Zitto ataka wabunge wote walioko Dodoma wawekwe kwenye karantini

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,014
144,371
Ujumbe wake huu hapa chini kupitia twitter:

Wabunge wote mliopo Dodoma muwekwe karantini, mpimwe na mfuatiliwe ( contact tracing ). Minister Mwalimu there shall be no two set of laws - for MPs and for the people. Wabunge watengwe, wapimwe na wafuatiliwe. Tulishauri toka mwanzo kuwa Bunge lisiendelee na vikao. Ni hatari

Zitto.JPG
 
Wabunge wa Tanzania wengi ni wajinga sana jana pamoja na kwamba wanajifanya kusema bungeni hawajali kabisa jana nimekuta na mbunge eti anataka kunipa mkono yaani ananiamini kiasi gani mpaka anipe mkono.
Ni kujisahau mkuu tabia mpya inataka mazoea....

Leo nimekutana na jamaa yangu kaa maski afu anataka kunipa mkono....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari kutoka Bungeni Kama ilivotolewa na Naibu Spika Tulia ya kwamba kuna Mbunge mmoja amepatikana na maambukizi ya Covid-19 zinasikitisha,zinatisha na zinanyong'onyesha katika mapambano dhidi ya Covid-19!

Kabla ya Bunge kuanza watu walishauri Bunge liahirishwe kutokana na tishio la Covid-19. Lakini Spika Ndugai alikuja na hoja dhaifu za kuwa ATI Kuna mikakati imara itakayo wahakikishia Wabunge kuwa watakuwa salama wa salimini ndani ya mjengo!

Hata baada ya Bunge kuanza Kuna Wabunge wa Upinzani kina Mh.Mbowe.Lema, Halima Mdee. Mch. Msigwa na Matiko WALISHAURI WABUNGE WAPIMWE KWANZA ILI KUJUA AFYA ZAO KABLA YA KUENDELEA NA KIKAO. Siku zote Wapinzani hata wakiwa na hoja yenye mashiko inawekwa kapuni!!

Sasa basi kwa Hali hii Mhe. Job Ndugai Spika wa Bunge la JMT na Tulia Ackson Naibu wa Spika mpigieni simu Rais Magufuli kumtaarifu kuwa maji yamezidi Unga na Ni LAZIMA BUNGE LIAHIRISHWE MARA MOJA NA WABUNGE WOTE WAPIMWE COVID-19 NA WAENDE QUARANTINE YA SIKU 14.

Nje ya hapo ni kutaka kuliangamiza Taifa kwa UZEMBE ulio wazi na dhahiri na kwa hili CCM mtawajibika mbele za Mungu na Watanzania wote.

Nawasilisha.
 
Ujumbe wake huu hapa chini kupitia twitter:

Wabunge wote mliopo Dodoma muwekwe karantini, mpimwe na mfuatiliwe ( contact tracing ). Minister Mwalimu there shall be no two set of laws - for MPs and for the people. Wabunge watengwe, wapimwe na wafuatiliwe. Tulishauri toka mwanzo kuwa Bunge lisiendelee na vikao. Ni hatari
Au bunge livunjwe tu!
 
Back
Top Bottom