Zitto: Namsubiri Mbowe Mahakamani

Zitto: Namsubiri Mbowe Mahakamani

Status
Not open for further replies.

mkigoma

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2011
Posts
1,180
Reaction score
309
Mbunge wa kigoma kaskazini zitto Kabwe (Chadema), amesema anamsubiri mwenyekiti wa chama hicho, Freema mbowe mahakamani.
Zitto ametoa kauli hiyo baada mbowe kutangaza kumburuza mahakamani kutokana na kile kinachodaiwa kumzushia tuhuma za uongo
Nasema sitaki malumbano na kiongozi yoyote, nachotambua masuala ya mahakama yanajibiwa mahakamani na si vinginevyo" alisema zitto.

Zitto alitoa kauli hiyo, baada ya MTANZANIA kutaka kujua msimamo wake kutokana na kauli ya Mbowe kukududia kumshitaki, kutokana na madai ya kusema uongo dhidi yake. Zitto ambaye yupo nchini Nigeria anakohudhuria vikao vya kamati za Bunge za serikali kwa nchi za Afrika, alisema pamoja na Hali hiyo mahakama ndio njia pekee ambayo haki ya mtu inaweza kupatikana.
Alisema kwa msingi huo, hivi sasa hayuko tayari kuruhusu malumbano ambayo Hayana tija kwa Taifa.

" nipo Nigeria na bahati mbaya ninaumwa sana, ila hivi Leo ninamshukuru Mungu nimepata nafuu kidogo. Kama nilivyosema mwanzo sitaki Malumbano na mtu. Pamoja na kusema anaumwa, hakuwa tayari kufafanua ni ugonjwa gani unaomsumbua.

" huu muda nahitaji kutafakari maisha yangu kisiasa na kwa vyovyote vile masuala ya mahakamani yatajibiwa mahakamani", alisisitiza zitto
 
Hamchoki kulumbana!!!!!??watu mna stamina ya migogoro!wengi tumechoka kelele zenu.
 
sasa wakili wa mbowe atakuwa nani?tundu lisu kashabwagwa na kijana msomi albert msando. au mbowe ataimgia dili lingine na nimrod mkono awe wakili wake
 
sasa wakili wa mbowe atakuwa nani?tundu lisu kashabwagwa na kijana msomi albert msando. au mbowe ataimgia dili lingine na nimrod mkono awe wakili wake
Unaweza kufanya kamchezo akapewa hela tena na mkono akahonge majaji ili kumkandamiza zitto.
 
Mara nyingi ukifanya argument na ndumilakuwili huwezi kushinda kwa kuwa atatafuta jambo la kukukera kisha atatumia mwanya huo kukushinda kwa kutumia uzoefu!
 
Nigeria kuna wachungaji bora kabisa Afrika!

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Zito kajibu safi.haya malumbano ya mbowe na zito kwaupande fulan naona watu wao wakaribu wanaowashauli sio wazuri.
 
Mbona Zitto watu wengi tumeshaanza kumsahau?

Siku hizi ukiweka habari yoyote Positive ya Zitto kwenye gaZeti lako hupati wanunuzi. Mfano Gazeti la Mwananchi, toka walipoanza kumpamba Zitto kwenye Gazeti lao mapato yalipungua zaidi ya nusu.
 
Ya... watu wanalilimia, lakini wakati wa mavuno wanalitupa nyuma ya nyumba...
Haliozi mkuu,msimu ukifika utalitafuta tu,ukitaka kuchimba shimo utalipigia magoti,kukwetua majani......mwe,jembe acha kabisa!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom