Zitto: Namsubiri Mbowe Mahakamani

Zitto: Namsubiri Mbowe Mahakamani

Status
Not open for further replies.
Mbunge wa kigoma kaskazini zitto Kabwe (Chadema), amesema anamsubiri mwenyekiti wa chama hicho, Freema mbowe mahakamani.
Zitto ametoa kauli hiyo baada mbowe kutangaza kumburuza mahakamani kutokana na kile kinachodaiwa kumzushia tuhuma za uongo
Nasema sitaki malumbano na kiongozi yoyote, nachotambua masuala ya mahakama yanajibiwa mahakamani na si vinginevyo" alisema zitto.

Zitto alitoa kauli hiyo, baada ya MTANZANIA kutaka kujua msimamo wake kutokana na kauli ya Mbowe kukududia kumshitaki, kutokana na madai ya kusema uongo dhidi yake. Zitto ambaye yupo nchini Nigeria anakohudhuria vikao vya kamati za Bunge za serikali kwa nchi za Afrika, alisema pamoja na Hali hiyo mahakama ndio njia pekee ambayo haki ya mtu inaweza kupatikana.
Alisema kwa msingi huo, hivi sasa hayuko tayari kuruhusu malumbano ambayo Hayana tija kwa Taifa.

" nipo Nigeria na bahati mbaya ninaumwa sana, ila hivi Leo ninamshukuru Mungu nimepata nafuu kidogo. Kama nilivyosema mwanzo sitaki Malumbano na mtu. Pamoja na kusema anaumwa, hakuwa tayari kufafanua ni ugonjwa gani unaomsumbua.

" huu muda nahitaji kutafakari maisha yangu kisiasa na kwa vyovyote vile masuala ya mahakamani yatajibiwa mahakamani", alisisitiza zitto
Nukuu za gazeti la Mtanzania ni za kichonganishi na zinalenga kutugawa watanzania. Sijui kwa nini na wewe unayebandika andiko hili hapa unafurahia kukiweka. Ukabira ni silaha ya mtu asiye na hekima na ni dalili ya ujinga.
 
Wachaga wamesoma wa mwandiga wanakesha ngomani na kuvua dagaa na vibarazani. Nani ampende kubwa zitto

Wewe angalia kabla hujabonyeza button kuandika..ushabiki wa kijinga kabisa kwa elimu mbowe hafikii hata robo ya zitto, kila mtu analijua hilo. Pili usijipumbaze kwani hao migebuka na dagaa hawatakiwi kuvuliwa? Muda mzuri wa kuvua ni usiku na sio mchana.. Jamani ushabiki usitufanye kuwa vituko lets think beyond and outside the box
 
Zito ni kama alitakiwa awe mwanamke kwani anapenda sana mipasho! Huyu ndie alitaka awe raisi? aazishe bendi ya taarabu ataweza!

We unaonekana hata sifa ya kuwa balozi huwezi, kwani hapo zitto ammepasha nani? Amesema hayo baada ya gazeti kumuuliza na sio kwamba ameropoka kama wewe, kwani mbona mbowe alipohojiwa na waandishi badala ya kujibu hoja alianza kutoa mipashe au ndio nyani haoni kundule, kama unania ya kuwa kiongozi baadae uwe unafikiria kwanza kabla ya kusema maana unaweza kutoa maamuzi yakakujeruhi we mwenyewe.
 
Mbunge wa kigoma kaskazini zitto Kabwe (Chadema), amesema anamsubiri mwenyekiti wa chama hicho, Freema mbowe mahakamani.
Zitto ametoa kauli hiyo baada mbowe kutangaza kumburuza mahakamani kutokana na kile kinachodaiwa kumzushia tuhuma za uongo
Nasema sitaki malumbano na kiongozi yoyote, nachotambua masuala ya mahakama yanajibiwa mahakamani na si vinginevyo" alisema zitto.

Zitto alitoa kauli hiyo, baada ya MTANZANIA kutaka kujua msimamo wake kutokana na kauli ya Mbowe kukududia kumshitaki, kutokana na madai ya kusema uongo dhidi yake. Zitto ambaye yupo nchini Nigeria anakohudhuria vikao vya kamati za Bunge za serikali kwa nchi za Afrika, alisema pamoja na Hali hiyo mahakama ndio njia pekee ambayo haki ya mtu inaweza kupatikana.
Alisema kwa msingi huo, hivi sasa hayuko tayari kuruhusu malumbano ambayo Hayana tija kwa Taifa.

" nipo Nigeria na bahati mbaya ninaumwa sana, ila hivi Leo ninamshukuru Mungu nimepata nafuu kidogo. Kama nilivyosema mwanzo sitaki Malumbano na mtu. Pamoja na kusema anaumwa, hakuwa tayari kufafanua ni ugonjwa gani unaomsumbua.

" huu muda nahitaji kutafakari maisha yangu kisiasa na kwa vyovyote vile masuala ya mahakamani yatajibiwa mahakamani", alisisitiza zitto

Amesahau aliposema hana hata jina moja la walioficha mabilion uswisss!

Ngoma ikivuma sana, hupasuka.
 
Mungu akulinde Zitto, Pigania nchi yako mpaka mwisho.

ImageUploadedByJamiiForums1389682603.739677.jpg
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom