinyume na mtazamo wako basi wewe utambatiza kila aina ya jina mara mnafki mara hivi mara vile, kumbe sasa nimejiridhisha ni kweli chama chako kiliposema huna maadili hakuna walipokuwa wamekosea, kwa nini unatetea Alliance ndani ya chama? narudia kukwambia tena jifunze kwa John Mnyika, yule kijana anaaminika machoni pa watu kwa sababu he is humbled,......jiulize ni kwa nini kijana mmoja Mnyika alundikiwe vyeo na nyinyi wasomi mpo? endelea na Alliance. zako.